Ban ataka kuongeza kasi ya mchakato wa kisiasa Sri Lanka ili kubaini kiini cha vita vilivyodumu kwa muda mrefu

Kusikiliza /

Mahinda Samarasinghe na Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa mchakato wa haraka wa kisiasa ili kujadilia na kubaini kiini cha kuzuka kwa vita vya kiraia nchini Sri Lank, vilivyomalizika miaka mitatu iliyopita kwa serikali kuibuka mshindi dhidi ya kundi la waasi la Tamil.

Ban amesema hayo wakati alipokutana na waziri wa viwanda wa Sri Lank Mahinda Samarasinghe,mjini New York. Ban alipongeza juhudi zinazochukuliwa na serikali ya Sri Lank lakini akataka kuongezwa juhudi zaidi kukamilisha mchakato wa kuwarejesha kwenye maeneo yao ya kawaida raia waliokwenda mtawanyikoni.'

Vikosi vya serikali ya Sri Lank vilitangaza kuwashinda waasi wa Tamil Tiger mwaka 2009 baada ya mapigano yaliyodumu kwa miongo kadhaa na kusababisha uharibifu wa maisha ya raia na mali zao.

Ban ameitaka serikali hiyo kurejesha moyo wa matumaini kwa raia wake hasa wakati huu ambapo taifa hilo linafufua upya vyombo vyake vya maamuzi na utawala.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031