Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Syria kujadili hali nchini humo

Kusikiliza /

KM Ban ki-moon na waziri wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa taifa la Syria, Bwana Walid Al-Moualem, wakati wa mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Bwana Ban amezungumzia kuhusu mauaji yanayoendelea, uharibifu kwa kiwango kikubwa, ukiukaji wa haki za binadam, mashambulizi ya angani na makombora, ambayo ambayo yanatekelezwa na serikali ya Syria. Amesema kwamba ni watu wa Syria ndio wanaouawa kila siku, na kutoa wito kwa serikali ya Syria kuwa na huruma kwa watu wake.

 

Ameongeza kuwa kupunguza ghasia kunaweza kuiweka serikali tayari kwa harakati za kisiasa. Ameelezea masikitiko yake kuwa baada ya miezi 19 ya ukandamizaji na mapigano, hali inazidi kuzorota.

Katibu Mkuu na waziri huyo pia wamejadili kuhusu hali ya kibinadam inayozidi kuzorota ndani mwa Syria, na ambayo inaenea hadi nchi jirani kwa viwango vya kutisha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031