Cameroon na Nigeria ni mfano wa kuigwa katika kutatua mgogoro wa mpaka: Ban

Kusikiliza /

raia wa Cameroon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesifu kitendo cha Nigeria na Cameroon cha kuheshimu uamuzi uliotolewa miaka Kumi sasa juu ya mgogoro wa mpaka baina yao kwenye rasi ya Bakassi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ban imemkariri Katibu huyo akisema kuwa kitendo cha kukubali uamuzi huo uliotolewa na mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ ni mfano wa kuigwa kwa nchi zingine zinazokumbwa na changamoto za migogoro ya mipaka.

Mgogoro wa mpaka kati ya Nigeria na Cameroon ulizua mzozo mkubwa hadi mchakato ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa kumaliza mgogoro huo ulipohitimishwa na uamuzi wa ICJ mwaka 2002 na Nigeria ikatambua mamlaka ya Cameroon katika rasi ya Bakassi na kuwa eneo moja la mpaka.

Hata hivyo Ban amezisihi Cameroon na Nigeria kufikia makubaliano ya mpaka sahihi katika eneo lingine lililobakia la kilometa 200 huku akisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa uko nao katika kuzisaidia kutekeleza uamuzi wa ICJ.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930