Nyumbani » 09/08/2012 Entries posted on “Agosti 9th, 2012”

Mashirika ya kibinadamu yaomba dola milioni 32.5 kufadhili mahitaji yanayongezeka Myanmar

Kusikiliza / John Ging

Akikamilisha ziara yake ya siku nne Myanmar, Mkurugenzi wa shughuli za Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadam, John Ging ameelezea hofu yake kuhusu hatma ya zaidi ya nusu milioni ya wakimbizi wa ndani, na kutoa wito ziheshimiwe kanuni na sheria za kimataifa za kibinadamu ili kuyawezesha mashirika ya kutoa misaada kuyafikia maeneo yaloathiriwa na mzozo [...]

09/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM watoa dola milioni 158 kwa mahitaji ya kibinadamu ambayo hayajafadhiliwa vyema mwaka 2012

Kusikiliza / Valerie Amos

Mkuu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ametenga dola milioni 55 kutoka kwenye mfuko wa Mfuko wa Ufadhili wa Maswala ya Dharura (CERF), ili kuimarisha operesheni za kibinadamu katika nchi nane zenye mahitaji ya kibinadam yaliyopuuzwa. Fedha zilizotengewa mataifa ya Afghanistan, Cameroon, Colombia, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC), Ethiopia, Madagascar, [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Athari za radio na mabadiliko ya hali ya hewa kwa jamii za kiasili nchini Peru

mtu wa asili, Peru

Jamii za kiasili kwenye milima ya kusini mwa Andean nchini Peru wanaripotiwa kuathiriwa pakubwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Jamii hizi zinakabiliwa na hali mbaya ya umaskini suala linalochangiwa na mavuno duni. Jamii hizi zinazoishi mbali milimani hazina uwezo wa kupata hamasisho kutoka mijini kuhusu njia za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali [...]

09/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wakatibisha Muafaka wa pande tatu nchini Sudan

Kusikiliza / Mark Cutts

  Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Mark Cutts amekaribisha utiaji saini wa maelewano baina ya serikali ya Sudan, kundi la SPLM-North pamoja na Muungano wa Afrika, Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kuhusu msaada wa kibinadamu katika majimbo yaliyoathirika na vita ya Kordofan Kusini na Blue [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wimbi la wakimbizi wa ndani Syria ni kutokana na kutoheshimu sheria za Kimataifa:UM

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Kupuuza haki za binadamu za kimataifa na sheria za kimataifa kumechangia kuwepo kiasi kikubwa sana cha wakimbizi wa ndani nchini Syria, wakati mgogoro unapozidi kutokota, amesema mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wakimbizi wa ndani, Chaloka Beyani. Bwana Beyani ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya takriban watu milioni 1.5, ambao wamelazimika kuhama [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wawatahadharisha waasi wa M23 wa DRC

Kusikiliza / waasi wa M23 nchini DRC

Msemaji wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO Manodj Monoubay ametoa tangazo la kuwatahadharisha waasi wa M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yanayotishia salama Mashariki mwa nchi hiyo kusitisha mara moja zoezi la kuwaingiza watoto jeshini. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kishasa Jumatano Monoubary amesema ikiwa waasi [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasisitiza Umuhimu wa Diplomasia ya Kuzuia Migogoro

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea umuhimu wa diplomasia ya kutambua mapema na kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani kama njia ya kuzuia migogoro zaidi. Wanachama wa Baraza hilo wameelezea umuhimu wa kisiasa, kibinadamu na kimaadili, pamoja na faida za kiuchumi za kuzuia kutokea, kuongezeka au kurejelea migogoro. Katika taarifa ilotolewa kwa waandishi [...]

09/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bei ya Bidhaa za Chakula Yapanda kwa asilimia 6:FAO

Kusikiliza / mazao

Bei ya bidhaa za chakula ilipanda kwa kiasi cha asilimia 6 mwezi Julai, baada ya miezi mitatu ya kushuka bei hiyo, limesema Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO. Kipimo wastani cha viwango vya bei za bidhaa za chakula cha FAO, hupima mabadiliko ya kila mwezi katika bei za kapu la bidhaa za chakula. Kwa [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada Imara wa Kibinadamu wahitajika DRC:Amos

Kusikiliza / wakimbizi nchini DRC

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya dharura na misaada ya kibinadamu Valarie Amos amehitimisha ziara yake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi baada ya kuzuru eneo la Kanyaruchinya nje kidogo ya mji wa Goma siku ya Jumatano. Katika eneo hilo watu 30,000 wamepatiwa makao na amesema inasikitisha kuona watu hususani [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyombo vya Habari vya Kijamii vinatoa fursa kwa jamii ya Watu wa Asili:ILO

Kusikiliza / vyombo vya habari vya kijamii

Katika muktadha huo wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wa kiasili leo, Shirika la Kimataifa la kazi duniani, ILO, limesema vyombo vya habari vya kijamii vinachangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza haki za watu wa kiasili. Shirika la ILO limesema hili linatokana na kwamba, takriban nusu ya idadi ya watu wa kiasili kote ulimwenguni wanaishi [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wa Asili ni Muhimu Kushirikishwa katika vyombo vya Habari:UM

Kusikiliza / maasai

Imeelezwa kwamba huu ni wakati pekee ambao watu wa kiasili hupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari, ni pale wanapouawa. Hii ni dhana ya kusikitisha na ni mojawepo tu ya mifano ya malalamishi yaliyofikishwa kwa Mkuu wa Sekritariati ya Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa kiasili, Chandra Roy-Henriksen. Siku ya kimataifa ya [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awapongeza Watu wa Asili kwa kutumia Vyombo vya Habari vya Asili na vya Kisasa

Kusikiliza / watu wa asili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa asili kwa kujitokeza kutumia vyombo vya habari vya asili na vya kisasa katika kuchagiza masuala mbalimbali yanayowahusu. Katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya watu wa asili Alhamisi Ban amesema kuanzia magazeti, tovuti hadi mitandao ya kijamii watu wa asili wanatoa changamoto [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031