UM wawatahadharisha waasi wa M23 wa DRC
Kusikiliza /Msemaji wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO Manodj Monoubay ametoa tangazo la kuwatahadharisha waasi wa M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yanayotishia salama Mashariki mwa nchi hiyo kusitisha mara moja zoezi la kuwaingiza watoto jeshini.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kishasa Jumatano Monoubary amesema ikiwa waasi watakaidi wito huo basi baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litachukua hatua ambayo itatekelezwa na MONUSCO kama alivyotangaza Katibu Mkuu Ban Ki-moon.
(SAUTI YA MANODJ MONOUBARY)
Makundi yenye silaha yamekwa yakiendesha asi Mashariki mwa Congo, ikiwa ni pamoja na vitendo vya maaji, bakaji na kuwashirikisha watoto vitani.
