Askofu Mkuu Tutu asema ni ujinga kabisa kuwapuuza wanawake

Kusikiliza /

Askofu Mkuu Desmond Tutu

Askofu Mkuu Desmond Tutu amesema haileti maana yoyote kuwaengua wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wote duniani huku akisema kuwa ni hivi karibuni tu ambapo wanawake wameanza kutambuliwa kuwa na uwezo na wanashika nyadhifa mbali mbali kwenye ofisi ikiwemo zile za kidini.

Kauli hiyo ya Tutu ameitoa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ambako ameshiriki shughuli maalum ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani na kuupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuanzisha wazo la kuwa na siku hiyo.

“Kumekuwepo na unyanyasaji mkubwa dhidi ya kundi hili ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wote duniani. Tunahitaji kuchukua hatua dhidi ya hali hii. Ninasema ni ujinga kabisa. Hivi huelewi hesabu? Asilimia hamsini unaitupilia mbali. Haina maana kabisa."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031