Miji inapaswa kuimarisha hali ya usafi:Mkuu wa UN-Habitat

Kusikiliza /

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi UN-Habitat amesema kuna umuhimu wa kuzingatiwa usafi na utaalamu wakati wa uendelezaji wa miji.

Akizungumza wakati wa kongamano la kimataifa linalofanyika Naples nchini Italy Dr Joan Clos amesema kuwa matumaini ya watu wengi sasa yanapelekwa katika maeneo ya mijini ambako kiasi cha watu 200,000 duniani kote hukimbilia mjini kila siku.

Amesema kwa maana hiyo kuna umuhimu wa kuangazia hali ya miji na maendeleo yake kwani bila kufanya hivyo kunaweza kutatiza hali ya ustawi wa kijamii.

Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili ukiwaleta pamoja jumla ya wajumbe 3,000 kutoka ofisi za kiserikali, mashirika binafsi na wawakilishi wa mashirika ya kiraia

Jumla ya nchi 114 zinashirika mkutano huo ambao mwaka huu umeweka zingatio lisemalo " mustabala wa usoni wa miji.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031