Makundi yaliyojihami kaskazini mwa Mali yanaendelea kuwaajiri watoto:UNICEF
Kusikiliza /Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema limepokea ripoti kuwa makundi yaliyojihami kaskazini mwa Mali yanaendelea kuwatumia watoto kwenye mapigano. Kuajiriwa na kutumiwa kwa watoto walio chini ya miaka 18 na makundi yaliyojihami ni kinyume na sheria ya kimataifa na nikitu kinachotajwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu iwapo watoto walio chini ya miaka 15 watatumiwa jeshini. Hata kama idadi kamili ya watoto hao haijulikana ripoti zinasema kuwa ni mamia ya watoto wanaotumiwa na idadi hiyo inazidi kuongezeka. Mwezi Julai UNICEF ilisema kuwa watoto wa kiume 175 walio na umri wa kati ya maiaka 12-18 walitumiwa na makundi yaliyojihami kaskazini mwa nchi. UNICEF inatoa wito kwa pande zote kwenye mzozo na viongozi na jamii kuhakikisha kuwa watoto wamelindwa kutokana na athari za mizozo na pia kuhakikisha kuwa hawashirikishwi kwenye mambo kama hayo. Marxie Mercado kutoka UNICEF anaeleza.
(SAUTI YA MARXIE MERCADO)
