Muafaka wa suala la mafuta baina ya Sudan na Sudan Kusini wakaribishwa na Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Muafaka baina ya Sudan na Sudan Kusini wa kutatua mzozo kuhusu mafuta umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Mwishoni mwa wiki nchi hizo mbili zimetangaza kwamba zimekamilisha muafaka kwa Sudan Kusini kusafirisha mafuta yake kwa kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan na jinsi ya kugawana mapato ya mafuta hayo.

Katibu Mkuu amesema maafikiano hayo ni hatua muhimu sana kwa ujenzi wa uhusiano wa jirani mwema baina ya mataifa hayo mawili. Martin Nesirky ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA MARTIN NESERKY)

"Katibu Mkuu anatiwa moyo kwamba serikali hizo mbili zimelegeza msimamo wao kwa sula hilo nyeti. Anasikitika hata hivyo hazijatimiza muda wa mwisho wa Agosti pili uliowekwa na baraza la usalama wa kidhinisha mpango wa amani wa baraza la amani na salama la Afrika. Amewataka viongozi wa Sudan na Sudan Kuusini kuzingatia na kutekeleza ari ya kisiasa ya kutatua masuala mengine yaliyosalia."

Ban pia ameipongeza serikali ya Sudan na waasi kwa kutia saini makbaliano ya msaada wa kibinadamu kwa majimbo yaliyoathitrika na vita la Kordifan Kusini na Ble Nile. Ban amepongeza juhdi za Muungano wa Afrika zilizoongozwa na Rais Thabo Mbeki na mwakilishi wake maalumu wa Sudan na Sudan Kusini Haile Menkerios.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031