FAO kusimamia mradi wa kuendeleza matumizi ya mazao ya bahari

Kusikiliza /

matumizi ya mazao ya bahari

Mradi mkubwa wa kimataifa wenye lengo la kuongeza uelewa zaidi wa nafasi ya mazao ya bahari katika kukabiliana na uhaba wa chakula kwa mamilioni ya wakazi maskini kwenye nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini umeanzishwa na Umoja wa Ulaya na utadumu kwa miaka mitatu chini ya usimamizi wa shirika la chakula duniani, FAO.

Mradi huo utakaogharimu Euro Milioni Moja utahusisha mashirika ya 20 ya maendeleo ya kimataifa, serikali, na vyuo vikuu na utajengea uwezo nchi zenye uhaba wa chakula katika mabara hayo kutengeneza sera endelevu kwa ajili ya kuimarisha maisha ya mamilioni ya wakazi wake masikini kupitia mazao ya baharini. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031