Ban alaani vikali shambulizi dhidi ya msichana wa Pakistan

Kusikiliza /

malala10

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo amelaani vikali shambulizi lililotekelezwa dhidi ya msichana mwenye umri wa miaka 14 ambaye amekuwa akipigania haki ya wasichana na wanawake nchini Pakistan kupata elimu, na kutaka walotekeleza kitendo hicho cha kikatili wafikishwe mara moja mbele ya vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, msichana huyo, Malala Yousufzai, ambaye alipinga vizuizi vya kundi la Taliban nchini Pakistan dhidi ya elimu ya wanawake, alikuwa katika hali mahtuti baadda ya kupigwa risasi kwenye shingo na kichwani hapo jana akitoka shule katika eneo la Swat Pakistan. Wasichana wengine wawili pia walijeruhiwa.

Wataliban wamedai kuwa ni wao walitekeleza shambulizi hilo, wakisema msichana huyo aliunga mkono nchi za magharibi na desturi za ng'ambo, na kwamba alikuwa akiwapinga. Kwa mujibu wa msemaji wake, Bwana Ban, kama watu wengi kote duniani, alitiwa moyo sana na juhudi za msichana huyo, za kuendeleza haki ya kimsingi ya elimu kwa wote.

Shirika la Kuhudumia Watoto la UNICEF, pia limelaani vikali shambulizi hilo, na kuelezea hofu yake kuhusu hali ya wasichana hao watatu. Mwingine aliyelaani vikali kitendo hicho ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na vita vya silaha, Leila Zerrougui

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031