Nyumbani » 31/08/2012 Entries posted on “Agosti, 2012”

CERF watoa ufadhili wa dola milioni 950 kufadhili oparesheni nchini Syria

Kusikiliza / wakimbizi wa syria

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola milioni 950 kufadhili oparesheni za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Syria. Fedha hizo zinatarajiwa kuwasaidia wahamiaji 650 waliokwama wasio na njia nyingine ya kurudi nyumbani kuukimbia mzozo. Kati ya wahamiaji hao ni wanawake wafanyikazi wa nyumbani waliopelekwa Syria na mashirika ya [...]

31/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaonyongwa yazidi kuongezeka:UM

Kusikiliza / nemba ya UN

Umoja wa Mataifa umeelezea wasi wasi wake kutokana na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaonyongwa kutoka na uhalifu tofauti nchini Gambia, Sudan Kusini na Iraq. Hivi majuzi watu 6 walinyongwa nchini Gambia hata baada ya kutishwa kwa sheria hiyo tangu mwaka 1985. Nchini Iraq watu 26 wamenyongwa mwezi huu. UM unasema kuwa kesi zinazosababishwa [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya Maisha ya wakimbizi wa ndani wa Goma nchini DRC

Kusikiliza / kambi nchini DRC

Hali ya maisha inaarifiwa kuwa duni sana katika maeneo kadhaa ya mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mapigano yanayoripotiwa mara kwa mara kati ya Vikosi vya serikali na waasi wa M23. Ingawa mapigano yamesimama au kupunguka kiasi, wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani waliopiga kambi kandokando na Mji wa Goma imekuwa ni kero [...]

31/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yakamilisha kuwasafirisha watu 2700 wanaorejea Sudan Kusini

Kusikiliza / raia wa Sudan

Mashua nane za mwisho zinazowasafirisha zaidi ya watu 2700 na mizigo yao zinatarajiwa kutia nanga kwenye bandari ya Juba baada ya majuma matatu ya safari kutoka eneo la Renk kwenye jimbo la Upper Nile. Mashua hizo ziliondoka eneo la Renk ambapo bado raia 16,000 wa Sudan Kusini wamekwama mnamo tarehe kumi mwezi huu zikipitia kwenye [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM una wasi wasi wa matumizi ya nguvu kupita kiasi nchini Guinea

Kusikiliza / Rupert Colville

Ofisi ya haki binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi mjini Conakry nchini Guinea. Mapema juma hili kuliripotiwa makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani kwenye mji wa Conamry ambapo kulifyatuliwa risasi na watu kujeruhiwa. Makabiliano hayo yanajiri kufuatia mauaji ya watu 6 na wanajeshi [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi kutoka Syria waendelea kuwasili nchini Lebanon

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa kuna ongezeko kwa wakimbizi kutoka Syria wanaowasili mashariki bonde la Bekaa nchini Lebanon ikikadiriwa kuwa takriban watu 2,200 wamewasili eneo hilo juma lililopita. Hata hivyo wakimbizi wanaowasili kaskazini mwa Lebanon wamesalia kuwa ni watu 400 wanaowasili kila siku. UNHCR inaweka laini mpya za simu ili [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kutolewa ripoti juu ya ubadilishanaji madaraka Maldives

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anafurahishwa na kukaribisha ripoti iliyotolewa na kamishna ya Maldives iliyoundwa kuchunguza mazingira yaliyosababishwa kubadilishwa madaraka kulikofanyika mwezi February mwaka huu. Kwa mujibu wa msemaji wake, Ban amezitolea mwito pande zote kukubali matokeo hayo ya ripoti hiyo na kuweka vinyongo pembeni na kuanza utekelezaji wake. Ametaka [...]

31/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ECHO yaipiga jeki IOM kutekeleza miradi ya wahamiaji Zimbabwe

Kusikiliza / wahamiaji wa Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji nchini Zimbabwe IOM limepokea kiasi cha euro milioni 1 kutoka kwa kamishna ya Umoja wa Ulaya inayozingatia masuala ya dhaura na usamaria mwema ECHO. Kiwango hicho cha fedha kinatazamia kusaidia kukamilisha mradi ambao umelenga kuwafadhilia jamii ya wahamiaji ambao wapo kwenye mkwamo. Sehemu kubwa ya mradi huo [...]

31/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia nchini Syria wanakabiliwa "maangamizi ya kimkakati"

Kusikiliza / Jan Eliasson

Kundi ya raia nchini Syria ikiwemo watoto na wanawake wanakabiliwa na kile kinachoelezwa na afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa " maangamizi ya kimkakati" Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson kiasi cha watu milioni 2.5 ikiwemo wakimbizi wa Kipalestina na Iraq wapo kwenye maisha ya taabu na dhiki kubwa. [...]

31/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Serikali ni lazima zishirikiane katika mitazamo kuhusu sekta ya Posta:UM

Kusikiliza / kenya stamps.jpg2

Wiki chache kabla ya kufunguliwa kongamano la kimataifa kuhusu hatma ya huduma za posta, Mkurugenzi wa mashirika maalum katika Umoja wa Mataifa, Edouard Dayan amesema serikali kote duniani zinapaswa kubadilishana mawazo kuhusu mtazamo zilizo nao kwa ajili ya sekta ya posta, ili kudumisha umuhimu wake kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja [...]

31/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya Wasyria milioni 2.5 wanahitaji msaada:UM

Kusikiliza / Jan Eliasson

Zaidi ya watu milioni 2.5 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini Syria, lakini ombi la misaada hiyo limefadhiliwa kwa asilimia 50 tu, amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson. Bwana Eliasson amesema kuwa amesema anataraji kuwa juhudi za kuwafikia watu wanaohitaji msaada nchini Syria zitaungwa mkono, na kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuchagiza [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi waliokimbia Libya kwenda Tunisia sasa kupewa makazi Ujerumani:IOM/UNHCR

Kusikiliza / wahamiaji kutoka Libya

Baada ya miezi 18 ya kusubiri katika kambi ya muda iliyopo kilometa saba kutoka mpaka wa Libya na Tunisia sasa wakimbizi 195 wataondoka Jumatatu ijayo kwenda kuanza maisha mapya nchini Ujerumani. Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa ndege itakayowasafirisha kutoka Djerba kuelekea Frankfurt kwa niaba ya [...]

31/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwenye siku ya watu waliotoweka, familia zisaidiwe kufahamu ni nini kilichofanyika:ICRC

Kusikiliza / familia za watu waliotoweka

Familia za watu waliotoweka kote duniani kutokana na migogoro ya silaha na hali nyingine za dharura, zinakabiliana na uchungu wa kutopata habari zozote kuwahusu watu hao. Wakati serikali husika zina wajibu chini ya sheria ya kibinadamu ya kimataifa kufanya vyovyote vile kutambua ni nini kilichofanyika kwa wale walotoweka, bado kunahitajika kujitolea zaidi ili kuzisaidia familia [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa mahakama ya Israel kuhusu kesi ya Rachel Corrie haukuonyesha haki na uajibikaji:UM

Kusikiliza / Richard Falk

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Wapalestina yalokaliwa, Richard Falk, amelaani uamuzi ulofanywa wiki hii na jaji mmoja wa Israel wa kuzuia kesi ilowasilishwa na familia ya mwanaharakati wa Kimarekani aliyeuawa na tingatinga Gaza, mwaka 2003 Katika taarifa yake, Bwana Falk amesema uamuzi wa jaji huyo [...]

30/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani vikali mauaji yanayoendelea Iraq na kutaka yakomeshwe

Kusikiliza / Iraq

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kunyonga watu kinyume na sheria na mauaji ya kiholela, Christof  Heyns, amelaani vikali mauaji yalofanywa siku ya Jumatatu ya watu 21 nchini Iraq, wakiwemo wanawake watatu. Siku mbili baadaye, watu wengine 5 waliripotiwa kunyongwa, kufanya idadi ya watu walouawa tangu Januari 1 2012 kufika watu 96. Bwana Heyns [...]

30/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto ni taswira ya Mali ya matatizo ya chakula na lishe:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos

Watoto ndio taswira ya matatizo ya chakula na lishe nchini Mali na eneo zima la Sahel amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja nwa Mataifa bi Valarie Amos baada ya nkukamilisha ziara yake nchini humo. Bi Amos alitembelea kituo cha lishe cha Gabriel Toure mjini Bamako ambacho kinatibu watoto zaidi [...]

30/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Homa ya Kidingapopo iaongezeka duniani:WHO

Kusikiliza / mosquito-malaria-who

Shirika la afya duniani WHO limechapisha ripoti inayoonyesha kwamba homa ya kidingapopo inaongezeka duniani. Kwa mujibu wa shirika hilo katika miongo mitano iliyopita matukio ya kuzuka kwa homa ya kidingapopo yameongezeka mara 30 . Kumekuwa na visa vipya kati ya milioni 50 hadi 1000 vinavyokisiwa kuzuka kila mwaka katika zaidi ya nchi 100. Ripoti inasema [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali zakutana Bangkok kujiandaa kwa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Doha:UNFCCC

Kusikiliza / UNFCCC

Wawakilishi wa serikali kutoka kote duniani wameanza kukutana katika mji wa Bangkok ili kujiandaa kwa ajili ya maazimio yatakayofikiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika mjini Doha, Qatar. Kwa mujibu wa msimamizi wa mpango wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (UNFCCC) Christiana [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukulima wa mijini ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika:FAO

Kusikiliza / FAO

Idadi ya watu mijini katika bara la Afrika inaongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko eneo jingine lolote lile, lakini mingi ya miji yenyewe haishikamani na ongezeko la mahitaji ya chakula yanayotokana na ukuaji huo wa idadi ya watu, limesema shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO. Katika ripoti yake mpya iitwayo, Growing [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya Gambia yanarudisha nyuma juhudi za kulinda haki za binadamu: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema kuwa amesikitishwa sana kuwa baada ya miaka 27 bila kutekeleza rasmi hukumu ya kunyonga nchini Gambia, wafungwa tisa walohukumiwa kifo waliuawa wiki hii kwa kufyatuliwa risasi katika tukio lililoonyesha kupiga hatua nyuma katika ulinzi wa haki za binadamu nchini humo. Bi Pillay [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka Iran kujenga uaminifu kuhusu mipango yake ya nyuklia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban nchini Iran

Hakuna tishio kwa amani na usalama wa dunia lililokubwa kuliko mipango ya nyuklia amesema Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Alhamisi akizungumza kwenye mkutano wa 16 wa nchi zisizofungamana na upande wowote NAM unaofanyika nchini Iran. Ban amesema Iran kuanza uongozi wa NAM inapata fursa ya kudhihirisha kwamba inaweza kukuchukua jukumu muhimu na [...]

30/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM lataka kukakimilika kwa amani kipindi cha mpito nchini Somalia

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha kupitishwa kwa katiba mpya nchini Somalia, kuchaguliwa kwa bunge pamoja na kuteuliwa kwa spika ambapo limetoa wito kwa pande zote kushirikiana kuhakikisha kuwa kipindi cha mpito kumekamilika kwa njia ya amani. Professor Mohammed Osman Jawari alichaguliwa kama spika kwa bunge jipya uchaguzi ambao uliweka msingi wa kuteuliwa [...]

30/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka Ufaransa kuheshimu sheria za kimataifa

Kusikiliza / Roma displaced

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki ameitaka serikali ya Ufaransa kutoziendelea kinyume sheria za kimataifa zinazoangazia kutokuwepo kwa ubaguzi wakati inapotekeleza hatua ya kuyahamisha makazi ya Kiroma na kuwarejesha wahamiaji wake. Ufaransa imedaiwa kuendesha operesheni ya kuwarejeresha makwao wahamiaji kadhaa ikiwemo wale walioko katika miji ya Lille, Lyon na Paris. [...]

30/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM yazileta pamoja Israel, Lebanon kujadilia mzozo wa mpakani

Kusikiliza / UNFIL Lebanon

Maafisa kutoka Israel na Lebanon wamekutana kwa majadiliano ya utanzuaji wa hali ya shaka shaka ya mpaka ambayo yanatishia kudumaza hali ya usalama kwa upande zote mbili. Chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa pande zote mbili zimeanzisha majadiliano hayo ambayo kimsingi yanafanyika kwa ajili ya kuepusha hali kutoaminiana kama ilivyoshuhudia hapo awali kiasi cha [...]

30/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Iran ina wajibu muhimu wa kutekeleza katika eneo la Mashariki ya Kati:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa Iran ina fursa ya kutekeleza wajibu muhimu katika kanda ya Mashariki ya Kati na katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimataifa. Bwana Ban ambaye yuko ziarani nchini Iran, ametoa ujumbe wa hongera kwa serikali ya Iran kwa kufanywa mwenyekiti wa jumuiya ya mataifa yasoegemea upande [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kufanya majaribio ya silaha za nyuklia bado ni hatari kwa afya ya mwanadamu na amani duniani:Ban

Kusikiliza / peace2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kufanya majaribio ya silaha za nyuklia kunahatarisha afya ya mwanadamu na amani na utulivu kote duniani. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake kwenye siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya silaha za nyuklia, ambayo huadhimishwa kila Agosti 29. Bwana Ban amesema kuwa siku ya leo [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea nyumbani yaongezeka

Kusikiliza / wakimbizi wa Afghanistan

  Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan waliorejea nyumbani kwa kipindi cha miezi minane ya kwanza ya mwaka 2012 kutoka Pakistan, Iran na nchi zingine imepita wakimbizi 50,000. Takariban wakimbizi 213 wamekuwa wakirejea Afghanistan kila siku ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 wakati kama huo mwaka uliopita ambapo wakimbizi 190 walikuwa wakirejea nyumbani kila siku. Wakimbizi [...]

29/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Washiriki wa ‘Myfishbowl’ wachangisha chakula kwa watoto wa shule nchini Lao

Kusikiliza / mchezo wa 'myfishbowl'

Mchezo "MyFishBowl" ambao ni wa kichina kwenye mtandao wa Facebook umezindua kampeni ya mtandao ya juma moja inayojulikana kama "Hatua Dhidi ya Njaa" kwa ushirikiano na shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Kwa siku Moja washiriki kwenye mchezo huo walichangisha zaidi ya dola 100,000 zinazoweza kuwalisha watoto 300,000 wa shule walio kwenye mpango wa [...]

29/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa UM wazindua mkakati wa viwango wastani vya kimataifa vya kudhibiti silaha ndogondogo

Kusikiliza / silaha

  Mkutano wa wiki mbili unaorejelea mpango wa kuchukua hatua kuhusu silaha ndogondogo haramu umeingia siku yake ya tatu, ambapo imefanyika hafla ya uzinduzi wa viwango wastani vya kimataifa vya kudhibiti silaha ndogondogo. Kikao cha leo pia kimeangazia ufuatiliaji wa usambazaji wa silaha haramu na jinsi ya kukabiliana na athari za silaha hizo, pamoja na [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Warsha ya wanafunzi wanaoandaa mijadala inayoiga UM yakamilika mjini New York

Kusikiliza / wanafunzi

Warsha ya kuelimisha wanafunzi na walimu kuhusu jinsi shughuli za Umoja wa Mataifa zinavyoendeshwa imekamilika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Warsha hiyo ya siku tatu, iliandaliwa na idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuelimisha watu kuhusu jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi, na imewaleta pamoja wanafunzi 50 na [...]

