Rwanda, Argentina, Australia, Luxembourg, na Jamhuri ya Korea zachaguliwa kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza /

kupiga kura katika baraza kuu

Nchi za Rwanda, Argentina, Australia, Luxembourg, na Jamhuri ya Korea, leo zimechaguliwa kama wanachama wasio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Uchaguzi huo umefanyika katika kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Wanachama hao wasio wa kudumu watahudumu kwa kipindi cha miaka miwili, kuanzia Januari 1 mwaka 2013.

Jamhuri ya Rwanda imechaguliwa kama mwakilishi wa bara la Afrika, huku Argentina ikichaguliwa kuliwakilisha bara la Amerika ya Kusini na eneo la Karibi. Jamhuri ya Korea, imechaguliwa kuyawakilisha maeneo ya Asia na Pasifiki; huku Australia, na Luxembourg, zikichaguliwa kuwakilisha maeneo mengine na Magharibi mwa Ulaya.

Ingawa wanakaa kwenye vikao vya Baraza la Usalama, wanachama wasio wa kudumu hawana kura ya veto kwenye Baraza hilo. Uwezo huo umo mikononi mwa wanachama wa kudumu, ambao ni Marekani, Ufaransa, Uchina, Uingereza na Urusi.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031