Ban asikitishwa na athari za kimbunga Sandy

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema anafuatilia kwa karibu hatma ya kimbunga cha Sandy, ambacho kimesababisha vifo na uharibifu mkubwa katika maeneo ya Marekani na Karibi.

Akizungumza kutoka Incheon, Korea Kusini siku ya Jumanne, Bwana Ban amesema kimbunga hicho kimeathiri mamilioni ya familia, wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Amesema anawaza kuhusu wote wale wanaokabiliana na wakati mgumu uliosababishwa na kimbunga hicho. Ametuma risala  za rambi rambi kwa watu wa Haiti na kwingineko katika maeneo ya Karibi ambao wameathirika na kimbunga hicho kwa kupoteza watu wao.

Kimbunga cha Sandy kimeripotiwa kuwaua zaidi ya watu 100 Marekani, Haiti, Cuba, Jamaica, Bahamas, Jamhuri ya Dominica na Puerto Rico. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York yamefungwa tangu Jumatatu kwa sababu ya kimbunga hicho.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031