29/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yataka kulindwa kwa sehemu za kitamaduni nchini Libya

Kusikiliza / sehemu za kitamaduni Libya

Mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa uharibifu wa maeneo ya kitamaduni unaondelea nchini Libya hautakubalika. Bokova ameelezea wasi wasi wake kutoka na uvamizi kwenye maeneo haya akisisitiza kuwa uvamizi huu ni lazima ukomeshwe ikiwa Libya inahitajika kukamilisha mabadiliko kuekea demokrasia. Kulingana na vyombo vya [...]

29/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM nchini Somalia wapongeza kuchaguliwa kwa Spika wa Bunge

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia umepongeza kuchanguliwa kwa spika mpya wa bunge nchini humo ukiutaja kama hatua kubwa kwa taifa hilo ambalo limekumbwa na vita vya muda mrefu. Professor Mohammed Osman Jawari alichaguliwa kwa wingi kwenye uchaguzi uliofanyika katika kituo cha kuwapa mafunzo polisi mjini Mogadishu ambapo watu 230 walishirki. Mjumbe wa katibu [...]

29/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji kwenye eneo la Masisi nchini DRC

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Makundi ya waasi yanaripotiwa kuwaua raia kadhaa na kuwalazimu wengine kuhama makwao tangu mwanzo wa mwezi huu wa Agosti kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa makundi hayo yaliyojihami yaliendesha uvamizi wa kikatili kwa raia uvamizi ambao umetajwa kuwa ukiukaji [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya kulinda amani Ivory Coast vyaongezwa kwenye maeneo ya ukaguzi

Kusikiliza / UNOCI

Vikosi vya kulinda amani nchini Ivory Coast vimeongezwa katika kile kinachoonekana ni kukabiliana na hali ya wasiwasi katika vituo vya ukaguzi kufuatia tukio la shambulizi lililosababisha vifo vya watu wanne. Watu wasiojulikana wakiwa kwenye gari walifyatua risasi kuwalenga askari wa serikali waliokuwa wakiweka doria kwenye vituo vya ukaguzi katika kijiji cha Iribo kilichopo umbali wa [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aelekea Iran kuhudhuria mkutano wa NAM

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameondoka mjini New York kuelekea mji mkuu wa Iran Tehran ambako anatazamia kuhudhuria mkutano wa jumuiya isiyofungamana na upande wowote Kandoni mwa mkutano huo wa wiki moja, Ban anatazamia kukutana na viongozi wa mataifa yanayochipukia kiuchumi kwa ajili ya majadiliano katika maaeneo mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji maamuzi yaliyofikiwa [...]

29/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waunga mkono michezo ya olimpiki ya walemavu ili kuchagiza ushiriki wa wote na amani katika jamii

Kusikiliza / michezo ya olimpiki, London

Leo michezo ya olimpiki ya walemavu imefunguliwa rasmi mjini London Uingereza kwa washiriki zaidi ya 4200 kutoka nchi 166 wakishindana katika michezo 21. Kwa mtazamo wa Umoja wa Mataifa michezo ya olimpiki ya walemavu ni michezo inayotoa fursa muhimu ya kujumuisha wote na kuwawezesha watu wenye ulemavu kupitia michezo na pia ni kusherehekea kuishi kwa [...]

29/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO katika jitihada za kuangamiza minyoo ya Guinea

Kusikiliza / maji safi

  Shirika la afya duniani WHO linafanya jitihada za kukabiliana na minyo ya Guinea baada ya visa 396 vya ugonjwa huo kuripotiwa kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya mwaka huu na asilimia kubwa ya visa hivyo ikiripotiwa nchini Sudan kusini huku visa 2 vya ugonjwa huo vikiripotiwa nchini Mali, Chad kisa kimoja na [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado watu milioni 18 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Sahel

Kusikiliza / njaa katika eneo la Sahel

Eneo la Sahel magharaibi mwa afrika bado linapitia hali ngumu wakati watu milioni 18 wakiwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Watoto milioni 4 walio chini ya miaka mitano kwa sasa wanakabiliwa na utapiamlo. Nchini Mali ukame na ukosefu wa usalama vimewalazimu zaidi ya [...]

28/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji ya mfanyikazi wake nchini Somalia

Kusikiliza / wafanyakazi wa FAO

Umoja wa Mataifa umelaani maauaji ya mfanyikazi wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Matifa FAO kwenye eneo la Marka kusini mwa Somali. Tangu Agosti mwaka 2011 watoa huduma za kibinadamu 20 wameuawa nchini Somalia wanapojitahidi kutoa huduma kwa mamilioni ya watu wanaoteseka nchini humo. Idadi ya raia wa Somalia wanaopokea misaada imeongezeka [...]

28/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto wasio na wazazi kutoka Syria wanazidi kukimbilia usalama nchi majirani

Kusikiliza / watoto wa Syria

Mzozo unaoendelea nchini Syria umewalazimu mamia ya watoto wasio na wazazi kukimbilia usalama kwenye nchi majirani kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Watoto wanaopokelewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kwenye kambi ya Za'atri nchini Jordan wanasema kuwa wazazi wao wamekufa au wamebaki nyuma kuwatunza wengine na [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM kuzuru Honduras kuchunguza uzalishaji watoto

Kusikiliza / Najat Maalla M'jid

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ustawi wa watoto katika maeneo ya ngono, Najat Maala M'jid anatazamia kufanya ziara yake ya kwanza nchini Honduras kuchunguza madai ya uuzwaji watoto, pamoja na kutumikishwa kwenye vitendo vya ngono. Ziara hiyo inayotazamiwa kuanza August 30 hadi Septemba 7 inakuja kufuatia mwaliko uliotolewa na serikali ya Honduras [...]

28/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaanzisha tamasha kuelimisha uhamiaji haramu Ethiopia

Kusikiliza / wahamiaji

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM likishirikiana na serikali za majimbo nchini Ethiopia imeanzisha tamasha lililopewa dhima ya Mutach yaani yule aliyepotea kwa shabaha ya kutoa elimu inayoelezea athari za kuwepo kwa wahamiaji haramu katika maeneo ya vijijini. Tayari tamasha hilo limeanzishwa kwenye maeneo ya vijijini na linatazamiwa kudumu hadi mwezi Octoba [...]

28/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Global Fund yaidhinisha dola milioni 400 za misaada mipya

Kusikiliza / Global Fund

Halmashauri ya mfuko wa ufadhili wa kimataifa katika kukabiliana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, Global Fund, imeidhinisha maombi 45 mapya ya ufadhili kutoka kwa nchi 37 kwa muda wa miaka miwili. Fedha hizo, jumla ya dola milioni 419.2, zinatarajiwa kufadhili miradi ya kuzuia, kutibu na huduma za uuguzi kwa watu walioathiriwa na magonjwa hayo [...]

28/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika kuhakikisha mamilioni ya watu wanapata maji safi ya kunywa:UNICEF

Kusikiliza / maji safi

Licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika karne mbili zilizopita kuwawezesha mabilioni ya watu kupata maji safi ya kunywa, kuhitimisha kazi hiyo hakutakuwa rahisi, limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, mwanzoni mwa Juma la Kimataifa la Maji. Kwa mujibu wa UNICEF, kumekuwa na ufanisi mkubwa katika kila eneo la ulimwengu, lakini kazi [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaohama Yemen kutoka pembe ya Afrika imefurutu ada:UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema idadi ya wakimbizi kutoka Pembe ya Afrika wanaoelekea Yemen kupitia Ghuba ya Adeni na Bahari ya Sham inaendelea kuzidi viwango vya awali. Katika miezi 7 ya kwanza mwaka 2012, zaidi ya watu 63, 000 walifanya safari hiyo ngumu, ikilinganishwa na watu 48, 700 wakati kama [...]

28/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Gambia yatakiwa kusitisha mauaji ya watu 39 waliohukumiwa kifo:UM

Kusikiliza / Christof Heyns

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yaliyo ya halali, au kunyonga kiholela Christof  Heyns ameitaka serikali ya Gambia kujizuia na kutotekeleza mauaji ya watu 39 ambao wako kwenye orodha ya waliohukumiwa kifo, kufuatia kunyongwa kwa watu tisa Agosti 26 mwaka huu. Kabla ya mauaji haya utekelezaji wa hukumu ya kifo ya mwisho rasmi [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tufani Isaac imedhihirisha haja ya kufunga makambi Haiti:IOM

Kusikiliza / kambi nchini Haiti

Tufaini Isaac iliyokumba Haiti mwishoni mwa wiki imedhihirisha haja ya kuyafunga makambi 575 yaliyosalia nchini humo tangu tetemeko la ardhi la mwaka 2010, na kutoa huduma ya makazi bora kwa watu 390,000 ambao bado wanaishi kwenye mahema. Kwa mujibu wa Luca Dall'Oglio mkuu wa mpango wa msaada wa IOM Haiti makambi hayo yamenusurika safari hii [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasyria wanaokimbilia Jordan watasababisha wimbi kubwa la wakimbizi:UNHCR

Kusikiliza / makambi, Jordan

Kiwango cha watu wanaowasili kutoka kwenye mpaka wa Syria na kuingia kwenye kambi ya Za'atri Kaskazini mwa Jordan kimeongezeka mara mbili wiki iliyopita limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Wati zaidi ya 22,000 wamepokelewa katika kambi ya Za'atri tangu ilipofunguliwa Julai 30 mwaka huu. Wakimbizi hao wanasema wenzao kwa maelfu bado [...]

28/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka ulinzi zaidi wa raia baada ya mauaji ya kinyama Afghanistan

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa UM afghanistan Jan Kubis

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mauaji ya kinyama ya raia 17 wa Afghanistan, ambao baadhi yao waliuawa kwa kuchinjwa, na kutaka wahusika kuchukulia hatua za kisheria. Kwa mujibu wa duru za habari, miili ya wanawake wawili na wanaume 15 ilipatikana kando ya barabara katika jimbo la kusini la Helmand. Miili hiyo ilionyesha dalili kuchinjwa kwa [...]

27/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani kuzuka upya machafuko Sudan Kusini

Kusikiliza / Bi Hilde Johnson

Mwakilishi mkuu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini amelaani shambulizi lililotekelezwa na makundi ya waasi wenye silaha katika jimbo la Jonglei mashariki mwa taifa hilo, akisema kuwa ghasia hizo ni jaribio la kukusudia kuvunja hatua zilizopigwa katika barabara ya kuleta amani na maridhiano nchini humo. Bi Hilde Johnson, ambaye ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika kudhibiti usambazaji wa silaha ndogondogo: Ban

Kusikiliza / arms_big_4

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa serikali kote duniani kufanya juhudi zaidi ili kukomesha usambazaji wa silaha ndogondogo haramu. Katika ujumbe ulowasilishwa na naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, Bwana Ban amesema kuwa silaha ndogondogo haramu zinabaki kupendelewa na wale wanaotaka kuasi uongozi wa kisheria, kueneza hofu na kuzorotesha usalama, pamoja [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM kuhusu Gaza yasisitiza umuhimu wa kuondoa vikwazo

Kusikiliza / GAZA-BLOCKADE

Umoja wa Mataifa umesisitiza umuhimu wa kuondoka vikwazo na vizuizi dhidi ya Ukanda wa Gaza, ili kupunguza mateso na hali ngumu ya maisha kwa Wapalestina. Katika ripoti yake inayohoji ikiwa hali ya ukanda wa Gaza itaendelea kuwepo mwaka 2020, wawakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA pamoja na Shirika la [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa ombi la dola milioni 54 kugharamaia mahitaji kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Syria

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 54 ili kugharamia mahitaji yanayoongezeka kwa maelfu ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan, hasa kwa watoto. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linasema kuwa fedha hizo zinahitajika kwa dharura kugharamia huduma za afya na za usafi na maji kwa wakimbizi wanaoendelea kuwasili nchini Jordan. [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wafanya maadhimisho ya kwanza tangu shambulizi kwenye makao yake Abuja, Nigeria

Kusikiliza / mashambulizi yaliyofanyika Abuja, Nigeria

Umoja wa Mataifa nchini Nigeria umefanya maadhimisho ya kwanza kabisa tangu kutokea kwa shambulizi la bomu kwenye makao yake mjini Abuja, ukisema kuwa shambulizi hilo halitozuia Umoja wa Mataifa kutekeleza wajibu wake nchini humo. Watu 23, wakiwemo wafanyikazi 13 wa Umoja wa Mataifa na 10 wasiokuwa wafanyikazi, waliuawa huku zaidi ya watu wengine 120 wakijeruhiwa. [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na marafiki zake aliosoma nao miaka 50 iliyopita

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban na marafiki zake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na marafiki zake aliokutana nao kwa mara ya kwanza nusu karne iliyopita mjini Washington ambao anasema kuwa ndiyo waliompa hamasa ya kuingia kwenye utumishi wa umma. Kusanyiko hilo ambalo liliratibiwa na chama cha msalaba mwekundi cha Marekani limetoa fursa kwa pande zote mbili kubadilishana mawazo na [...]

27/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM nchini Somalia wataka shughuli ya kuwachagua mabunge wapya

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga, Somalia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia umeelezea wasi wasi wake kufutia kuendelea kucheleshwa kukamilishwa kwa orodha ya wabunge wapya ukionya kuwa huenda hali hilo ikavuruga mipango ya uchaguzi. Baada ya miaka mingi ya vita Somalia imekuwa kwenye mchakato wa kutafuta amani ambapo serikali ya mpito ilitekeleza kinachojulikana kama barabara ya amani. Kati ya hatua [...]

27/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa IAEA ahimiza hatua ichukuliwe haraka kutekeleza mpango wa usalama wa nguvu za kinyuklia

Kusikiliza / Yukiya Amano

Wawakilishi wa nchi 75 wanachama wa mkataba kuhusu usalama wa nyuklia (CNS), wanakutana mjini Vienna Austria kuanzia leo hadi Ijumaa Agosti 31 ili kurejelea suala la usalama wa nguvu za nyuklia baada ya ajali ilotokea kwenye kiwanda cha Fukushima Daiichi nchini Japan. Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kwanza cha mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa [...]

