Mahiga akaribisha tamko la kumaliza serikali ya mpito Somalia

Kusikiliza /

Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga amekaribisha tamko lililotolewa leo na watiaji saini mpango wa kumaliza serikali ya mpito, wakati wa kukamilisha mkutano uliokuwa ukijadili masuala yaliyosalia na kuhakikisha kwamba majukumu yote yanakamilishwa ili kumaliza kipindi cha mpito katika wiki mbili zijazo.

Ajenda sita zimejadiliwa katika mkutano huo zikiwemo kuunda na kutangaza orodha ya wazee wa kiasili, uchaguzi wa wabunge 275, kuheshimu na kulinda kamati ya kiufundi ya uchaguzi, taratibu za uchaguzi wa spika , naibu spika na Rais zitakazofatwa na bunge na mwisho ni hali ya kisiasa ya Galmadug. Mahiga amesema majadiliano yalikuwa magumu lakini washiriki waliongea kwa uwazi na ujasiri na mwisho muafaka ukafikiwa kwa masuala yote na tamko limetolewa na pande zote zilizohudhuria.

Mahiga ingawa amekaribisha muafaka huo alakini ameelezea hofu kuhusu muda uliotumika kutatua masuala muhimu. Amesema muda unakwenda na mchakato hauwezi kuchelewa zaidi. Amesema kwa  sasa mjadala umekwisha anazitaka pande zote kuelekeza nguvu zake katika kukamilisha majkumu yaliyobaki kwa wakati kama walivyoahidi hadharani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930