Nyumbani » 13/08/2012 Entries posted on “Agosti 13th, 2012”

Askari wa UNAMID auwawa Kusini mwa Darfur

Walinda Amani wa UM Darfur

Askari wa kulinda amani anayefanya kazi chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID katika jimbo lenye mzozo la Darfur nchini Sudan ameuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Kwa mujibu wa duru za habari, kundi la watu wenye silaha walivamia kambi moja ijulikanayo Nyala iliyoko Kusin mwa Darfur na kuanzisha mashambulizi yaliyosababisha [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahiga ashutumu vikali mauaji ya afisa wa serikali na mwandishi wa habari nchini Somalia

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mjumbe maaalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ameshutumu vikali mauaji ya Yusuf Ali Osman ambaye ni afisa wa serikali nchini Somalia na yale ya mwandishi wa habari. Ali au kwa jina lingine Buniste yaliyotokea mjini Mogadishu. Yusuf mwandishi wa habari wa zamani alikuwa mfanyikazi kwenye wizara ya habari [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban Ahusunishwa na Kuangamia kwa watu Kutokana na Tetemeko la Ardhi nchini Iran

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban

  Katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea kaskazini magharibi mwa Iran mwishoni mwa wiki. Kupitia kwa msemaji wake Ban ametoa rambi rambi zake kwa serikali ya Iran, watu wake na hasa kwa familia za wale [...]

13/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Valerie Amos kuzuru Syria na Lebanon

Kusikiliza / Bi Valerie Amos

  Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, anatarajiwa kusafiri kwenda Syria na Lebanon kuanzia tarehe 14 hadi 16 Agosti. Ziara hiyo ya siku tatu inalenga kuuchagiza ulimwengu kuangazia hali ya kibinadamu inayozidi kuzorota nchini Syria, na athari za mgogoro ama kwa walosalia nchini Syria, au walokimbilia nchi zingine, ikiwemo [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP azuru Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / Bi Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, ameanza ziara ya siku tatu katika mataifa ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini. Cousin ameanza ziara yake kwa kukutana na mafisa wakuu wa serikali mjini Khartoum, wawakilishi wa mashirika ya kutoa misaada na wafanyakazi wa WFP. Sudan ni mojawapo wa maeneo ambako [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Azindua Mkakati mpya wa Kulinda Bahari

Kusikiliza / Bahari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amezindua mkakati mpya wa kulinda bahari na watu ambao riziki zao zinategemea bahari, na kutoa mwito kwa mataifa kufanya kazi pamoja ili kufikia udhibiti endelevu wa mali ghafi hiyo azizi, na kukabiliana na hatari zinazoikabili. Kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 30 tangu kufunguliwa mkataba wa Umoja wa [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasaidia juhudi za Ufilipino kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

Kusikiliza / Mafuriko Ufilipino

Kufuatia mvua nzito iliosababisha mafuriko katika majimbo ya Luzon ya Kati na Manila Mjini, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limeandaa misaada ya chakula ili kuisaidia serikali ya Ufilipino katika juhudi zake za kuwasaidia watu waloathiriwa na mafuriko, likisaidiana na idara ya Maslahi ya Kijamii na Maendeleo katika majimbo ya Luzon Kati, [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Palestina nchini Syria wasafirishiwa msaada toka nyumbani

Kusikiliza / Mkimbizi wa Kipalestina na mtoto Syria

Msafara wa msaada wa chakula na dawa ambao umeandaliwa na mamlaka ya Palestina kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, uliwasili mjini Damascus tarehe 8 Agosti. Msafara huo wa malori 17 ulichukua tani 360 za unga, mchele, sukari, ngano na madawa yenye thamani ya dola 650,000. Msaada huo umetolewa na mashirika ya Kipalestina, wafanyabiashara na watu binafsi wakati [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Yazidi Kuongezeka Syria:Gaye

Kusikiliza / Jenerali Babacar Gaye

  Ni dhahiri kwamba ghasia zinaongezeka katika maeneo mengi ya Syria amesema mkuu wa mpango wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIS Jenerali Babacar Gaye alipozungumza na waandishi wa habari Jumatatu mjini Damascus. Gaye amesema matumizi ya silaha nzitonzito yanayofanywa na serikali na mashambulizi ya kulenga yanayofanywa na upinzani katika maeneo mbalimbali mijini [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujuma wanajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake ili wafikie malengo ya kuchagiza maendeleo na kuipeleka dunia katika mstakhbali bora. Ban ameyasema hayo mjini Seuol Korea Jumatatu kwenye kongamano la kwanza la kimataifa la shirikiano wa wasichana. Ban amesema [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930