27/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

OCHA yaendelea kukagua hali ya mambo Haiti baada ya Tufani ya Isaac

Kusikiliza / tufani Isaac,  Haiti

Ofisi ya mratibu mkuu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, inaendelea kufanya ukaguzi wa uharibifu ulofanyika nchini Haiti kutokana na tufani ijulikanayo kama Isaac hivi karibuni. Watu sita wameripotiwa kufariki dunia kutokana na tufani hiyo, akiwemo msichana mwenye miaka 8. Maeneo 41 ya makazi ya dharura yamefunguliwa huku vyakula na maji vikisambaziwa [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame unaojirudia ni ishara ya haja ya kudhibiti rasilimali ya maji na kulinda usalama wa chakula

Kusikiliza / ukame

Ukame katika baadhi ya maeneo duniani umeathiri uzalishaji wa chakula na kuchangia kupanda kwa gharama za chakula kila mwaka tangu mwaka 2007, ikiashiria haja ya kubadili jinsi maji yanavyotumika na kupotea katika mfumo mzima wa uzalishaji wa chakula. Huu ni moja ya ujumbe maalumu uliotolewa na shirika la kilimo na chakula FAO wiki hii katika [...]

27/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tuzo ya kwanza ya hatari ya majanga ya UNISDR yaenda kwa Msumbiji

Kusikiliza / beira

Mji wa pwani ulioathirikana mafuriko wa Beira nchini Msumbiji umetajwa Jumatatu ya leo kuwa mshindi wa tuzo ya kwanza ya hatari ya majanga iliyotolewa kwa ushirikiano wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza majanga UNISDR, wakfu wa Munich na kongamano la kimataifa la hatari ya majanga Davos. Tuzo hiyo ambayo ni Euro 100,000 ni [...]

27/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la kujadilia nafasi ya "wana Diaspora" kusukuma shughuli za maendeleo laanza Ghana

Kusikiliza / diaspora-accra

Kongamano la kimataifa lenye dhima ya kujadilia umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya ukuzaji uchumi kwa raia walioko nje ya nchi zao yaani diaspora limeanza leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra . Kongaamano hilo linawajumuisha pia wajumbe kutoa mashirika ya kiraia pamoja na taasisi huru za kibiashara. Kwa muda wa siku tatu, wajumbe [...]

24/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa fuko la UM juu ya mabadiliko ya tabia nchi wakutana kwa mara ya kwanza

Kusikiliza / UNEP

Mpango wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa kwa ajili ya kukusanya rasilimali zitakazowezesha kurahisisha juhudi za kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi umeanzisha mkutano wake wa kwanza. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2011 wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya mazingira na maendeleo huko Durban, Afrika Kusin unashabaha ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana [...]

24/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kitengo cha UN Women chatia saini mkataba na Kamati ya Olimpiki kuendeleza usawa wa kijinsia

Kusikiliza / Michelle Bachelet

Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa, yaani UN Women, kimetia saini mkataba wa ushirikiano na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ili kuendeleza juhudi za kuwapa wanawake uwezo zaidi kupitia katika michezo. Kwa niaba ya UN Women, Mkurugenzi Mkuu Michelle Bachelet ametia saini mkataba huo na kamati ya Olimpiki, ikiwakilishwa na rais wa kamati hiyo, [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaanda mkutano kuhusu uhamiaji kusini mwa Afrika nchini Mauritius

Kusikiliza / nemba ya IOM

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na ofisi inayohusika na uhamiaji na maendeleo nchini Mauritius wanatarajiwa kuandaa mkutano kuhusu uhamiaji kwenye nchi za kusini mwa Afrika wenye lengo kuunga mkono uhamiaji kwa minajili ya maendeleo ya kuchumi na kijamii kwenye nchi za SADC. Mkutano huo wa siku mbili ambao inaong'oa nanga Agosti 27 mjini Balaclava [...]

24/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM na washirika wajiandaa kutoa misaada wakati tufani Isaac inapoelekea Haiti

Kusikiliza / tufani Isaac

Serikali imeyaomba mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao wajiandae kukabiliana na athari za tufani Isaac. Mashirika la Umoja wa Mataifa na washirika wameanzisha shughuli ya kuhamisha bidhaa za misaada nchini Haiti kwenyewe na kutoka nchini Panama. Kati ya bidhaa hizo ni pamoja na chakula kinachoweza kuwalisha watu 35,000, vifaa vya kutoa makao na [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kiafaya kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini yatia wasi wasi:UNHCR

Kusikiliza / hali ya wakimbizi sudan kusini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema lina wasi wasi kufuatia hali ya kiafya kati ya wakimbizi 170,000 kutoka Sudan ambao bado wamesalia kwenye kambi na maeneo mengine kwenye majimbo ya Unity na Upper Nile nchini Sudan Kusini. UNHCR inasema kuwa mvua zinazonyesha na baridi vimesababisha magonjwa ya kupumua , kuendesha na [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za kuwasaidia wakimbizi kutoka Syria zaanza:UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kuendelea kuzoroteka kwa hali ya usalama nchini Lebanon kunazuia oparesheni zake. Wakimbizi wanaendelea kuingia nchini Lebanon hasa kutoka miji ya Damascus, Aleppo na Daraa huku kukiwa na karibu wakimbizi 51,000 kutoka Syria nchini Lebanon waliotuma maombi au waliojiandikisha na UNHCR. Wakimbizi 74,000 tayari wameandikishwa [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muziki wa asili barani Afrika

Kusikiliza / muziki wa asili barani Afrika

Pamoja na msukumo mkubwa unaochagizwa na maendeleo katika sekta ya sayansi na teknolojia, lakini kwa kiwango kikubwa muziki wa asili barani Afrika unaendelea kusalia kwenye ramani ya juu, ukiwavutia watu wa rika zote. Basi katika makala yetu George Njogopa anatupia jicho nafasi ya mziki huo, na akiangazia pia kongamano moja la kimataifa lililofanyika jijini Dar [...]

24/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS yatoa wito hatua ichukuliwe kulinda jitihada za amani katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini

Kusikiliza / UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Sudan Kusini, UNMISS, umetoa wito kwa taasisi zote katika Sudan ya Kusini na wadau wengine wanaohusika katika kuimarisha jimbo la Jonglei kuchukuwa hatua mara moja, ili kulinda ufanisi uliofikiwa katika jitihada za kutafuta amani, kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu katika kata ya Pibor, na kuwafikisha wahalifu mbele ya [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Afrika inaweza kuwasaidia zaidi wachimba migodi:ILO

Kusikiliza / madini Afrika ya Kusini

Mauaji ya wachimba migodi zaidi ya 30 kwenye machimbo ya Marikana wiki iliyopita yamedhihirisha hali ya kufanya kazi katika sekta ya migodi nchini Afrika ya Kusini. Kwa mujibu wa mtaalamu wa uchimbaji madini wa shirika la kazi ILO Martin Hahn, Afrika ya Kusini imechukua hatua kubwa tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, lakini [...]

24/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam huru wa UM wahimiza kukomeshwa ukatili dhidi ya wanaotetea haki za binadamu Bahrain

Kusikiliza / manama

Kundi la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa, leo limeelezea wasiwasi wake kuhusu kampeni ya ukatili unaotekelezwa na uongozi wa Bahrain dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo. Wataalam hao wameitaka serikali ya Bahrain kumwachilia huru mara moja mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu, Nabeel Rajab, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela [...]

23/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa aelezea hofu yake kuhusu ghasia Lebanon

Kusikiliza / Lebanon

Naibu mratibu mkuu wa maswala ya Lebanon katika Umoja wa Mataifa, Robert Watkins, amesema kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifuatilia kwa karibu matukio ya hivi karibuni ya kiusalama nchini Lebanon, yakiwemo utekaji nyara wa raia wa Syria na wengine nchini humo. Bwana Watkins amesema hayo katika ujumbe wake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa [...]

23/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Filamu kuhusu utunzi wa maji yazinduliwa

Kusikiliza / utunzi wa maji

Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na wizara ya mazingira nchini Korea Kusini wana mipango ya kuweka filamu fupi kwenye mtandao kuhusu upatikanaji wa maji safi na mazingira safi yenye lengo la kuweka sera kuhusu usimamizi wa maji na pia kutoa hamasisho kuhusu masuala ya maji. Maji ni muhimu kwa [...]

23/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNAMID waripotiwa kupotea Sudan

Kusikiliza / askari wa UNAMID

Duru kutoka nchini Sudan zinasema kuwa askari wawili wa vikosi vya kulinda amani vya muunganiko wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID hawajulikani waliko na tayari juhudi za kuwasaka vimeanzishwa. Afisa mmoja wa UNAMID amesema kuwa askari hao walipotea tangu tarehe 20 mwezi huu wa August katika mji wa Kabkabiya ulioko kilometa 140 [...]

23/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mafuriko yawaua watu 45 na kuathiri wengine 345,000 Niger

Kusikiliza / mafuriko, Niger

Zaidi ya watu 45 wamefariki kutokana na mafuriko nchini Niger, huku watu wengine zaidi ya laki tatu na arobaini na tano elfu wakiwa wameathiriwa na mafuriko hayo, kwa mujibu wa Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo, Modibo Traore. Watu wamepoteza mali zao kwa wingi, ikiwemo mimea ambayo [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kutatua mzozo wa Syria ni lazima ziendelee:Jan Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson

Bado kuna fursa ya kupata suluhu ya kisiasa kwa mzozo wa Syria, amesema naibu Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson. Katika mahojiano na Maha Fayek wa Radio ya Umoja wa Matifa, Bwana Eliasson amekaribisha kuteuliwa kwa Bwana Lakhdar Brahimi hivi karibuni kama mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya [...]

23/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Naibu Katibu Mkuu wa UM asisitiza umuhimu wa kutatua mizozo kwa njia ya amani

Kusikiliza / Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesisitiza umuhimu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro kwa njia ya amani Mwanadiplomasia huyo kutoka Uswiss amesema sehemu za mkataba anazofurahia zaidi ni sura mbili. Moja ni sura ya VI ambayo inahusika na kutuatua mizozo kwa njia ya amani na sura ya VII [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utafiti mpya wachunguza jinsi shule zinavyofundisha historia ya mauaji ya kimbari ya wayahudi ya Holocaust

Kusikiliza / Holocaust

Ni vipi shule kote duniani zinafundisha suala la Holocaust, yaani mauaji ya kimbari ya wayahudi wanaokadiriwa kuwa milioni sita, yalotekelezwa na serikali ya Adolf Hitler? Na ni katika maeneo yapi duniani kunakofundishwa historia ya Holocaust? Majibu kwa maswali haya yanatarajiwa kupatikana kutokana na mradi unaosimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yatoa wito kwa ulimwengu kuwazia suala la Utumwa

Kusikiliza / utumwa

Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya kukumbuka biashara ya utumwa na kupigwa marufuku biashara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, amewasihi watu wote ulimwenguni kuwazia mabadiliko yaloletwa na biashara ya utumwa duniani, na kutoa wito kwa mataifa kuwalinda raia wao dhidi ya ubaguzi wa rangi na ajira za utumwa. [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni bora kupunguza majanga kwa kuangazia mazingira:UNEP

Kusikiliza / majanga

Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limetaja kuangazia mazingira kama jambo muhimu katika kuweka tahadhari dhidi ya majanga, mbele ya kongamano la kimataifa kuhusu majanga. Haja ya kukomesha mwendo wa pole katika kugeuza fikra kuhusu tahadhari na majanga kuwa vitendo, ni mojawepo ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la kimataifa kuhusu [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka Marekani kufanya mazungumzo na watu wa asili kuhusu uuzaji wa ardhi

Kusikiliza / James Anaya

Mtaalamu huru kutoka Umoja wa mataifa ametoa wito kwa serikali ya Marekani na utawala kwenye jimbo la South Dakota kuanza mazungumzo na watu wa asili kuhusu suala la uuzaji wa ardhi ambao huenda ukaathiri eneo lenye umuhimu kwa kidini kwao. Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za jamii za kiasili James Anaya [...]

23/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UNAMID kupunguza mvutano Darfur Kaskazini

Kusikiliza / kikosi cha UNAMID

Ujumbe wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kulinda amani Darfur UNAMID umezuru eneo la Mellit, Darfur Kaskazini Agosti 21 kukutana na viongozi wa kijamii ili kupunguza mvutano baina ya makabila makubwa ya Ziyadiah na Berti. Kiongozi wa ujumbe huo wa UNAMID, Hassan Gibril, ameelezea hofu yao kutokana na matukio [...]

23/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa kwanza wakamilishwa chini ya WIPO kutafiti maradhi yaliyopuuzwa

Kusikiliza / nembo ya WIPO

Utafiti wa kutengeneza tiba ya maradhi yaliyopuuzwa yanayoathiri nchi za hari au tropic umepata msukumo mwezi huu wakati kampuni ya AstraZeneca ilipokamilisha makubaliano kupitia WIPO na kampuni ya dawa ya IThemba ya Afrika ya Kusini, Chuo kikuu cha Califonia, cha San Francisco Marekani na chuo kikuu cha Dundee chanUingereza. Mikataba hiyo mitatu ni ushirikiano wa [...]

23/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Muafaka wa mataifa mawili huru ndilo suluhisho pekee kwa mzozo wa Israel na Palestina:UM

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Licha ya kuwepo mkwamo katika mazungumzo kati ya Waisraeli na Wapalestina, muafaka wa mataifa mawili huru bado ndio suluhu inayofaa, amesema mkuu mpya wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman, wakati akilihutubia Baraza la Usalama siku ya Jumatano. Bwana Feltman amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaamini kuwa pande hizo mbili, pamoja na [...]

22/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pande hasimu nchini Syria zimeshindwa kuwalinda Raia:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos

Majeshi ya serikali na wapiganaji wa upinzani nchini Syria wameshindwa kutekeleza sheria za kimataifa za kuwalinda raia. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Jumatano baada ya kukamilisha ziara yake Syria Bi Amos amesema watu milioni 2.5 wanahitaji msaada wa haraka. Ameongeza kuwa huduma za afya, malazi, chakula, maji na safi ni miongoni ya [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban kuhudhuria mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote nchini Iran

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon atazuru Iran mwishoni mwa mwezi kushiriki katika mkutano wa 16 wa nchi zisizofungamana na upande wowote yaani NAM amesema msemaji wake. Ameongeza kuwa Ban anauona mkutano huo kama fursa nzuri ya kushirikiana na waku wa nchi na serikali wanaoshiriki mkutano huo ikiwemo mwenyeji wa mkutano katika kupata [...]

22/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa lakini bado kuna changamoto ya watu kutoweka Chile:UM

Kusikiliza / bendera ya Chile

Uchunguzi na kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya watu kutoweka kwa lazima ni mafanaikio muhimu kwa serikali ya Chile na jamii katika vita dhidi ya ukwepaji sheria kwa kukiuka haki za binadamu. Hayo yamesema na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na watu kutoweka bila hiyari yao waliohitimisha ziara yao nchini Chile. Wameongeza kuwa pamoja na [...]

22/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Urusi na Ufilipino waidhinisha makataba unaowapa mabaharia haki za kikazi

Kusikiliza / Juan Somavia

Shirika la kazi duniani ILO limetangaza viwango vya ajira kwa mabaharia milioni 1.2 wanaofanya kazi kote duniani kuhusu viwango vya kisasa vya ajira , afya na masusla ya usalama sasa vinatarajiwa kuanza kutumika baada ya kuidhinishwa. Kuidhinishwa kwa viwango hivyo vya mwaka 2006 na mataifa ya Urusi na Ufilipino kunatimiza mahitaji ya mataifa 30 wanachama [...]

