Bokova kumuwakilisha Ban kwenye mkutano wa Kinshasa

Kusikiliza /

Irina Bokova

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova anatarajiwa kumuakilisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 14 wa mataifa yanayozungumza lugha ya kifaransa mjini Kinshasa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ukiwa ndio mkutano wa kwa kwanza kuandaliwa eneo la Afrika ya kati.

Akizungumzia eneo la Sahel ambapo watu milioni 20 wameathiriwa na uhaba wa chakula , ambapo usalama wa mabadiliko ya hali ya hewa, ukame pamoja misukosuko ya kisiasa imechochoea ghasai, Bokova ametoa wito wa kuwepo ushirikiano kukabiliana na hali iliyopo. Mkutano huo unafanyika kila baada ya miaka miwili unawaleta pamoja marais na maafisa wa serikali wa nchi zinazotumia lugha ya kifaransa kama lugha ya kitaifa. Lengo la Mkutano huo ni kuunga mkono maadili ya nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa na kuleta ushirikiano kati yao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930