Ban alaani mashambulizi kwenye makazi ya Dokta Mukwege huko Bukavu, DRC

Kusikiliza /

Dkt. Denis Mukwege

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashamublizi yaliotekelezwa leo usiku kwenye nyumba ya Dk Denis Mukwege, mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Panzi katika mji wa Bukavu ulioko mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

Msemaji wa Bwana Ban amemkariri Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akieleza kusikitishwa kwake na taarifa kuwa watu wenye silaha waliingia nyumba ya Dk Mukwege na familia yake, na kutisihia familia yake kwa bunduki na hatimaye kumuua mlinzi wake.

Bwana Ban amesema kazi ya ajabu inayofanywa na Dk Mukwege imeokoa maisha ya maelfu ya Wakongo wakiwemo maelfu ya wanawake na watoto waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia masharika mwa DRC na Daktari huyo anaendelea na kazi yake njema na hospitali ya Panzi itazidi kuhifadhi watu wanaokaa katika mazingira magumu.

Katibu Mkuu Ban ametoa wito kwa serikali ya DRC kuhakikisha usalama wa Dkt. Mukwege na familia yake, na kufanya kila iwezalo kutambua wale waliotelekeza mashambulizi hayo na kuwapeleka mbele ya mkono wa sheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031