Bado kuna changamoto kutokomeza Kifua Kikuu duniani: WHO

Kusikiliza /

ugonjwa wa kifua kikuu

Shirika la afya duniani, WHO limesema uhaba mkubwa wa fedha unatishia jitihada za kimataifa za kutibu na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Kifua Kikuu.

WHO imesema kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo zinahitajika dola Bilioni Nne nukta Nne zaidi kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na TB ikiwemo utafiti wa dawa mpya.

Shirika hilo limesema ijapokuwa idadi ya wagonjwa wapya inapungua, bado Kifua Kikuu ni tatizo kubwa la afya duniani ambapo mwaka jana pekee kulikuwepo na wagonjwa wapya Milioni Nane nukta Saba.

Takwimu hizo zimo katika ripoti ya mwaka ya WHO ambayo pia imeonyesha kwa India na China kwa pamoja zina asilimia 40 ya wagonjwa wote wa Kifua Kikuu duniani huku bara la Afrika likiwa na asilimia 24. Dkt. Phillipe Glaziou ni Afisa kutoka idara ya Kifua Kikuu ya WHO

(SAUTI YA DKT. GLAZIOU)

"Katika ripoti yetu tumeonyesha mafanikio yaliyopatikana Cambodia, nchi ambayo miaka kumi iliyopita ilikuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kifua Kikuu duniani na sasa imepunguza kwa asilimia 45 katika kipindi cha miaka tisa. Utafiti unaonyesha matumaini makubwa kwa dawa mpya ambayo ni ya kwanza kutolewa katika kipindi cha miaka 40, dawa ambayo inaweza kuingizwa sokoni mapema mwakani, pamoja na chanjo nyingine 11 za majaribio. Tunahitaji kuwekeza zaidi. Tatizo la fedha linatishia uwezo wa kuzuia, kutibu na hata kuchelewesha kubuni mbinu mpya. Tuko njiapanda kati ya kutokomeza Kifua Kikuu wakati huu au kuwa na mamilioni ya vifo kutokana na ugonjwa huu katika miaka kadhaa ijayo."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930