Asilimia 20 ya vijana hawapati stadi za kuwawezesha kuajiriwa: UNESCO

Kusikiliza /

vijana wanotafuta ajira

Vijana Milioni 200 katika nchi zinazoendelea wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 hawakumaliza elimu ya msingi na hivyo wanahitaji njia mbadala ya kuwapatia stadi za msingi kuweza kuajiriwa au kuwa na maisha bora.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Kumi ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO inayofuatilia mpango wa elimu kwa wote ikijikita zaidi katika stadi za vijana.

Ripoti hiyo imeeleza umuhimu wa haraka wa kuwapatia stadi vijana wakati huu ambapo idadi yao duniani ni kubwa kuwahi kutokea, ambapo kijana mmoja kati ya wanane hana ajira, na robo ya wenye ajira wanafanya kazi ambazo bado zinawaweka katika maisha ya ufukara.

UNESCO imesema kadri hali ngumu ya uchumi inavyoendelea kubinya maisha ya jamii mbali mbali duniani, madhara ya vijana kutokuwa na kazi yanakuwa mabaya kuliko kuwahi kutokea.

Ripoti hiyo imesema licha ya maendeleo ya kuridhisha katika baadhi ya maeneo, nchi chache ziko kwenye mwelekeo wa kufikia lengo la sita la milenia la elimu kwa wote na zingine bado ziko nyuma.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031