Bado kuna kazi nyingi ya kufanya kuyafikia malengo ya milenia: Eliasson

Kusikiliza /

Jan Eliasson

Ikiwa imesalia miaka mitatu na miezi mitatu tu kabla ya tarehe ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, bado kuna kazi nyingi ambayo inahitajika kufanywa. Hayo ni kwaa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa 67 wa Baraza Kuu, ambao umehitimishwa wiki hii.

Bwana Eliasson amesema bado kuna mengi muhimu ambayo hayajatimizwa kufikia sasa, na hivyo juhudi zaidi zinahitajika ili malengo haya yatimie.

 

Ametaja suala la afya ya akina mama wajawazito kama mojawepo ya malengo ambayo mwendo wake ni wa pole sana, akisema kwamba hilo linahusunisha. Amesema kuwa ni jambo la aibu kwamba ni hatua chache sana zimepigwa katika kuhakikisha usafi kwa wote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031