22/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu Wa UNESCO alaani mauwaji ya mwandishi wa habari wa kijapan Mika Yamamoto huko Aleppo, Syria

Kusikiliza / Bi Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova amelaani vikali mauwaji ya mwandishi mmoja wa habari raia wa Japan aliyeuwawa wakati akifuatilia mapigano yanayoendelea nchini Syria. Katika taarifa yake, Bi Bokova amezilotea mwito pande zote zinahasimiana kwenye mkwamo huo kuweka mbele masuala yanayotambua uhuru wa maoni [...]

22/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM nchini Kosovo azitolea mwito jumuiya za kimataifa kulipiga jeki taifa hilo

Kusikiliza / Farid Zarif

Mkuu wa ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo amezitolea mwito jumuiya za kimataifa kuchukua hatua mpya juu ya utekelezaji mipango ya kulisaidia taifa hilo. Farid Zarif amesema kuwa jumuiya za kimataifa zinapaswa kubadilisha makusudio yao kuhusu kulipiga jeki taifa hilo tena akasisitiza kuwa zinapaswa kuonyesha vitendo halisi kwa kuanzisha malengo ya kweli. Kamishna [...]

22/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Cambodia ni mfano wa kuigwa maeneo ya Asia na Pacific kwa ajili ya maendeleo endelevu:Hayzer

Kusikiliza / Noeleen Heyzer

Mkuu wa Tume ya Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya maeneo ya Asia na Pasifik, Noeleen Heyzer, amesema kuwa taifa la Camboda linatoa mfano mzuri wa ufumbuzi na uongozi, ambao unahitajika kuigwa na mataifa ya Asia na Pasifiki katika hatua zitakazofuata za kumakinika zaidi katika ukuaji na maendeleo ya kiuchumi. Bi Heyzer amesema hayo katika [...]

22/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bhutan, Columbia, Indonesia na Rwanda zatunukiwa na UNESCO katika masuala ya elimu

Kusikiliza / nemba ya UNESCO

Mipango ya kujua kusoma na kuandika kutoka Bhutan, Indonesia, Colombia na Rwanda ndiyo iloshinda tuzo za UNESCO mwaka 2012. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova amewatangaza washindi hao leo, ambao walipendekezwa na jopo la majaji wa kimataifa. Washindi watazipokea tuzo zao kwenye hafla ambayo itafanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mnamo tarehe 6 Spetemba, kama [...]

22/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanachama wa WTO wafikia 157 baada ya Urusi na Vanuatu kujiunga

Kusikiliza / vanuatu

Jumatano Agosti 22 Urusi imekwa mwanachama wa 156 wa shirika la kimataifa la biashara WTO. Vanatu imeelezwa kwa itajiunga na shirika hilo Agosti 24 mwaka huu na kufanya idadi ya wanachama kufikia 157. Kwa mujibu wa mkrugenzi mkuu wa WTO Pascal Lamy imekuwa ni safari ndefu kwa nchi hizo mbili kufikia maamuzi ya kujiunga na [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zenawi alikuwa mfanisi katika masuala ya mazingira:UNEP

Kusikiliza / waziri mkuu wa Ethiopia

Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nalo limetuma risala kama hizo kwa serikali na wananchi wa Ethiopia, kufuatia kifo cha kiongozi wao, Meles Zenawi. Katika taarifa yake, UNEP imesema kuwa Bwana Meles ameacha sifa ya ufanisi katika masuala ya mazingira, hasa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi unaojali mazingira. [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amkumbuka Waziri Mkuu wa Ethiopia aliyeaga dunia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Waziri Mkuu Meles Zenawi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea huzuni yake kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi. Bwana Meles aliripotiwa kufariki Jumatatu jioni akiwa ng'ambo kupokea matibabu kwa ajili ya ugonjwa ambao haukutajwa. Katika taarifa yake, Bwana Ban amesema Waziri Mkuu Meles atakumbukwa kwa uongozi wake shupavu na kupigania masuala ya [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi zinaendelea kusaidia DR Congo kupambana na Ebola:WHO

Kusikiliza / ebola DRC

Juhudi zinaendelea kusaidia kudhibiti viruzi vya Ebola maradhi ambayo yameshakatili maisha ya watu tisa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema shirika la afya duniani WHO. Kwa mujibu wa Gregory Hartl msemaji wa shirika hilo kuna wafanyakazi wawili wa WHO katika eneo lililoathirika na wafanyakazi wengine wanaelekea huko kushirikiana na timu ya wizara ya [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaitaka serikali ya Tanzania kulifungulia gazeti

Kusikiliza / waandishi habari nchini Tanzania

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yameikosoa serikali kwa jinsi inavyotendea  uhuru wa vyombo vya habari na wakati huo huo yametoa siku saba kwa serikali hiyo kulifungulia gazeti moja ililolifungia vinginevyo yataanzisha maandamano ya amani nchi nzima. Mashirika hayo ni yale yanayotetea ustawi wa kijamii yakiwemo kituo cha sheria na haki za binadamu, [...]

22/08/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uzoefu wa vitendo au Internship waweza kusaidia au kutumika vibaya:ILO

Kusikiliza / ILO internships

Tarajali, au uzoefu wa vitendo ambao ni internship unaweza kutoa fursa nzuri ya uzoefu wa kazi kwa vijana, lakini pia yakizidi unaweza kuwa na hatari ya kutumika vibaya hasa wakati huu wa msukosuko wa uchumi limesema shirika la kazi duniani ILO. Katika tathimini yake ya kuangalia faida na hasara za tarajali ILO inasema wakati kiwango [...]

22/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yaipatia IOM dola 7000 kusaidia kurejesha nyumbani wakimbizi wa Liberia walioko Ghana

Kusikiliza / wakimbizi wa Liberia

Marekani imetoa kiasi cha dola 750,000 ili kufadhilia shughuli za wakimbizi wa Liberia walioko nchini Ghana ambao sasa wanakubali kurejea nyumbani kwa hiari. Inakadiriwa kwamba kiasi cha wakimbizi wa Liberia walioko katika taifa hilo la jirani kimefikia 3,500 na kutolewa kwa fedha hizo kutaliwezesha shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM kuratibu wa [...]

21/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM, Kenya zakubaliana kuanzisha mashirikiano ya kusafirisha wafanya kazi vijana

Kusikiliza / vijana nchini Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM pamoja na serikali ya Kenya kwa pamoja wamekubaliana kuanzisha mashirikiano ya miaka minne ambayo yatashuhudia idadi kadhaa ya watu wenye ujuzi wa kufanya kazi wakisafirishwa katika mataifa ya nje. Mpango huo utakapoanza kutekelezwa unakusudia kuwafaa zaidi vijana na kwa sasa inakisiwa kuwa kila mwaka kiasi cha [...]

21/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shirika la WMO laonya kuhusu ukame wa hali ya juu unaoukabili ulimwengu

Kusikiliza / ukame wa hali ya juu ulimwenguni

Shirika la Kimataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa, WMO, limesema kuwa ulimwengu unashuhudia ukame ambao ni wa hali ya kipekee. Shirika la WMO limesema ukame unayoikumba Marekani na athari zake dhidi ya bei za chakula kwenye soko la kimataifa, unaonyesha uwezo mdogo wa ulimwengu mzima kustahmili hali kama hii. Shirika hilo limesema kuwa mwaka [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awapongeza Wasomali kwa bunge jipya

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha kuzinduliwa kwa bunge jipya la taifa nchini Somalia siku ya Jumatatu, kulikofanyika katika mji mkuu Mogadishu. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma risala ya pongezi kwa watu wa Somalia kwa wakati huu wa kihistoria, katika safari yao kwenye barabara ya amani, utulivu na [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kundi la UM laitaka Tunisia kulinda mafanikio kwenye usawa na haki za binadamu kwa wanawake

Kusikiliza / wanawake kutoka Tunisia

Kundi la Umoja wa Mataifa linalohusika na masusla ya ubaguzi dhidi ya wanawake limetoa wito kwa serikali mpya ya Tunisia kuchukua kila hatua kulinda mafanikio yaliyopatikana nchini humo kuhusu usawa, kutokuwepo ubaguzi na haki za wanawake kuambatana na kanuni za kimataifa kuhusu haki za binadamu. Watalaamu hao wamewapongeza viongozi nchini Tunisia ambao wamefanya jitihada za [...]

21/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM na Japan wazindua mpango kuhusu usimamizi wa mpaka nchini Sudan Kusini

Kusikiliza / nemba ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Japan wametia sahihi makubaliano ya kuzindua mpango mpya wa kufanya kazi na serikali ya Sudan Kusini wa kuwa na kikosi cha polisi na kusimamia mipaka yake na kujenga vituo 16, katika ujenzi wa taasisi ya uhamiaji mjini Juba na kubuni mfumo wa mafunzo kuhusu usimamizi wa [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 9 waaga dunia kutokana na mkurupuko wa Ebola nchini DRC

Kusikiliza / ugonjwa wa Ebola nchini Uganda

Watu tisa wameripotiwa kuaga dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. WHO inasema kuwa takriban visa 15 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwenye maeneo ya Isiro, Pawa na Dungu kwenye mkoa wa Orientale mashariki mwa DRC. Glenn Thomas kutoka WHO anasema kuwa [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 203 waaga dunia nchini Sierra Leone kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu

Kusikiliza / kipindupindu Sierra Leone

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa watu 203 wameaga dunia nchini Sierra Leone kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu huku visa 11,189 vikiripotiwa kwenye wilaya 10 kati ya wilaya 13 . WHO inasema kuwa hata kama ugonjwa huo umedhibitiwa kusambaa kwake wakati wa msimu wa mvua ilikuwa ishara kuwa jitihada zaidi zilikuwa zikihatajika [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waonya kuhusu hatari ya homa ya nguruwe ya Afrika katika kanda ya Caucasus

Kusikiliza / ugonjwa wa homa ya nguruwe

Kufuatia kubainika kwa mara ya kwanza homa ya nguruwe ya Afrika nchini Ukraine , shirika la chakula na kilimo FAO linaonya kwamba wakati hatua za dharura zinaonekana kudhibiti ugonjwa huo, kusambaa kwa ugonjwa huo kumeonekana katika kanda ya Caucasus na kuendelea kuwa tishio katika maeneo ya jirani. Mbali ya maeneo ya Ukraine nchi za jirani [...]

21/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa yaunga mkono kumalizika kwa kipindi cha mpito Somalia

Kusikiliza / somalia

Kabla ya siku hii ya kumalizika kipindi cha mpito Somalia, jamii ya kimataifa imetoa taarifa ikikaribisha hatua zilizopigwa hadi kufikia tarehe hii ya kuhitimisha kipindi cha mpito nchini Somalia. Wawakilishi wa Muungano wa Afrika, Umoja wa Mataifa, IGAD, pamoja na mataifa ya Ethiopia, Djibouti, Italia, Norway, Uturuki, Uingereza, Marekani na Jumuiya ya nchi za Ulaya [...]

20/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Balozi Mahiga akaribisha kumalizika kipindi cha mpito

Kusikiliza / Augustine Mahiga

  Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, pamoja na jumuiya nyingine za kimataifa na nchi binafsi, zimekuwa zikijihusisha kwa njia moja au nyingine katika kusaidia kuielekeza Somalia kwenye mkondo wa kufikia utaratibu wa kikatiba na kidemokrasia. Umoja wa Mataifa ulimteua Balozi Augustine Mahiga kuwa mwakilishi maalum kuhusu Somalia. Kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, [...]

20/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge jipya nchini Somalia laapishwa katika tukio la kihistoria

Kusikiliza / Wabunge wapya Somalia

Bunge jipya limeapishwa leo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, na kukaribisha kuanza serikali mpya, na kumalizika miaka minane ya kipindi cha mpito, ambacho kilipaswa kuhitimishwa leo Agosti 20. Bunge hilo ambalo ndilo la kwanza nchini humo katika kipindi cha miongo miwili, linakabiliwa na majukumu mawili muhimu mwanzoni: kwanza ni kumchagua Spika wa Bunge na [...]

20/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu awapongeza Waislamu kwenye Siku ya Eid Al-Fitr

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Huku Waislamu wakiadhimisha siku ya Eid al-Fitr Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amewatakia Waisalmu wote heri njema, mali na afya nzuri wanaposheherekea siku hii. Amesema kuwa sherehe hizo ambazo ni za kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan zinajiri wakati inapoendelea kumalizika kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa [...]

20/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban alaani matamshi ya raia wa Iran aliyetaka kufutwa kwa taifa la Israel

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekerwa na kushangazwa na matamshi yaliyotolewa na Iran iliyotaka kufutiliwa mbali kwa taifa la Israel.Ban pamoja na kulaani vikali matamshi hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya uchokozi tena yanayo palilia hali ya uhasama pia ametaka yapuuzwa.   Duru za vyombo vya habari zilimnukuu Rais wa Iran Mahmoud [...]

20/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waangalizi wa UM Syria wazitaka pande zote kuweka silaha chini

Kusikiliza / Jenerali Babacar Gaye

Wakati ujumbe wa waangalizi Umoja wa Mataifa nchini Syria ukijiandaa kuondoka nchini humo, bado umeendelea kusisitiza haja ya pande zinazozozana kuweka china silaha na kutojiingoza zaidi kwenye machafuko ambayo yanaripotiwa kushika kasi katika eneo la kati la mashariki  Mkuu wa ujembe huo Lieutenant General Babacar Gaye amewaambia waandishi wa habari mjini Damascus ya kwamba pande [...]

20/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Darfur atuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya ndege Sudan

Kusikiliza / Milimo ya Nuba, Kordofan Kusini

Mkuu wa mpango wa pamoja na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID ameelezea huzuni yake kufuatia ajali mbaya ya ndege ambayo imeuwa watu wengi akiwemo waziri wa serikali ya Sudan. Afisa huyo wa UNAMID anayekaimu Aichatou Mindaoudou amesema ajali ambayo imekatili ujumbe mzima ulioambatana na Waziri waserikali ya Sudan [...]

20/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa kijani utasaidia kutengeza ajira mpya Hispania:ILO

Kusikiliza / kazi za kijani, Hispania

Ripoti moja iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayohusika na maendeleo endelevu imesema kuwa Hispania inahitaji kuchukua mkondo sahihi wa kutekeleza mipango inayojali uchumi unaozingatia mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia wakati mgumu wa ongezeko la ukosefu wa ajira. Ripoti hiyo ambayo ni sehemu pia ya vidokezo vya shirika la kazi duniani ILO [...]

