Afghanistan kwenye mkondo wa matumaini siku za usoni

Kusikiliza /

Jan Kubis

Hata baada ya kuwepo changamoto nyingi zikiwemo za uongozi na usalama nchini Afghanistan taifa hilo bado liko kwenye mkondo wa matumaini wa siku za baadaye, amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Akiongea kwenye mkutano wa waaandishi wa habari mjini Kabul Jan Kubis amezungumzia ziara ya juzi mjini New York ambapo alihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali iliyopo nchini Afghanistan. Bwana Kubis amesema kuwa yeye pamoja na wanachama wa baraza hilo walikubaliana kuwa Afghanistan kwa sasa inakabiliwa na changamoto kadha zinazohusiana na uongozi bora , ufisadi, ulanguzi wa madawa, ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na hali ya usalama isiyotabirika

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031