Nyumbani » 02/08/2012 Entries posted on “Agosti 2nd, 2012”

Nyota wa Muziki Beyonce Aungana na Mashirika ya Kimataifa kwenye Siku ya Kibinadamu Duniani

Beyonce

Nyota wa muziki Beyonce na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa wanazindua kampeni ya kimataifa hii leo inayowashauri na kuwapa watu motisha ya kuwafanyia vyema wengine. Siku ya kimataifa ya kibinadamu inaadhimishwa ili kusherehekea ubinadamu na moyo wa watu kusaidia watu. Video ya wimbo ya nyota huyo kwa jina "I Was Here" inatarajiwa kuchezwa [...]

02/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Familia zaidi ya 129,000 za Kipalestina kupokea msaada wa chakula kutoka Uturuki

Kusikiliza / nemba ya UNRWA

Zaidi ya familia 129,000 za Kipalestina zitafaidika na msaada wa chakula kutoka serikali ya Uturuki ambao unathamani ya dola milioni 6.6 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada klwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Tani 12,500 za ngano zitawasili katika wiki nane zijazo hku awamu ya kwanza ikiwasili leo na zitaweza kuwalisha watu wapatao 687,000 [...]

02/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Misaada zaidi inahitajika kuwafadhili wakimbizi wa Mali walioko mafichoni:Guterres

Kusikiliza / Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa shirika la kuwahumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres amesema kuwa wakati huu kuna hali ya mkwamo inayowandama mamia ya wakimbizi wa Mali waliokwama vichakana na akaenda mbali zaidi kwa kuitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza mafunga ya msaada kwa ajili ya kuwanusuru raia hao. Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuogeza [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amedhibitisha mwakilishi wake Yemen

Kusikiliza / Jamal Benomar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amedhibitisha bwana Jamal Benomar ambaye amepewa jukumu la kuwa mwakilishi wake huko Yemen akihusika zaidi na jukumu la kujenga mashirikiano mema hasa wakati huu taifa hilo likiwa kwenye kipindi cha mpito. Bwana Benomar amekuwa kifanya kazi kama mwakilishi wake nchini humo kuanzia mwezi April mwaka jana lakini [...]

02/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bima inaweza kusaidia kuwalinda maskini dhidi ya Ongezeko la joto duniani:ILO

Kusikiliza / ILO

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO hali ya hewa haiwezi kuwekewa bima lakini baadhi ya athari zake zinaweza kukatiwa bima hata kwa masikini ambao huathirika zaidi na athari za ongezeko la joto duniani. Craig Churchill ambaye anaongoza kitengo cha ILO kinachohusika na masuala ya bima anasema licha ya changamoto, kwa msaada wa ruzuku, [...]

02/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mataifa lazima yakabili Chuki, Ghasia na Ubaguzi dhidi ya Roma:UM

Kusikiliza / roma-se-europe

Mataifa yote na hususani yenye jamii za Waroma lazima leo yaadhimishe kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya Waroma yaani Roma Holocaust, huku yakijikita katika kukabiliana na chuki, ghasia na ubaguzi dhidi ya Roma na kutafuta suluhu ya kutengwa kwa jamii hiyo. Kauli hii imetolewa na wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Moto Waunguza Soko kwenye Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Kusikiliza / moto katika kambi ya Dadaab, Kenya

Moto mkubwa uliochoma soko katika Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya mwishoni mwa wiki umeonyesha haja ya kuwa na maandalizi bora ya moto na usalama Katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani. Moto ulizuka siku ya Jumapili jioni katika soko la kambi ya Dagahaley ambayo ni moja ya makambi tano katika Kambi kubwa ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kofi Annan Kujiuzulu kama mwakilishi wa UM na Umoja wa Nchi za Kiarabu Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Taarifa iliyotolewa hivi pnde na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Alhamisi inasema kwa masikitiko anatangaza taarifa za kujiuzulu kwa Kofi Annan kama mwakilishi maalum wa Umoja na moja wa nchi za Kiarabu nchini Syria. Bwana Annan amemuarifu Katibu Mkuu wa Muungano wan chi za Kiarabu Nabil El Araby kuhusu nia yake ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uongozi wa Somalia lazima kujitahidi Kuwalinda Waandishi Habari:Mahiga

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ametoa wito kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwalinda waandishi habari na kazi zao. Mahiga amesema afosi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kisiasa ya Somalia UNPOS iko tayari kuisaidia serikali kukomesha ukatili na unyanyasaji dhidi ya waandishi na kumaliza mzunguko wa wahalifu [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka Amani idumu wakati wa Kuhamishwa kwa Watoro wa Iran kutoka kambi nchini Iraq

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amezitaka pande mbili husika kushirikiana na kukamilisha kwa amani kuhamishwa kwa watoro wa Iran waliosalia kwenye kambi moja nchini Iraq. Kuambatana na makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi Disemba kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq ni kwamba theluthi mbili ya watu au 2000 wamehamishwa kwenda [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU kuboresha uwezo wa Broadband barani Afrika

Kusikiliza / nembo ya ITU

Mungano wa teknolojia ya mawasiliano ITU na kampni ya Nexpedience moja ya wasambazaji wakubwa wa miundombinu ya broadband wanashirikiana ili kupanua wigo wa fursa ya upatikanaji wa broadband barani Afrika. Chini ya muafaka wa pande hizo mbili Nexpedience itatoa mitambo ya thamani ya dola milioni 1 itakayopelekwa katika mataifa sita barani Afrika. Taifa la kwanza [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WaSyria milioni 3 wanahitaji msaada wa Chakula, Mazao na Mifugo:FAO na WFP

Kusikiliza / msaada wa chakula kwa watu wa Syria

Takribani watu milioni tatu wanahitaji msaada wa chakula, mazao na mifugo nchini Syria kwa mujibu wa tathimini ya karibuni iliyopfanywa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria. Watu milioni 1.5 kati ya hao wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita ijayo na hususani kwenye maeneo ambayo yanashuhudia vita [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuendelea kutoa Msaada wa Chakula kwa Wakimbizi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / msaada kutoka WFP, Sudan

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema lina mpango wa kuendelea kutoa msaada unaohitajika haraka wa chakula kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi kwenye jimbo la Upper Nile Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WFP Sudan Kusini Chris Nikoi wakimbizi wanaowasili kamimbini huwa wamedhoofu na wenye njaa baada ya kusafiri wiki kadhaa msituni [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031