Ban apongeza makubaliano ya amani ya Philippines

Kusikiliza /

ufilipino

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza kuunga mkono mpango wa usitishaji miongo kadhaa ya mapigano baina ya kundi la waasi na vikosi vya serikali nchini Philippines.

Serikali ya Philippnes imetiliana saini ya kuanzisha duru jipya la maelewano baina yake ya kundi la lijulikanalo the Moro Islamic Liberation Front (MILF) lenye ngome yake kusin mwa nchi hiyo lilipigana kujitenda na kuwa dola huru kwa miaka mingi

Katika ujumbe wake Ban amesifu makubaliano hayo na kuonyesha matumaini yake kuhusiana na mustakabala mpya kwa watu wa eneo la Mindanao ambao sasa watapata fursa ya kuwa dola lenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kisiasa.

Amesema kuwa makubaliano hayo ni hatua kubwa na tena yanaweka historia mpya kwa watu wa eneo hilo walioishi kwa kuhasimiana kwa miongo kadhaa. Ametaka kudumishwa kwa makubaliano hayo ya amani na ametaka pande zote kuheshimu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031