17/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Argentina yatekeleza kwa vitendo mpango wa MERCOSUR na kuwahalalisha wahamiaji zaidi ya milioni

Kusikiliza / bendera ya Argentina

Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na uhamiaji IOM limezindua chapisho lake linaloangaazia mpango unaojulikana MERCOSUR ambayo inalenga kuimarisha ustawi wa watu jamii ya wahamiaji. Katika chapisho hilo IOM imeeleza pia hatua zilizochukuliw a na serikali ya Argentina ambayo imeuhalalisha mpango huo na kuwafaidia jamii ya wahamiaji milioni kadhaa wanaoshi nchini humo. Katika kipindi cha [...]

17/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM Syria kuondoka mwishoni mwa juma

Kusikiliza / baraza la usalama

Wakati ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ukitaraji kusitisha shughuli zake nchini Syria, Baraza la Usalama lilikutana kujadilia hali ya mambo nchini humo limekubali kuanzisha ofisi itayohusika na usaidizi wa kisiasa ambayo pia itamulika masuala ya haki za binadamu. Umoja wa Mataifa umesema utaondoa ujumbe wake ifikapo jumapili usiku katika wakati hali ya mapigano bado [...]

17/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yachunguza sheria mpya iliyopitishwa na Australia kuhusu watafuta hifadhi

Kusikiliza / nembo ya UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linachunguza mapendekezo yaliyotolewa na taifa la Australa wiki hii kutoka kwa kundi moja la wataalamu na uamuzi ulitolewa na bunge ambapo watafuta hifadhi wataandikishwa kwenye kambi zilizo kwenye bahari ya Pacific. Hata hivyo matakwa ya UNHCR yamesalia kuwa mipango itakayoruhusu watafuta hifadhi wanaowasili kwa mashua nchini [...]

17/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kibinadamu yalenga kuwasaidia watu milioni 6 nchini Yemen

Kusikiliza / raia wa Yemen

Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yanalenga kuwahudumia watu milioni sita mwaka huu wa 2012 ikiwa ni ongezeko la asilimia 62 ikilinganishwa na miezi sita iliyopita. Kulingana na makadirio fedha zinazozohitajika kwa sasa ni jumla ya dola milioni 584. Katika eneo la Abya lililo kusini mwa nchi, shirika la kuratibu masusla ya kibinadamu OCHA limezindua [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani nchini Syria

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeazisha usambazaji wa misaada isiyokuwa chakula kupitia kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa watu waliohama makoa ambao kwa sasa wamepiga kambi kwenye shule nne mjini Damascus. Juma hili IOM ilisambaza vifaa 581 kwa usafi kwenye shule ya Fariz Daboos kwenye shule ya Somaya Al Makhzomiya pamoja na kwenye shule [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makundi yaliyojihami kaskazini mwa Mali yanaendelea kuwaajiri watoto:UNICEF

Kusikiliza / kuajiri kwa watoto

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema limepokea ripoti kuwa makundi yaliyojihami kaskazini mwa Mali yanaendelea kuwatumia watoto kwenye mapigano. Kuajiriwa na kutumiwa kwa watoto walio chini ya miaka 18 na makundi yaliyojihami ni kinyume na sheria ya kimataifa na nikitu kinachotajwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu iwapo [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yasema hospitali na vituo vya afya vimeharibiwa kwa viwango vikubwa nchini Syria

Kusikiliza / hospitali nchini Syria

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema wizara ya Afya nchini Syria inakadiria kuwa hospitali 38 na vituo vingine 149 vya afya vimeharibiwa kwa kiasi kikubwa, au hata kabisa, na hivyo kufanya utoaji wa huduma za afya kuwa mgumu. Mkurugenzi wa Kudhibiti Matukio ya Dharura na Hatari katika, WHO, Richards Brennman, amesema shirika hilo linahusika kwa [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wanaendelea kukimbilia nchi jirani kwa sababu ya ghasia Syria:UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria nchini Uturuki

  Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya raia wa Syria wanaokimbilia Uturuki, limesema Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Kati ya Jumanne na Jumatano, watu 3,500 walivuka mpaka na kuingia katika mikoa ya Kilis na Hatay, kwa mujibu wa maafisa wa serikali mikoani. Watu 1700 waloingia kwenye mkoa wa Kilis walitoka [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waadhimisha Siku ya Watoaji Huduma za Kibinadamu duniani

Kusikiliza / B2

Kila Agosti 19 ni Siku ya Watoaji wa Huduma za Kibinadamu, na leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, imefanyika hafla ya kuweka ua la heshima kwa kumbukumbu ya wahudumu wa Umoja wa Mataifa ambao waliuawa mjini Baghdad, pamoja na watoaji huduma za kibinadamu wote ambao wameuawa wakijaribu kwa ajili ya [...]

17/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya utoaji Huduma za Kibinadamu

Kusikiliza / siku ya utoaji huduma za Kibinadamu

Huku siku ya kimataifa ya utoaji wa huduma za kibinadamu ikisherehekewa tarehe 19 mwezi huu Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kutaka kufahamu maisha ya mtoaji huduma ni ya aina gani. Kunapotokea majanga kama vile mafuriko, mitetemeko ya ardhi au mikurupuko ya magonjwa watoa huduma za kibinadamu huonyesha ukakamavu mkubwa wanapoingia sehemu zilizoathirika na kuwahudumia [...]

17/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Kibinadamu:Beyonce

16/08/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatoa ushauri kwa wakimbizi kutoka Bhutan walio nchini Nepal

Kusikiliza / UNHCR, Nepal

Prem Bahadur mwenye umri wa miaka 25 ana matumani ya kupata makao mapya kwa kuwa anaelewa kuwa kuna huduma nzuri kwenye nchi zinazowachukua watu walio na matatizo ya kuona. Lakini hata hivyo babake mwenye umri wa miaka 60 ana hofu kuwa huenda mwanawe akakumbwa na matatizo ya kuishi kwenye nchi mpya kutokana na tatizo lake [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM azuru Guatemala kwa sababu ya uuzaji watoto na dhuluma za Kingono

Kusikiliza / child-abuse-prevention

Mtaalam wa wa haki za binadamu katika Umoja Mataifa, Najat Maalla M'jid ataizuru nchi ya Guatemala tokea tarehe 20 hadi 29 Agosti mwaka huu. Hii itakuwa ziara ya pili kufanywa na mtaalam huru, tangu ziara ya miwhso iliyoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, ili kuchunguza uuzaji wa watoto, [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa Wanachama wa IAEA wapitisha mpango wa usalama wa nyuklia licha ya kutofautiana

Kusikiliza / nemba ya IAEA

Hatua kubwa zimepigwa katika imarisha usalama wa nyuklia duniani tangu ajali ya Fukushima Daichi Japan limesema shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA. IAEA imefanya tathimini ya ripoti iliyotayarishwa kwa ajili ya mktano wa kila mwaka wa wanachama utakaofanyika mwezi ujao ambao ulipitisha mpango huo kwa pamoja mwezi Septemba mwaka jana licha ya kukukosolewa [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaendelea kudondosha kwa njia ya ndege msaada Sudan Kusini

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza awamu ya kwanza ya kudondosha kwa njia ya ndege msaada unaohitajika haraka wa chakula kwa watu zaidi ya 100,000 Sudan Kusini ambao wamekimbia mapigano. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WFP Ertharin Cousin Jumatano mchana tani 32 za ngano zilidondoshwa kwenye makazi ya wakimbizi ya eneo la [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia mkakati mpya wa elimu duniani akiwa Timor Leste

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon nchini Timor Leste

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuna mkakati mpya wenye lengo la kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa elimu kwenye ajenda ya ulimwengu mzima. Akiwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu wa Timor-Leste katika mji mkuu, Dili, Ban ametaja elimu kama kitu cha kipaumbele. (SAUTI YA BAN Ki-MOON) Mkakati wa "Elimu Kwanza" utatangazwa rasmi mwezi [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 2.5 wanahitaji msaada wa haraka Syria:Valerie Amos

Kusikiliza / Valerie Amos nchini Syria

Mratibu Mkuu wa Maswala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura katika Umoja wa Mataifa, Bi Valerie Amos, amesema amekuwa nchini Syria tangu Jumanne ili kujionea mwenyewe athari za mgogoro unaozidi kutokota , na kujadili njia za kuongeza utoaji wa misaada ya kibinadamu. Amesema ghasia zimeongezeka, na mara nyingi ukatili unakuwa ni wa kijumla. Amezitaka pande [...]

16/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya serikali na vya upinzani vimetenda uhalifu wa kivita nchini Syria: ripoti ya UM

Kusikiliza / 496268-Pinheiro

Vikosi vya serikali nchini Syria na vile vya upinzani vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Tume huru ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu wakati wa mzozo unaoendelea nchini humo. Ripoti hiyo ambayo iliidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasifu kuanza Majadiliano ya Kuzima Uhasama uliosababisha Machafuko Mynamar

Kusikiliza / Rakhine, Myanmar

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua mujarabu zilizochukuliwa na serikali ya Uturuki iliyoanzisha majadiliano na kurejesha hali ya utulivu katika jimbo la Rakhine lililoko kusin mwa Mynmar ambalo hivi karibuni lilikumbwa na machafuko yaliyosababisha watu kadhaa kukimbilia uhamishoni. Hivi karibuni ujumbe wizara ya mambo ya nje ya Uturuki pamoja na maafisa kutoka jumuiya ya kiislamu nchini [...]

15/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNDP ahimiza Kuwekeza zaidi katika Kupunguza Hatari za Majanga

Kusikiliza / Helen Clark

Mataifa ni lazima yawekeze katika kujiandaa na kuzuia majanga, na mataifa yanayotoa misaada na mashirika ya maendeleo hayana budi kuchangia hilo kama suala la kipaumbele katika kuzisaidia nchi maskini, ili maendeleo ya kibinadamu na ya kiuchumi yafanywe badala ya kupotezwa, amesema Bi Helen Clark, Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, ambaye sasa ni Mkuu [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yakaribisha uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu ya Australia

Kusikiliza / tobacco_graphic_large_who

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekaribisha kwa mikono yote uamuzi ulofanywa na Mahakama Kuu ya Australia wa kutupilia mbali kesi ilowasilishwa na sekta ya tumbaku, na kutoa wito kwa mataifa mengine duniani kuiga mtindo wa Australia unaoweka masharti makali kuhusu uuzaji wa bidhaa za tumbaku. Makampuni kadhaa makuu ya tumbaku yaliipeleka serikali ya Australia kortini, [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria mpya ya EU kuhusu Uchafu wa Vifaa vya Komputa yaanza kutekelezwa:UNEP

Kusikiliza / E-Waste

Jumuiya ya nchi za Ulaya imeweka kanuni mpya kuhusu mabaki ya vifaa vya elektroniki (yaani e-waste) ambazo zinatoa uwezo kwa nchi wanachama wa EU kukabiliana ipasavyo na uuzaji haramu wa mabaki kama hayo. Sheria hiyo mpya pia inatazamia kuboresha viwango vya kurejesha mabaki ya vifaa vya elektroniki, na imetokana na aina mbalimbali za utafiti, ukiwemo [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huu ndio wakati ya kumaliza ghasia nchini Syria:Ban

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema kuwa kilicho muhimu ni kuwa ni lazima vikosi vya serikali ya Syria na vile vya upinzani kusitisha ghasia. Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari hii leo nchini Timor-Leste Ban amesema kuwa ni lazima wote wasitishe ghasia na kuanzisha mazungumzmo ya kutafuta suluhu. Ban ameongeza kuwa [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM lashutumu mashambulizi kwa kikosi cha UNAMID

Kusikiliza / Baraza la Usalama

  Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameshutumu vikali mashambulizi yaliyoendeshwa kwa kituo cha polisi cha kikosi cha pamoja cha Mungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID kwenye mji wa Nyala ulio Darfur Kusini nchini Sudan ambapo mlinda amani mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa. Wanachama hao wametuma rambi rambi zao kwa [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwandiplomasia kutoka Nepal ateuliwa kuwa mjumbe maalum wa katibu mkuu kwenye masuala ya nchi masikini zaidi duniani

Kusikiliza / Gyan Chandra Acharya

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtua balozi wa Nepal kwenye Umoja wa Mataifa kama masaidizi wake kwenye masuala yanayohusu nchi maskini zaidi duniani. Gyan Chandra Acharya atahudumua kama mjumbe maalum kwa nchi maskini zaidi duniani na visiwa vidogo vinavyoendelea akichukua mahala pa Cheick Sidi Diarra kutoka Mali ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu [...]

15/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yakabiliana na Ebola nchini Uganda

Kusikiliza / ugonjwa wa Ebola nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO linashirikiana na wizara ya afya nchini Uganda na mashirika mengine kukabiliana na mkurupuko wa ugonjwa Ebola nchini humo. WHO inasema kuwa ilichukua hatua za mara moja kulipothibitishwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola mnamo tarehe 28 mwezi Julai mwaka huu. Msemaji wa WHO Fadela Chaib anasema kuwa visa 23 [...]

15/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM Kuondoa Operesheni yake ya Kulinda Amani Timor-Leste:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon nchini Timor-Leste

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hivi sasa Umoja wa Mataifa unajiandaa kuondoa operesheni yake ya kulinda amani nchini Timor-Leste. Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano mjini Dili Ban amesema anaamini mapendekezo yaliyotolewa na timu ya tathimini kwamba Timor-Leste haihitaji opereshenin ya kulinda amani hivi sasa. Ban amesema jeshi la polisi la [...]

15/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu waliotawanywa na Machafuko Syria wanahitaji haraka msaada:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos nchini Syria

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Valarie Amos ameelezea hofu yake baada ya kukutana na watu waliotawanywa na machafuko wilaya ya Zaheria Damascus katika mwanzo wa ziara yake ya siku tatu Syria na Lebano. Bi Amos amesema watu aliokutana nao waemwambia wanahitaji maji safi, vifaa vya usafi, madawa [...]

15/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kamati kuhusu Silaha yajadili aina mpya za Silaha za Maangamizi ya Halaiki

Kusikiliza / silaha

Kamati ya kimataifa inayohusika na kuondoa au kupinga matumizi na silaha za nyuklia, imejadili aina mpya za silaha za maangamizi ya halaiki pamoja na mifumo mipya ya silaha kama hizo, zikiwemo silaha za miyale ya Uranium. Kamati hiyo pia inajadili mpango wa kina kuhusu uondoaji wa silaha kama hizo, na uazi kuhusu mataifa kujihami kwa [...]

14/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM kwenye michezo ya Olympics "Michezo ya mwaka huu ilivuka viwango"

Kusikiliza / Wilfried Lemke

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa London kwenye michuano ya Olimpiki umesifu mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye michezo ya mwaka huu hatua ambayo wameeleza kuwa inafungua njia ya kupatikana mafanikio zaidi kwenye maeneo yanayohusu ustawi wa kijamii ikiwemo ujenzi wa amani na kupunguza matabaka ya kijinsia. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ujumbe huo umewapongeza [...]

14/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakfu Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, UNRWA wakusanya nguvu kuwalisha Wapalestina 28,000

Kusikiliza / UNRWA

Wakfu wa Khalifa Bin Zayed Al Nahyan ukishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakipimbizi wa Kipalestina UNRWA umefaulu kuanzisha mpango unaoitwa " walishe wafungao" kwa ajili ya kuwakirimu wananchi wa Ukingo wa Gaza walioko kwenye kipindi cha mwezi wa Ramadhani. Chini ya mpango huo kiasi cha watu zaidi 28,000 wanatazamia kufaidika wakipatia [...]

