UNAMID yatiwa hofu na Machafuko Darfur Kaskazini

Kusikiliza /

kikosi cha UNAMID

Vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika vya kulinda amani Darfur UNAMID vimesema vinatiwa hofu na machafuko na mashambulizi dhidi ya raia katika mji wa Kutum na viunga vyake katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan

Kwa mujibu wa mkuu wa vikosi hivyo Ibrahim Gambari mauaji na uharibifu sio jibu na ametoa wito kwa pande zote husika kuweka silaha chini na kutafuta suluhu ya amani kwa njia ya mazungumzo.

Katika taarifa iliyotolewa na UNAMID Gambari amesema anatumai kwamba serikali itajitahidi kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo ikitimiza wajibu wake wakuwalinda raia na kuruhusu watunwaliokimbia kurejea makwao. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031