Mkutano wa kamati ya UM wajadili utokomezaji wa silaha za kinyuklia
Kusikiliza /Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusu kukomesha matumizi ya silaha za nyuklia, inaendelea na mazungumzo kuhusu njia mwafaka za kuhakikishia mataifa yasiyo na silaha za nyuklia kuhusu matumizi au tishio la kushambuliwa na silaha kama hizo.
Mwakilishi wa Japan kwenye kamati hiyo ameelezea hamu ya taifa la Japan kuona ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia, na kutoa wito kwa kamati hiyo iweze kujiondoa kwenye mkwamo iliomo sasa kuhusu muafaka kuhusu suala hili tete.
Wajumbe wengi kwenye mkutano wa kamati hiyo wamekubaliana kuwa utokomezaji wa sialaha za nyuklia kabisa ndilo hakikisho la kipekee la kutozitumia au kuondoa tishio la kuzitumia, na kwamba pasi kulifikia hili, mataifa ambayo hayana silaha hizi yana haki ya kujihami mbeleni dhidi ya matumizi au tishio la matumizi ya silaha hizi.
