Nyumbani » 03/08/2012
Entries posted on “Agosti 3rd, 2012”
Kusikiliza /

Jumuiya ya Kimataifa imetolewa wito na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban kuchukua hatua za kumaliza mgogoro unaoendelea katika Syria. Bwana Ban amesema haya katika mkutano wa Baraza Kuu wa kupitisha azimio la kulaani vurugu inayoendelea nchini. Alisema mgogoro wa Syria ni mtihani wa kuwepo kwa Umoja wa Mataifa na kazi yake yote. “Shinikizo [...]
03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Serikali ya Ujerumani umetoa msaada ya Euro milioni mbili zitakazosaidia kulisha wakimbizi wa kipalestina 667,500 kwenye ukanda wa Gaza. Fedha hizo ni msaada wa ombi la mwaka 2012 la shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbzii wa kipalestina UNRWA la mwaka 2012 la kusaidia wakimbizi kwenye ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi. Mkuu wa [...]
03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inahofia mswaada wa sharia ambao hivi sasa umefikishwa mbele ya bunge la Liberia ambo unapendekeza mabadilikon ya sheria ambayo yatafanya kuwa ni uhalifu tabia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Sheria ambayo imeshapitishwa na bunge l seneti infany kuwa ni kosa la jinai la kiwango cha [...]
03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa kwa sasa unatekeleza mpango wa majaribio katika nchi nane barani Afrika kwa shabaya ya kuharakisha maendeleo. Mpango huo pamoja na mambo mengine pia unatupia macho maeneo ya ustawishaji wa demokrasia, ukuzaji uchumi na kusukuma mbele shughuli za kimaendeleo. Katika makala yetu leo mwenzetu George Njogopa anamulika juhudi zinazofanywa na Shirika hili la [...]
03/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takwimu za muungano wa kimataifa wa teknolojia ya mawasiliano ITU na teknolojia ya mawasiliano ICT sasa zinapatikana kupitia mtandao wa umma wa utafutaji takwimu yaani Google Public data Explorer kupitia kwenye wavuti. Kwa ushirikiano wa mtandao wa Google na ITU sasa watumiaji wa mtandao wanaweza kutafuta na kuona takwimu muhimu zilizopo za teknolojia [...]
03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wanafanya juhudi kukabilina na visa vya utapiamlo, magonjwa na vifo kwenye kambi mbili zinazowahifadhi wakimbizi kutoka Sudan. Wahudumu wa afya kwenye kambi ya Yida jimbo la Unity walishuhudia kuongeza kwa vifo kwa watoto kwemye kambi mwezi Juni na mapema mwezi Julai. Mwa muda wa [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefungua ofisi mjini Dollow na kurejesha uwepo wake kwenye mji huo wa karibu na mpaka wa Somalia na Ethiopia ili kukabiliana na ongezeko la wakimbizi wa Somalia wanaokimbia ukame. Takwimu za karibuni zinaonyesha kwamba watu 11,000 zaidi wametawanywa ndani ya Somalia tangu mwanzo wa Aprili kutokana [...]
03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku ghasia zikiendelea kuchacha nchini Syria watu zaidi wanaendelea kuhama makwao kutafuta usalama wao. Takriban watu milioni 1.5 waliohama makwao wamesalia ndani mwa Syria wakitafuta hifadhi kwa familia zingine au kwa makao ya muda. Watu wengine wamekwama wakiwa na hofu na hofu ya kujipata kati kati mwa mapigano au kulengwa wakati wanapohama. Mji wa Aleppo [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku machafuko yakizidi kuchacha nchini Syria mnamo wakati mjumbe maalumu wa upatanishi kwenye mzozo huo Kofi Annan akiashiria kuachia wadhifa wa usuluhishi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu,Baraza la Usalama linatafakari hatma ya raia milioni 3 walioko kwenye hali mbaya wakihitaji msaada wa dharura. Wakati huu Ufaransa imechukua kiti cha urais wa kupokezena katika baraza hilo [...]
03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa kwa sasa kumeripitiwa visa 50 vya ugonjwa wa Ebola na vifo 16 vilivyosababishwa na ugonjwa huo nchini Uganda. Tangu siku ya Jumanne visa kadha vya ugonjwa huo vimeripotiwa hospitalini lakini ni watu wawili walioripotiwa kuaga dunia. Wizara ya afya nchini Uganda inashirikiana na washikadau pamoja na washirika wake [...]
03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama limerejelea mwito wake kutaka makundi ya askari waasi wanaoendesha vitendo viovu huko kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuweka silaha nchini kwa mustakabala wa taifa hilo na wananchi wake. Baraza hilo limesema kuwa kundi la askari waasi wa M23 wanapaswa kujieopusha na matumizi ya silaha kuzorotesha usalama katika eneo walikopiga ng'ome [...]
03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM leo limekabidhi vifaa tiba kwa vituo vya afya vinavyotoa huduma za utabibu katika maeneo ya vijijini vilivyoko kusini mashariki mwa mji wa Harare. Vifaa hivyo lakini vinatazamiwa kuwa habari njema kwa mamia ya waliokuwa wafanyakazi wa mashambani ambao wengi wao hawana makazi maalumu Kiasi cha wafanyakazi [...]
03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema kuwa vikosi vya usalama kwenye jimbo la Darfur huenda viliwaua watu wannane ambapo watano kati yao walikuwa ni wanafunzi walio na umri wa chini ya miaka mitano na kuwajeruhi watu wengine 50 siku ya Jumanne wakati walipowafyatuilia risasi waandamanaji kwenye mji wa mji mkuu [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonia Guterres ametoa wito wa jamii ya kimataifa kufanya kila iwezalo kukabiliana na hali iliyopo nchini Mali na kuzitaka nchi kusadia oparesheni ambazo sasa hivi zinakabiliwa na uhaba wa fedha kwenye eneo hilo ambalo halina uwezo wa kujilisha. Zaidi ya watu 250,000 wameikimbia Mali kwa [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha shughuli ya kuwapa mafunzo wafugaji 180 kutoka maeneo sita kwenye wilaya ya Daadab kaskazini mwa Kenya kuhusu jinsi watakavyowatunza mifugo wao wakati kunapotokea ukame. Ufugaji wa ng'ombe ndio tegemeo kwa wenyeji wa kaskazini na kaskazini masharki mwa Kenya walioko maelfu ya wasomali wanaokimbia vita na ukame nchini mwao. [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK wanatoa msaada wa chakula, vifaa visivyo chakula, madawa, maji na vifaa vya usafi kufuatia athari za mafuriko nchini humo. Mashirika hayo yanatarajiwa kuendelea kusaidia kutokana na mahitaji ya watu wa DPRK. Wakati kipaumbele kimetolewa kwa nchi ambazo zimemetembewa, [...]
03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »