Al-Za'tari alani shambulizi la bomu mjini Kadugli

Kusikiliza /

wakimbizi wa kadugli

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali Al-Za'tari, amelani mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa hii leo kwenye mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini Kadugli. Kulingana na ripoti mabomu yalianguka karibu na ofisi ya shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF , kwenye shule moja na pia kwenye kituo cha polisi.

Hakuna mfanyikazi wa Umoja wa Mataifa aliyeripotiwa kujeruhiwa na sasa hizi wafanyikazi hao wamehamishwa kwenda kwa kituo cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifae neo la Ayei kama moja ya njia ya kuchukua tahadhari. Hadi wakati wa shambulizi hilo kulikuwa kukiendelea mkutano wa amani wenye hadi wajumbe 600 wakiwemo watoto wa shule mjini Kadugli. Bwana Al-Za'tari anasema kuwa mashambulizi kama hayo kwa raia na makao ya Umoja wa Mataifa ni kinyume na sheria za kibinadamu za kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031