14/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yafanya uandikishaji wa wakimbizi kutoka Syria huku watu zaidi wakiendelea kuihama nchi hiyo

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Huku watu zaidi wakiendelea kuikimbia Syria kila siku shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafanya jitihada za kuwaaandiskisha wakimbizi kutoka nchi hiyo. Uandikishaji wa wakimbizi ni muhimu kwa sababu unaawasaidia wakimbizi kupata huduma muhimu. Kituo kipya kwa sasa kimefunguliwa kaskazini mwa Lebabon kitakachosaidia kuwaandikisha karibu watu 700 kwa siku . Kwa sasa [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia Waathiriwa wa Usafirishaji Haramu wa watu kutoka Kenya kurudi makwao kutoka Sudan Sudan kusini

Kusikiliza / usafirishaji haramu wa watu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa wamewasaidia waathiriwa wawili wa usafirishaji haramu wa watu kutoka Kenya kurejea makwao kutoka Sudan kusini. Inaripotiwa kuwa waathiriwa hao ambao ni vijana walitolewa kwenye jamii moja kijijini kwa kazi za nyumbani lakini baadala yake walilazimishwa na kuingizwa kwenye [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aelezea wasiwasi wake Kuhusu Kucheleweshwa Uchaguzi wa Bunge jipya Somalia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya chelewa chelewa inayozingira kuundwa kwa bunge jipya nchini Somalia, pamoja na matukio ya vitisho na ghasia ya hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa yake, Bwana Ban amesema matukio hayo na ghasia havitakiwi kuruhusiwa kuendelea au kuhatarisha kukamilishwa kwa kipindi cha mpito [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA yuko nchini Syria Kuchagiza Jitihada za Kuwafikishia Waathirika Misaada

Kusikiliza / Valerie Amos nchini Syria

Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Bi Valerie Amos, amewasili nchini Syria kwenye ziara ya siku tatu, ili kukagua hali ilivyo na jinsi ya kuwasaidia watu walioathiriwa na machafuko. Mjini Damascus, Bi Amos amepanga kufanya mazungumzo na maafisa wa serikali na wadau katika utoaji wa huduma za kibinadamu, pamoja na familia [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea katika Masuala ya Kibinadamu yapitisha Lengo la Kufikia watu milioni 100

Kusikiliza / Beyonce ashiriki katika kampeni ya siku ya kimataifa ya kujitolea katika masuala ya kibinadamu

Kampeni ya kimataifa lenye lengo la kuweka historia ya mitandao ya kijamii kwa kujaribu kuwafikia watu bilioni moja hapo Agosti 19 katika kusherehekea siku ya kimataifa ya masuala ya kibinadamu, imepita lengo lake la kwanza la kufikia watu milioni 100. Kampeni hiyo imepata msukumo mkubwa kufuatia tamasha la muziki lililofanyika Ijumaa kwenye baraza Kuu la [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Thathimini ya IOM,UNHCR na WFP yaonyesha haja ya Msaada kwenye mpaka wa Kenya na Ethiopia

Kusikiliza / msaada kutoka kwa mashirika

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaomba msaada wa fedha ili kukabiliana na mahitaji ya haraka ya kibinadamu kwa watu 8000 wa Kiethiopia waliotawanywa na machafuko na jamii zinazowahifadhi kwenye maeneo ya Somare, wilaya ya Moyale upande wa Kenya kwenye mpaka na Ethiopia. Tathimini ya pamoja iliyoongozwa na IOM, shirika la wakimbizi UNHCR na shirika [...]

14/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNAMID auwawa Kusini mwa Darfur

Walinda Amani wa UM Darfur

Askari wa kulinda amani anayefanya kazi chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID katika jimbo lenye mzozo la Darfur nchini Sudan ameuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Kwa mujibu wa duru za habari, kundi la watu wenye silaha walivamia kambi moja ijulikanayo Nyala iliyoko Kusin mwa Darfur na kuanzisha mashambulizi yaliyosababisha [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahiga ashutumu vikali mauaji ya afisa wa serikali na mwandishi wa habari nchini Somalia

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mjumbe maaalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ameshutumu vikali mauaji ya Yusuf Ali Osman ambaye ni afisa wa serikali nchini Somalia na yale ya mwandishi wa habari. Ali au kwa jina lingine Buniste yaliyotokea mjini Mogadishu. Yusuf mwandishi wa habari wa zamani alikuwa mfanyikazi kwenye wizara ya habari [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban Ahusunishwa na Kuangamia kwa watu Kutokana na Tetemeko la Ardhi nchini Iran

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban

  Katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea kaskazini magharibi mwa Iran mwishoni mwa wiki. Kupitia kwa msemaji wake Ban ametoa rambi rambi zake kwa serikali ya Iran, watu wake na hasa kwa familia za wale [...]

13/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Valerie Amos kuzuru Syria na Lebanon

Kusikiliza / Bi Valerie Amos

  Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, anatarajiwa kusafiri kwenda Syria na Lebanon kuanzia tarehe 14 hadi 16 Agosti. Ziara hiyo ya siku tatu inalenga kuuchagiza ulimwengu kuangazia hali ya kibinadamu inayozidi kuzorota nchini Syria, na athari za mgogoro ama kwa walosalia nchini Syria, au walokimbilia nchi zingine, ikiwemo [...]

13/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP azuru Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / Bi Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, ameanza ziara ya siku tatu katika mataifa ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini. Cousin ameanza ziara yake kwa kukutana na mafisa wakuu wa serikali mjini Khartoum, wawakilishi wa mashirika ya kutoa misaada na wafanyakazi wa WFP. Sudan ni mojawapo wa maeneo ambako [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Azindua Mkakati mpya wa Kulinda Bahari

Kusikiliza / Bahari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amezindua mkakati mpya wa kulinda bahari na watu ambao riziki zao zinategemea bahari, na kutoa mwito kwa mataifa kufanya kazi pamoja ili kufikia udhibiti endelevu wa mali ghafi hiyo azizi, na kukabiliana na hatari zinazoikabili. Kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 30 tangu kufunguliwa mkataba wa Umoja wa [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasaidia juhudi za Ufilipino kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

Kusikiliza / Mafuriko Ufilipino

Kufuatia mvua nzito iliosababisha mafuriko katika majimbo ya Luzon ya Kati na Manila Mjini, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limeandaa misaada ya chakula ili kuisaidia serikali ya Ufilipino katika juhudi zake za kuwasaidia watu waloathiriwa na mafuriko, likisaidiana na idara ya Maslahi ya Kijamii na Maendeleo katika majimbo ya Luzon Kati, [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Palestina nchini Syria wasafirishiwa msaada toka nyumbani

Kusikiliza / Mkimbizi wa Kipalestina na mtoto Syria

Msafara wa msaada wa chakula na dawa ambao umeandaliwa na mamlaka ya Palestina kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, uliwasili mjini Damascus tarehe 8 Agosti. Msafara huo wa malori 17 ulichukua tani 360 za unga, mchele, sukari, ngano na madawa yenye thamani ya dola 650,000. Msaada huo umetolewa na mashirika ya Kipalestina, wafanyabiashara na watu binafsi wakati [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Yazidi Kuongezeka Syria:Gaye

Kusikiliza / Jenerali Babacar Gaye

  Ni dhahiri kwamba ghasia zinaongezeka katika maeneo mengi ya Syria amesema mkuu wa mpango wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIS Jenerali Babacar Gaye alipozungumza na waandishi wa habari Jumatatu mjini Damascus. Gaye amesema matumizi ya silaha nzitonzito yanayofanywa na serikali na mashambulizi ya kulenga yanayofanywa na upinzani katika maeneo mbalimbali mijini [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujuma wanajitahidi kwa kila njia kuwekeza kwa wanawake ili wafikie malengo ya kuchagiza maendeleo na kuipeleka dunia katika mstakhbali bora. Ban ameyasema hayo mjini Seuol Korea Jumatatu kwenye kongamano la kwanza la kimataifa la shirikiano wa wasichana. Ban amesema [...]

13/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana kwenye mstari wa mbele wa kutaka watambuliwe kama watu wenye manufaa kwenye jamii

Kusikiliza / kundi la vijana lijulikano kama YALDA

Huku mamilioni ya vijana wakiwa hawana ajira kote duniani baadhi yao wameamua kwamba ni vyema wajitokeze, wajionyesha na kujitambusha kwenye sekta mbali mbali duniani angalau kutambuliwa kama walio wenye manufaa makubwa kwa jamii. Baada ya kutambua kuwa hawashirikishwi vilivyo kwenye masuala yanayowahusu baadhi yao wamebuni mashirika yanayowaleta pamoja hasa wanafunzi wanaosomea taaluma mbali mbali na [...]

10/08/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Watu wa asili watoa maoni yao kuhusu Siku ya Kimataifa ya Watu wa asili

Kusikiliza / Wamaasai

Siku ya watu wa asili huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Agosti. Jason Nyakundi wa Redio wa Umoja wa Mataifa amezungumza na watu wa asili mjini Nairobi na kuwauliza watoe maoni yao kuhusu siku hii. Wasikilize.

10/08/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM yatoa mafunzo kwa Maafisa wa Uhamiaji wa Namibia

Kusikiliza / iom logo

Maafisa wa uhamiaji nchini Namibia wamehitimu mafunzo yaliyoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambayo imeendesha mafunzo hayo ya wiki mbili kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi maafisa uhamiaji. Maafisa hao nane wamepatiwa mbinu mpya za uongozi na namna ya kukabiliana na mienendo ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu. Pia [...]

10/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Angola yaadhimisha mwaka mmoja bila Ugonjwa wa Polio

Kusikiliza / mtoto Angola

Angola leo imeadhimisha mwaka mmoja wa kutokuwa na tukio lolote la ugonjwa wa polia na hivyo kuongeza msukumo kwenye jihada za kimataifa za kukabiliana na ugonjwa huo duniani kote. Kiwango cha ugonjwa huo katika mwaka 2010 kilipungua na kufikia wagonjwa 33 na hali ya kuimarika zaidi ilishuhudiwa mwaka uliofuata 2011 kukiwa na wagonjwa wa tatu [...]

10/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaendelea Kukabiliana na Hali ya Dharura ya Wakimbizi Sudan Kusini

Kusikiliza / wakimbizi wa Sudan

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema hali ya dharura ya wakimbizi katika Sudan ya Kusini imeongezeka hasa katika majuma ya hivi karibuni. Shirika la UNICEF sasa linaangazia kuwalisha watoto ambao wana tatizo la utapia mlo ulokithiri. Idadi ya watoto ambao hawana wazazi au walezi imeongezeka katika kipindi hicho, na kufikia watoto [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yazingatia mienendo inayoweza kusaidia kubadili hali ya ajira kwa vijana

Kusikiliza / siku ya vijana duniani

Shirika la Ajira Duniani, ILO, limesema kuendeleza ajira kwa vijana limekuwa suala la kipaumbele kwa serikali nyingi, wakati vijana milioni 75 kote ulimwenguni hawana ajira. Hata hivyo, shirika la ILO limeonya kuhusu kizazi cha vijana chenye vidonda vinanyotokana na ukosefu wa ajira, kukaa tu bila cha kufanya, ajira zenye hatari pamoja na umaskini ulokolea katika [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kufanya kazi na vijana na kwa ajili yao ni mojawepo ya mambo muhumu zaidi kwangu:Ban

Kusikiliza / vijana washikana pamoja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa kizazi cha sasa cha vijana, ambacho ni chenye idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni, wengi wao wakipatikana katika nchi zinazoendelea, kina uwezo mkubwa zaidi wa kuendeleza jamii nzima ya binadamu. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya vijana, ambayo huadhimishwa [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi Majirani wa Syria Waendelea Kuwapokea Wakimbizi zaidi

Kusikiliza / wakimbizi wa syria walioko Uturuki

Ofisi za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Lebanon, Uturuki , Jordan na Iraq zinaripoti kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi kutoka Syria juma hili. Kulingana na takwimu za UNHCR ambazo huonyesha wakimbizi waliojiandikisha na wale walio kwenye shughuli ya kujiandikisha zinaonyesha jumla ya wakimbizi 146,667 hadi Agosti tisa. Nchini Uturuki idadi ya [...]

10/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashua zawasafirisha watu 2500 kutoka mjini Renk nchini Sudan Kusini kwenda makwao

Kusikiliza / mfanyakazi wa IOM awasidia watoto Sudan

Huku mashua zikiwa tayari zimeondoka mji wa Renk kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zikiwasafirisha zaidi ya raia 2500 wa Sudan Kusini waliokwama kwenye mji huo kwa miezi kadha hatma ya watu wengine 16,000 haijulikani baada ya kuwepo uwezekano wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kusitisha oparesheni zake kutokana na ukosefu wa [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM lapongeza Mpango wa Amani nchini Somalia

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha hatua zilizopigwa katika kukamilisha majukumu kwenye barabara ya amani ya kumaliza kipindi cha mpito nchini Somalia. Wanachama hao pia wamekaribisha bunge kupitishwa kwa katiba mpya na bunge wakiongeza kuwa kupitishwa kwa katiba hiyo ni hatua muhimu ya mabadiliko nchini Somalia kuelekea kwenye uongozi ulio dhabiti. [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kinu cha Nyuklia karibu na Fukushima hakijaathirika:IAEA

Kusikiliza / IAEA

Timu ya watalamu wa kimataifa wa shirika la nguvu za atomi IAEA leo wamewasilisha ripoti yao ya awali baada ya ziar ya wiki mbili kukusanya taarifa kuhusu athari za tetemeko kubwa lililoikumba Japan mwaka jana kwenye mtambo wa nyuklia wa Onagawa . Ripoti yao inasema mtambo huo kwa bahati haukuathirika.Matokeo ya utafiti wao yatajumuishwa kwenye [...]

10/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Changamoto za jamii za Watu wa Asili kutoka Bujumbura nchini Burundi

Kusikiliza / watu wa asili Bujumbura, Burundi

Kongamano la watu asili kutoka Bara la Afrika limefanyika nchini Burundi wakati UM ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wa asili ambayo inafanyika kila mwaka Agosti 9. Komgamano hilo limeangazia jinsi watu wa Jamii hiyo wanaweza kunufaika na ujuzi wao kupitia haki miliki pamoja na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo [...]

10/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Amos atoa wito wa Misaada kwa wakimbizi wa DRC walio nchini Rwanda

Kusikiliza / wakimbizi nchini Rwanda

Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameitembelea kambi ya Kigeme iliyo kusini mwa Rwanda ambapo zaidi wakimbizi 11,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamepewa hifadhi. Zaidi ya watu 20,000 wamevuka mpaka wakikimbia ghasia kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC. Kwa sasa serikali ya Rwanda na shirika la kuhudumia [...]

