Brazil inaweza kulinda mazingira kwa kuiga mfano wa Afrika kusini wakati wa kombe la dunia: UNEP

Kusikiliza /

Brazil FIFA

Wakati Brazil inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 na yale ya Olimpiki mwaka 2016, Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limetoa ripoti inayoonyesha ufanisi wa kulinda mazingira ulotokana na kombe la dunia Afrika Kusini mwaka 2010, na kile kinachoweza kuigwa kutokana nao ili uendelezwe kwenye michuano ya Brazil.

Ripoti hiyo inayotokana na uchunguzi huru, imeonyesha kuwa uvukaji wa hewa chafu ya kaboni kwenye anga katika mashindano ya kombe la dunia 201, ilikuwa chini zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hali hii ilitokana na kuwa wageni katika mashindano hayo walikuwa wachache zaidi ya waliotarajiwa, wageni walitumia magari kwa pamoja, na viwanja vya michezo viliundwa kuwa na uwezo wa kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 30. Matumizi ya nishati ya miale ya jua, au sola, pia yalichangia hali hii, imesema ripoti hiyo.

Awali, ilitarajiwa kuwa viwango vya kaboni angani kutokana na mashindano ya Afrika Kusini vingefikia tani bilioni 2.64, lakini ni tani milioni 1.65 tu ndizo zilitokana nayo. Kwa mtazamo wa mbele, UNEP imetia saini mkataba na serikali ya Brazil kusaidia kufanya viwanja vya michezo itakayofanyika huko kuwa na uwezo wa kuendeleza mazingira safi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031