Bei ya chakula ilipanda kwa asilimia 1.4 mwezi Septemba: FAO

Kusikiliza /

bei ya vyakula

Bei ya chakula duniani ilipanda kwa asilimia 1.4 mnamo mwezi Septemba, limesema Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Shirika hilo la FAO limesema kuwa kiwango hicho kipya, ambacho ni ongezeko la pointi 3, kimefikiwa baada ya miezi miwili ya kutobadilika, kwa sababu ya kuimarika kwa bei ya bidhaa za maziwa na nyama.

Kiwango hicho cha bei, ambacho ni kipimo cha bei ya kapu moja la bidhaa za chakula zinazouzwa kimataifa, kilipanda kutoka pointi 213 mwezi Agosti hadi pointi 216 Septmeba. Hata hivyo, shirika la FAO linasema bei ya nafaka haikuongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa upande mwingine, bei ya sukari na mafuta ya kupikia ilishuka.

Utabiri wa hivi karibuni wa FAO unaonyesha kuwa uzalishaji wa nafaka mwaka huu utapungua kwa asilimia 2.6 hadi tani milioni 286, ikilinganishwa na rekodi ilowekwa mwaka 2011. Hata hivyo, uzalishaji wa nafaka unatarajiwa kupanda katika mataifa ya vipato vya chini na uhaba wa chakula.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031