Tamaduni na itikadi za jamii ya Maasai nchini Kenya na Tanzania

Kusikiliza /

maasai

Jamii ya Maasai inayoishi nchini Kenya na Tanzania ni moja ya jamii zilizofanikiwa kulinda na kudumisha utamaduni wao tangu jadi hadi leo. Jamii hii ambayo nchini Kenya inapatikana kwenye bonde la ufa, shughuli yao kubwa ni ufugaji hasa wa ng'ombe huku chakula chao kikiwa ni maziwa, damu na nyama. Jamii hii pia inaamini kuwa ng'ombe wote duniani ni wao. Hata hivyo kuna baadhi ya watu kutoka jamii hii ambao wameupiga teke utamaduni huo na kuingia mijini kama wakenya wengine na kuishi maisha ya raha na starehe.

Ili kuelewa zaidi utamaduni wa jamii ya Maasai mwandishi wetu wa Nairobi Jason nyakundi ametuandalia makala kuhusu utamaduni na itikadi za jamii ambayo ni maarufu kama kivutio cha watalii nchini Kenya

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2015
T N T K J M P
« jul    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31