10/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kibinadamu yaomba dola milioni 32.5 kufadhili mahitaji yanayongezeka Myanmar

Kusikiliza / John Ging

Akikamilisha ziara yake ya siku nne Myanmar, Mkurugenzi wa shughuli za Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadam, John Ging ameelezea hofu yake kuhusu hatma ya zaidi ya nusu milioni ya wakimbizi wa ndani, na kutoa wito ziheshimiwe kanuni na sheria za kimataifa za kibinadamu ili kuyawezesha mashirika ya kutoa misaada kuyafikia maeneo yaloathiriwa na mzozo [...]

09/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM watoa dola milioni 158 kwa mahitaji ya kibinadamu ambayo hayajafadhiliwa vyema mwaka 2012

Kusikiliza / Valerie Amos

Mkuu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ametenga dola milioni 55 kutoka kwenye mfuko wa Mfuko wa Ufadhili wa Maswala ya Dharura (CERF), ili kuimarisha operesheni za kibinadamu katika nchi nane zenye mahitaji ya kibinadam yaliyopuuzwa. Fedha zilizotengewa mataifa ya Afghanistan, Cameroon, Colombia, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC), Ethiopia, Madagascar, [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Athari za radio na mabadiliko ya hali ya hewa kwa jamii za kiasili nchini Peru

mtu wa asili, Peru

Jamii za kiasili kwenye milima ya kusini mwa Andean nchini Peru wanaripotiwa kuathiriwa pakubwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Jamii hizi zinakabiliwa na hali mbaya ya umaskini suala linalochangiwa na mavuno duni. Jamii hizi zinazoishi mbali milimani hazina uwezo wa kupata hamasisho kutoka mijini kuhusu njia za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali [...]

09/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wakatibisha Muafaka wa pande tatu nchini Sudan

Kusikiliza / Mark Cutts

  Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Mark Cutts amekaribisha utiaji saini wa maelewano baina ya serikali ya Sudan, kundi la SPLM-North pamoja na Muungano wa Afrika, Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kuhusu msaada wa kibinadamu katika majimbo yaliyoathirika na vita ya Kordofan Kusini na Blue [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wimbi la wakimbizi wa ndani Syria ni kutokana na kutoheshimu sheria za Kimataifa:UM

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Kupuuza haki za binadamu za kimataifa na sheria za kimataifa kumechangia kuwepo kiasi kikubwa sana cha wakimbizi wa ndani nchini Syria, wakati mgogoro unapozidi kutokota, amesema mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wakimbizi wa ndani, Chaloka Beyani. Bwana Beyani ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya takriban watu milioni 1.5, ambao wamelazimika kuhama [...]

09/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wawatahadharisha waasi wa M23 wa DRC

Kusikiliza / waasi wa M23 nchini DRC

Msemaji wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO Manodj Monoubay ametoa tangazo la kuwatahadharisha waasi wa M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yanayotishia salama Mashariki mwa nchi hiyo kusitisha mara moja zoezi la kuwaingiza watoto jeshini. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kishasa Jumatano Monoubary amesema ikiwa waasi [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasisitiza Umuhimu wa Diplomasia ya Kuzuia Migogoro

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea umuhimu wa diplomasia ya kutambua mapema na kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani kama njia ya kuzuia migogoro zaidi. Wanachama wa Baraza hilo wameelezea umuhimu wa kisiasa, kibinadamu na kimaadili, pamoja na faida za kiuchumi za kuzuia kutokea, kuongezeka au kurejelea migogoro. Katika taarifa ilotolewa kwa waandishi [...]

09/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bei ya Bidhaa za Chakula Yapanda kwa asilimia 6:FAO

Kusikiliza / mazao

Bei ya bidhaa za chakula ilipanda kwa kiasi cha asilimia 6 mwezi Julai, baada ya miezi mitatu ya kushuka bei hiyo, limesema Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO. Kipimo wastani cha viwango vya bei za bidhaa za chakula cha FAO, hupima mabadiliko ya kila mwezi katika bei za kapu la bidhaa za chakula. Kwa [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada Imara wa Kibinadamu wahitajika DRC:Amos

Kusikiliza / wakimbizi nchini DRC

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya dharura na misaada ya kibinadamu Valarie Amos amehitimisha ziara yake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi baada ya kuzuru eneo la Kanyaruchinya nje kidogo ya mji wa Goma siku ya Jumatano. Katika eneo hilo watu 30,000 wamepatiwa makao na amesema inasikitisha kuona watu hususani [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyombo vya Habari vya Kijamii vinatoa fursa kwa jamii ya Watu wa Asili:ILO

Kusikiliza / vyombo vya habari vya kijamii

Katika muktadha huo wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wa kiasili leo, Shirika la Kimataifa la kazi duniani, ILO, limesema vyombo vya habari vya kijamii vinachangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza haki za watu wa kiasili. Shirika la ILO limesema hili linatokana na kwamba, takriban nusu ya idadi ya watu wa kiasili kote ulimwenguni wanaishi [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wa Asili ni Muhimu Kushirikishwa katika vyombo vya Habari:UM

Kusikiliza / maasai

Imeelezwa kwamba huu ni wakati pekee ambao watu wa kiasili hupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari, ni pale wanapouawa. Hii ni dhana ya kusikitisha na ni mojawepo tu ya mifano ya malalamishi yaliyofikishwa kwa Mkuu wa Sekritariati ya Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa kiasili, Chandra Roy-Henriksen. Siku ya kimataifa ya [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awapongeza Watu wa Asili kwa kutumia Vyombo vya Habari vya Asili na vya Kisasa

Kusikiliza / watu wa asili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa asili kwa kujitokeza kutumia vyombo vya habari vya asili na vya kisasa katika kuchagiza masuala mbalimbali yanayowahusu. Katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya watu wa asili Alhamisi Ban amesema kuanzia magazeti, tovuti hadi mitandao ya kijamii watu wa asili wanatoa changamoto [...]

09/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyombo vinatoa mchango ya Kulinda Haki za Jamii za Kiasili

Kusikiliza / James Anaya

Mjumbe maaalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za jamii za kiasili James Anaya ameutaja mchango unaoweza kutolewa na vyombo vya habari katika kulinda haki za watu wa kiasili. Anaya amesema kuwa haki ya jamii za kiasili kuwa na vyombo vyao vya habari kwa lugha zao ni kutekelezwa kwa makubaliano ya haki za watu hao. [...]

08/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Palestina yapendekeza kuboreshwe mashirikiano ya kitaalumu baina yake ya UNCTAD

Kusikiliza / nemba ya UNCTAD

Mawaziri wa Kipalestina pamoja na maafisa wenginewa ngazi za juu wamesifu na kupongeza juhudi zinaazoendelea kuchukuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa UNCTAD linalochukua shabaha ya kusukuma mbele shughuli za kimaendeleo hasa katika eneo ka ukusaji uchumi. Hivi karibuni ujumbe wa UNCTAD ilifanya ziara ya siku tano nchini humo ukilenga kuimarisha mashirikiano ya kiutendaji lakini [...]

08/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Afghanistan wazidi kuwaathiri vibaya raia licha ya kupungua idadi ya mahasiri 2012:UM

Kusikiliza / watoto nchini Afghanistan

Katika miezi sita ya kwanza mwaka 2012, ghasia zinazotokana na migogoro nchini Afghanistan ziliendelea kuyagharimu maisha ya raia, imesema ripoti ya kipindi cha kwanza cha mwaka, ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Afghanistan, UNAMA, inayohusu kuwalinda raia katika migogoro ya silaha. Kati ya tarehe 1 Januari na Juni 30, 2012, idadi ya raia walioathirika ilizidi [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi zahitajika katika kuzuia Unyanyasaji wa watoto Mashariki mwa Asia na Pacific:UNICEF

Kusikiliza / watoto wa Asia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa ripoti leo Jumatato inayosema unyanyasaji wa kimwili usiokubalika unasababisha madhara ya muda mrefu kwa maisha na hatima ya watoto wengi Mashariki mwa Asia na Pacific. Ripoti hii iitwayo "Unyanyasaji wa watoto: Ushamiri, Matukio na Athari katika Mashariki mwa Asia na Pacific" ni ya kwanza ya [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lishe ni lazima ziwe endelevu:FAO na Bioannuai

Kusikiliza / FAO

Hatua zinahitajika kuchukuliwa mara moja ili kuwa na lishe endelevu na mazingira ya uzalishaji chakula, ili kuboresha afya ya wanadamu na ulimwengu wanamoishi, limesema Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO na shirika la Biodiversity International katika kitabu kipya. Licha ya ufanisi mwingi uliofikiwa katika sekta ya kilimo katika miongo mitatu iliyopita, [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaongeza kasi ya kuwasaidia wakimbizi wa DRC kurejea nyumbani kutoka nchi jirani ya Congo

Kusikiliza / wakimbizi wa Congo

Zaidi ya wakimbizi 11,000 wa Kongo wamerejea nyumbani kwao mwaka huu, kupitia mpango wa kurejeshwa kwa hiari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Operesheni hiyo iliyoanza tarehe 5 Mei, inatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu. Inatarajiwa kuwawezesha raia wa Kongo 49, 000 waliotoroka mapigano ya kikabila katika jimbo la Equateur katika [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Mali ni wenye Kukanganya na Maumbo tofauti:Ban

Kusikiliza / kijana nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa mzozo uliopo nchini Mali ni wenye kukanganya kimawazo na una maumbo tofauti. Katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bwana Ban amesema kuwa tangu ulipoanza mzozo wa Mali, hali imekuwa ikibadilika na kufikia viwango vya kutisha kila uchao, kila wiki. Amesema [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa ataka Waandishi kupewa Usalama nchini Honduras

Kusikiliza / waandishi habari

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kutoa maoni na kujieleza Frank La Rue ameanza ziara rasmi nchini Honduras ziara ambayo itakamilika tarehe 14 mwezi huu kwa mwaliko wa serikali. Mjumbe huyo atajaribu kubaini jinsi taifa la Honduras limejiandaa kutekeleza haki ya kujieleza na hatua zilizochukuliwa kuifanikisha na pia changamoto inazokumbana nazo. Wakati [...]

08/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hata baada ya kuwepo changamoto huduma za kibinadamu zinaendelea nchini Sudan

Kusikiliza / wakimbizi wa Sudan

Kurejea kwa utulivu kwenye sehemu nyingi za jimbo la Darfur nchini Sudan kumechangia watu kurejea makwao kuanzia mwezi Januari mwaka 2011. Watoa huduma za kibinadamu kwa sasa wanajitahidi kuhakikisha kuwepo kwa huduma muhimu kwenye maeneo wanakorejea watu hao. Tarehe tano mwezi Agosti serikali ya Sudan na kundi la SPLM-NORTH walisaini makubaliano na Muungano wa Afrika [...]

08/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza Ubaguzi wa Rangi yahitimisha Tathmini ya ripoti ya Ecuador

Kusikiliza / ubaguzi wa rangi

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na utokomezaji wa ubaguzi wa rangi Jumatano imehitimisha tathimini ya ripoti ya Ecuador kuhusu utekelezaji wa mkataba wa kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi wa rangi katika taifa hilo. Waziri wa utamaduni wa Ecuador Maria Fernanda Espinosa akiwasilisha ripoti hiyo kwenye baraza la haki za binadamu amesema ni kwa njia [...]

08/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Benomar akaribisha hatua ya Kufanyia Ukarabati Sekta ya Ulinzi Yemen

Kusikiliza / Jamal Benomar

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen amekaribisha hatua iliyopitishwa na Rais wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi tarehe 6 Agosti mwaka huu inayohusu kuipanga upya sektan ya ulinzi ya nchi hiyo. Amesema kupitishwa kwa hatua jizi kunakuwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa maafikiano ya kipindi cha mpito ya November [...]

08/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM na UNFPA zachagiza ufahamu kuhusu ulanguzi wa binadamu Indonesia

nemba ya IOM

Shirika la Kimataifa ya Uhamiaji, IOM, likishirikiana na serikali ya Indonesia na hazina ya Umoja wa Mataifa UNFPA, limezindua kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu hatari za usafirishaji haramu wa binadamu miongoni mwa watoto 3, 000 kati ya miaka 12-18 magharibi mwa Java, nchini Indonesia. Mchakato huo ambao unafadhiliwa na idara ya kuzuia usafirishaji haramu wa [...]

07/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Serikali ya mpito Somalia yasaini mkakati wa kukomesha mauaji ya watoto

Kusikiliza / ramani ya Somalia

Serikali ya mpito nchini Somalia imetia saini mkakati wa kuchukuwa hatua za kukomesha mauaji na ulemazaji wa watoto katika vita vya silaha. Mkakati huo ulotiwa saini pia na Umoja wa Mataifa, unalitwika jeshi la kitaifa la Somalia na makundi ya muungano yaliyoko chini ya usimamizi wake wajibu wa kukomesha mauaji na ulemazaji kama huo. Mkakati [...]

07/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na hali ya usalama DRC

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hasa kutokana na ghasia zinazochochewa na kundi la M23 na makundi mengine yenye silaha, yakiwemo ya kitaifa na ya kimataifa. Bwana Ban amesema haya katika ujumbe wake kwa kongamano la kimataifa kuhusu eneo [...]

07/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya hewa Arctic haieleweki

Kusikiliza / hali ya hewa

Ripoti za wataalamu wa hali ya hewa zinasema kuwa eneo la Artic linaendelea kushuhudia mabadiliko ya mara kwa mara na sasa kiwango cha hali joto kimepanda kwa zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia. Katika ripoti mpya iliyozinduliwa ikiwalenga watu wa eneo hilo, inaonyesha kuwa pamoja na tukio hilo kuwa ni la [...]

07/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulizi la kigaidi kwenye mpaka wa Misri eneo la Sinai Peninsula

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulizi la kigaidi lilitekelezwa katika mpaka wa Sinai Peninsula na kuuwawa askari 16 wa Misri. Tukio hilo la mwishoni mwa juma pia limesababisha watu kadhaa kujeruhiwa . Katika taarifa yake kufuatia shambulizi hilo, Ban amesema kuwa ni matumaini yake kuona wale waliohusika na ugaidi huo [...]

07/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uingereza yaipiga jeki IOM kufanikisha makazi ya waathirika wa mafuriko Pakistan

Kusikiliza / waathiriwa wa mafuriko Pakistan

  Serikali ya Uingereza imetenga kiasi cha paunti milioni 5 ili kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambalo linaendesha shughuli za kuwapatia hifadhi pamoja na chakula kwa mamia wa raia wa Pakistani walioathiriwa na mafuriko msimu uliopita. Pamoja na mambo mengine kiasi hicho cha fedha kinatazamiwa kuwafaidia zaidi ya familia [...]

