Ban apongeza Umoja wa Ulaya kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameupongeza Umoja wa Ulaya, EU kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2012 na kusema kuwa EU imekuwa ikizingatia misingi ya kuanzishwa kwake ambayo ni kujenga amani na umoja katika bara hilo lililosambaratishwa na vita kuu mbili za dunia.

Katika taarifa yake, Ban amesema mafanikio ya Umoja wa Ulaya ya kujenga amani ndani ya mipaka yake, kuweka mifumo bunifu ya majadiliano na utawala wa kisheria ni mfano wa kuigwa duniani kote.

Halikadhalika amesema Umoja wa Mataifa katika shughuli zake za kila siku hutegemea uongozi na ushiriki wa EU katika kushughulikia changamoto za sasa za dunia ikiwemo umaskini unaokabili mabilioni ya watu, misaada ya kibinadamu, haki za binadamu.

Kwa mantiki hiyo, Ban amesema ni matarajio yake kuwa ataendelea kuimarisha zaidi ushirikiano na Umoja huo wa Ulaya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031