Kofi Annan Kujiuzulu kama mwakilishi wa UM na Umoja wa Nchi za Kiarabu Syria

Kusikiliza /

Kofi Annan

Taarifa iliyotolewa hivi pnde na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Alhamisi inasema kwa masikitiko anatangaza taarifa za kujiuzulu kwa Kofi Annan kama mwakilishi maalum wa Umoja na moja wa nchi za Kiarabu nchini Syria.

Bwana Annan amemuarifu Katibu Mkuu wa Muungano wan chi za Kiarabu Nabil El Araby kuhusu nia yake ya kutoongeza muda wa majukumu yake hapo Agosti 31 mwaka huu kipindi chake cha awaki kikimalizika.

Ban amesema anamshukuru saana Bwana Annan kwa nia yake na juhdi za kijasiri alizozifanya kama mwakilishi maalmu kwa ajili ya Syria.

Ban amesema hivi sasa anafanya mawasiliano na Katibu Mkuu wa Umoja wa  nchi za Kiarabu ili kujadiliana kuhusu uteuzi wa mtu atakayemrithi Kofi Annan akikamilisha muda wake hapo Agosti 31.

Ban ameongeza kwa Umoja wa mataifa bado umejidhatiti ktafuta sulhu ya mgogoro wa Syria kwa njia ya kidiplomasia ili kumaliza machafuko ambayo yameshika kasi hivi karibuni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930