Adabu ya kifo inapotolewa iwe tu ni kwa makosa mabaya zaidi: Heyns

Kusikiliza /

Christof Heyns

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yasiyo ya kisheria na kunyonga watu kiholela, Christof Heyns, leo amezikumbusha serikali kuhusu masharti yanayohusiana na utoaji wa adabu ya kifo, hususan katika nchi ambazo bado zinashikilia adabu ya kifo katika katiba zao.

Bwana Heyns amesema, kwa yale mataifa ambayo bado yanaishikilia adabu ya kifo, sheria ya kimataifa inaweka masharti ambayo ni lazima yatimizwe ili adabu kama hiyo isionekane kuwa kinyume na sheria. Amesisitiza kuwa ni muhimu mataifa ambayo yamepiga marufuku adabu ya kifo yasiyasaidie yale ambayo bado yanashikilia adabu hiyo, iwe ya kisheria au kinyume na sheria.

Mtaalam huyo wa haki za binadamu amesema haki ya kuwa na uhai ni haki ya msingi ambayo haki zingine zote zinategemea, na inafaa kupewa ulinzi wa hali ya juu zaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031