FAO, ECOWAS na Ujerumani kushirikiana kutokomeza njaa Afrika Magharibi

Kusikiliza /

kutokomeza njaa Afrika magharibi

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS na Ujerumani zimezindua mradi wa pamoja wa kuhakikisha kuna utashi wa kisiasa na ushiriki mkubwa wa serikali na wadau katika kutokomeza njaa Afrika Magharibi.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO, José Graziano da Silva amesema mradi huo wa miaka mitatu ni muhimu kwa kuwa utajumuisha katika mipango thabiti ya maendeleo ya kilimo barani Afrika, CAADP haki ya kupata chakula na utakuwa mfano kwa nchi zingine za Afrika na Asia.

Amesema wakati takwimu za dunia zinaonyesha njaa imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, idadi ya wenye njaa imeongezeka kutoka watu Milioni 170 hadi Milioni 234.

Katika mradi huo Ujerumani inatoa dola Milioni 2.4 huku Kamishna wa ECOWAS Lapodini Atouga akisema kuwa wao pamoja na kuchangia gharama zinazobakia watahakikisha nchi zote wanachama zinashiriki kikamilifu mradi huo unaokwenda sambamba na azma ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kutokomeza njaa duniani aliyoanzisha kwenye mkutano wa Rio + 20.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031