07/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaeleza ongezeko la mahitaji ya kibinadamu Syria

Kusikiliza / msaada nchini Syria

Shirika la afya dunianin WHO linasema linahofia hali ya afya ya raia nchini Syria. Sekta ya afya ya nchi hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawaa na vifaa vya tiba. Syria imekuwa ikizalisha asilimia 90 ya tembe na madawa mengine lakini hivi sasa uzalishaji huo unatatizwa na masuala ya usalama, upungufu wa mali ghafi, vikwazo [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaitaka Bangladesh kuondoa marufuku kwa mashirika yasiyokuwa ya serikali

Kusikiliza / wakimbizi wa Myanmar

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa wito kwa serikali ya Bangladesh kuhakikisha kuwa misaada kutoka kwa mashirika yasiyokuwa ya seriali imeendea kutolewa kwa watu ambao hawajasajiliwa kutoka jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Juma lililopita mashirika yasiyokuwa ya serikali yakiwemo la Medecins Sans Frontières, Action Contre La Faim and Muslim Aid UK [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuwafikia watu zaidi na msaada wa chakula nchini Myanmar

Kusikiliza / msaada Myanmar

Shirika la mpango wa Chakula (WFP) kuwa litaendelea kutoa msaada kwa raia wa Myanmar ambao wamelazimika kuhama makwao na wale walopoteza makazi na riziki zao hadi mwezi Septemba, au hata Disemba mwaka huu. Tangu mwanzoni mwa mzozo wa Rakhine mwezi Juni, shirika la WFP limewafikia watu waloathirika na zaidi ya tani 2,000 za chakula. Zaidi [...]

07/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kamati ya UM wajadili utokomezaji wa silaha za kinyuklia

Kusikiliza / silaha za kinyuklia

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusu kukomesha matumizi ya silaha za nyuklia, inaendelea na mazungumzo kuhusu njia mwafaka za kuhakikishia mataifa yasiyo na silaha za nyuklia kuhusu matumizi au tishio la kushambuliwa na silaha kama hizo. Mwakilishi wa Japan kwenye kamati hiyo ameelezea hamu ya taifa la Japan kuona ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia, [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukaji mbaya wa haki za binadamu waripotiwa kuendelea nchini DRC

Kusikiliza / ukiukaji wa haki za binadamu, DRC

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa ukiukaji mbaya wa haki za binadamu umeripotiwa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ukiwemo mauaji ya kijiji kizima na makundi yaliyojihami, ubakaji, utekaji nyara na kuwaingiza watoto kwenye jeshi. Kote nchini DRC karibu watoto milioni moja wameathiriwa na hali mbaya ya utapiamlo huku taiafa [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali eneo la Sahel yachochewa na Ugonjwa wa Kipindupindu

Kusikiliza / ugojwa wa Kipindupindu katika eneo la Sahel

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa ugonjwa kwa kipindupindu kwa sasa umeripotiwa kwenye eneo la sahel eneo ambalo watoto tayari wamedhoofishwa na ukosefu wa lishe na utapiamlo. Nchini Niger hali inaendelea kuchochewa na mavuno haba baada ya mimea kukumbwa na magonjwa. Mwishoni mwa mwezi July watoto 161,000 walio chini ya [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yatiwa hofu na Machafuko Darfur Kaskazini

Kusikiliza / kikosi cha UNAMID

Vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika vya kulinda amani Darfur UNAMID vimesema vinatiwa hofu na machafuko na mashambulizi dhidi ya raia katika mji wa Kutum na viunga vyake katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan Kwa mujibu wa mkuu wa vikosi hivyo Ibrahim Gambari mauaji na uharibifu sio jibu na [...]

07/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito wa kuwashirikisha wanawake na wasichana kwenye matumizi ya programu za bure watolewa

Kusikiliza / FOSS

Kitengo cha usawa wa kijinsia cha shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa sasa kiko mbioni kutafuta makundi yaliyo na progamu yanayochangia kuinua majukumu ya wanawake na uwakilishi wao kwenye progamu isiyo ya malipo ya FOSS. Hata kama FOSS imebadili njia za kutayarishwa kwa programu , kusambazwa na kutumika matatizo [...]

06/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahiga akaribisha tamko la kumaliza serikali ya mpito Somalia

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga amekaribisha tamko lililotolewa leo na watiaji saini mpango wa kumaliza serikali ya mpito, wakati wa kukamilisha mkutano uliokuwa ukijadili masuala yaliyosalia na kuhakikisha kwamba majukumu yote yanakamilishwa ili kumaliza kipindi cha mpito katika wiki mbili zijazo. Ajenda sita zimejadiliwa katika mkutano huo zikiwemo kuunda [...]

06/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Muafaka wa suala la mafuta baina ya Sudan na Sudan Kusini wakaribishwa na Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Muafaka baina ya Sudan na Sudan Kusini wa kutatua mzozo kuhusu mafuta umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Mwishoni mwa wiki nchi hizo mbili zimetangaza kwamba zimekamilisha muafaka kwa Sudan Kusini kusafirisha mafuta yake kwa kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan na jinsi ya kugawana mapato ya mafuta hayo. Katibu Mkuu [...]

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO kutembelea Myanmar kuunga mkono mageuzi ya kisiasa yanayotekelezwa sasa

Kusikiliza / Irina Bokova

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova anatazamia kuanza ziara ya siku nne nchini Myanmar ambako pamoja na mambo mengine lakini anatazamia kuweka zingatio lake katika eneo la mageuzi ya kisiasa yanayoendelea nchini humo. Katika ziara yake hiyo inayoanza August 7 hadi 10 Bi Bokova anatazamia [...]

06/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la haki za msingi za binadamu bado ni changamoto kubwa kwa Myanmar, Mtaalamu wa UM

Kusikiliza / Tomas Ojea Quintana

  Juhudi zinapaswa kuchukuliwa sasa kwa taifa la Mynmar kuzitafutia majawabu changamoto zinazojitokeza kwenye maeneo ya haki za binadamu hasa katika wakati huu kunakoshuhudiwa kipindi cha mpiti kuelekea kwenye ujenzi imara wa mifumo ya kidemokrasia. Kwa mujibu wa mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki za binadamu nchini humo Tomas Ojea [...]

06/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO na PAMP kuzindua shughuli ya ukusanyaji wa safaru na medali

Kusikiliza / sarafu na medali

Shughuli ya shirika la sayansi na utamadunia la Umoja wa Mataifa ya kukusanya sarafu na medali itaaanza kote duniani kupitia makubalino kati ya shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na kampuni ya kuosha madini ya PAMP S.A. Programu hiyo mpya itasaidia kukusanya sarafu na medali zilizotengezwa kwenye nchi binafsi na [...]

06/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Machafuko yanayoendelea Syria yanatia Hofu:UNSMIS Babacar

Kusikiliza / Babacar Gaye-UNSMIS

Mkuu wa mpango wa uangalizi wa Umoja wa mataifa nchini Syria UNSMIS Luteni Jenerali Babacar Gaye akizungumzia hali ya machafuko yanayoendelea Aleppo nchini Syria amesema anatiwa hofu sana na hasa kwa kuzidi kuzorota kwa hali na athari zake kwa raia. Gaye amezitaka pande zote husika katika machafuko ya Syria kuwalinda raia na kuheshimu wajibu wao [...]

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya nchi za Caribbean imewataka wanachama wake 28 kutekeleza mpango wa UNCTAD

Kusikiliza / nemba ya jumuiya ya nchi za Caribbean

Mpango wa tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi na Biashara UNCTAD ujulikanao kama eRegulations ambao unazisaidia nchi kujikwamua kwa kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwazi katika taratibu na sheria za biashara unapaswa kupanua wigo wake kwa mataifa 28 ya muungano wa nchi za Caribbean ACS umesema muungano huo. Mpango wa eRegulations hivi sasa unatekelezwa katika [...]

06/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

FAO yapunguza matarajio ya mavuno ya mpunga kwa mwaka 2012

Kusikiliza / mpunga

Shirika la chakula na kilimo FAO limeshusha matarajio yake ya kimataifa ya zao la mpunga kwa mwaka 2012 kutokana na mvua chache za Monsoon nchini India, lakini limesema kwa jumla mazao ya mpunga duniani bado yatasalia kuwa ya juu kuliko mwaka 2011. FAO imeshusha maratajio ya mpunga mwaka huu kwa tani milioni 7.8 kutokana na [...]

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati Kukiadhimishwa kumbukumbu ya Hiroshima Dunia yatafuta upokonyaji wa Nyuklia:Ban

Kusikiliza / Hiroshima Peace Memorial Park in Hiroshima,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema watu wote duniani wanatafta njia za upokonjayi wa silaha za nyuklia kimataifa kwa minajili ya kuwa na mustakhbali huru bila silaha hizo. Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu kwenye mkutano wa kimataifa dhidi ya mabomu ya atomic na Hydrogen. Ban amesem,a watu wote wanaja kwamba lengo [...]

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yalaani mauaji ya mfanyakazi wake Kordofan Kusini

Kusikiliza / magari ya WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Jmapili limelaani vikali mauaji ya mmoja wa madereva wake katika shambulio kwenye jimbo la Sudan la Kordofan Kusini ambako machafuko yanaendelea kwa kikwazo kwa juhudi za kufikisha misaada za shirika hilo. Kwa mujibu wa WFP Jamal Al Fadil Farag Allah mwenye umri wa miaka [...]

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuendelea kuibana Morocco iondoke Sahara Magharibi:Tanzania

Kusikiliza / bendera ya Polisario

Serikali ya Tanzania leo imeitaka Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo pia Umoja wa Mataifa kuzidisha mbinyo kwa Morocco ilinayokalia kwa mabavu ardhi ya watu wa Sahel Magharibi ili iachie eneo hilo na kuwaacha raia wake wakiendesha shughuli zao kwa matakwa yao. George Njogopa anaarifu zaidi. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

06/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa ajili ya Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu na Rais wa Baraza Kuu

Jumuiya ya Kimataifa imetolewa wito na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban kuchukua hatua za kumaliza mgogoro unaoendelea katika Syria. Bwana Ban amesema haya katika mkutano wa Baraza Kuu wa kupitisha azimio la kulaani vurugu inayoendelea nchini. Alisema mgogoro wa Syria ni mtihani wa kuwepo kwa Umoja wa Mataifa na kazi yake yote. “Shinikizo [...]

03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yatoa fedha zaidi kwenye mchango wa kusaidia wakimbizi wa kipalestina

Kusikiliza / Filippo Grandi

Serikali ya Ujerumani umetoa msaada ya Euro milioni mbili zitakazosaidia kulisha wakimbizi wa kipalestina 667,500 kwenye ukanda wa Gaza. Fedha hizo ni msaada wa ombi la mwaka 2012 la shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbzii wa kipalestina UNRWA la mwaka 2012 la kusaidia wakimbizi kwenye ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi. Mkuu wa [...]

03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mswaaada wa Sharia wafika kwenye bunge la Liberia

Kusikiliza / bunge la Liberia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inahofia mswaada wa sharia ambao hivi sasa umefikishwa mbele ya bunge la Liberia ambo unapendekeza mabadilikon ya sheria ambayo yatafanya kuwa ni uhalifu tabia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Sheria ambayo imeshapitishwa na bunge l seneti infany kuwa ni kosa la jinai la kiwango cha [...]

03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua zinazopigwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango Endelevu UNDAP,nchini Tanzania

Kusikiliza / UNDAP Tanzania

Umoja wa Mataifa kwa sasa unatekeleza mpango wa majaribio katika nchi nane barani Afrika kwa shabaya ya kuharakisha maendeleo. Mpango huo pamoja na mambo mengine pia unatupia macho maeneo ya ustawishaji wa demokrasia, ukuzaji uchumi na kusukuma mbele shughuli za kimaendeleo. Katika makala yetu leo mwenzetu George Njogopa anamulika juhudi zinazofanywa na Shirika hili la [...]

03/08/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Google and ITU washirikiana kutoa bure kimataifa takwimu za teknolojia

Kusikiliza / nyembo ya kampuni ya Google

  Takwimu za muungano wa kimataifa wa teknolojia ya mawasiliano ITU na teknolojia ya mawasiliano ICT sasa zinapatikana kupitia mtandao wa umma wa utafutaji takwimu yaani Google Public data Explorer kupitia kwenye wavuti.   Kwa ushirikiano wa mtandao wa Google na ITU sasa watumiaji wa mtandao wanaweza kutafuta na kuona takwimu muhimu zilizopo za teknolojia [...]

03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR na Mashirika yasiyokuwa ya serikali watoa huduma kwenye kambi ya Yida

Kusikiliza / hali ya njaa nchini Sudan Kusini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wanafanya juhudi kukabilina na visa vya utapiamlo, magonjwa na vifo kwenye kambi mbili zinazowahifadhi wakimbizi kutoka Sudan. Wahudumu wa afya kwenye kambi ya Yida jimbo la Unity walishuhudia kuongeza kwa vifo kwa watoto kwemye kambi mwezi Juni na mapema mwezi Julai. Mwa muda wa [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yafungua Ofisi Dollo wakati Wasomali wakizidi kukimbia Ukame

Kusikiliza / nemba ya UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefungua ofisi mjini Dollow na kurejesha uwepo wake kwenye mji huo wa karibu na mpaka wa Somalia na Ethiopia ili kukabiliana na ongezeko la wakimbizi wa Somalia wanaokimbia ukame. Takwimu za karibuni zinaonyesha kwamba watu 11,000 zaidi wametawanywa ndani ya Somalia tangu mwanzo wa Aprili kutokana [...]

03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mamia ya watu wanaendelea kuhama nchini Syria kila siku kunapoendelea kushudiwa mapigano:UNHCR

Kusikiliza / Bw. Herve Ladsous wa UM

Huku ghasia zikiendelea kuchacha nchini Syria watu zaidi wanaendelea kuhama makwao kutafuta usalama wao. Takriban watu milioni 1.5 waliohama makwao wamesalia ndani mwa Syria wakitafuta hifadhi kwa familia zingine au kwa makao ya muda. Watu wengine wamekwama wakiwa na hofu na hofu ya kujipata kati kati mwa mapigano au kulengwa wakati wanapohama. Mji wa Aleppo [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasema linatupia macho hali za kibidamu nchini Syria

Kusikiliza / Herve Ladsous

Huku machafuko yakizidi kuchacha nchini Syria mnamo wakati mjumbe maalumu wa upatanishi kwenye mzozo huo Kofi Annan akiashiria kuachia wadhifa wa usuluhishi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu,Baraza la Usalama linatafakari hatma ya raia milioni 3 walioko kwenye hali mbaya wakihitaji msaada wa dharura. Wakati huu Ufaransa imechukua kiti cha urais wa kupokezena katika baraza hilo [...]

03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO imefanya Ushirikiano na Wizara ya afya nchini Uganda kudhibiti ugonjwa wa Ebola

Kusikiliza / mlipuko wa Ebola nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa kwa sasa kumeripitiwa visa 50 vya ugonjwa wa Ebola na vifo 16 vilivyosababishwa na ugonjwa huo nchini Uganda. Tangu siku ya Jumanne visa kadha vya ugonjwa huo vimeripotiwa hospitalini lakini ni watu wawili walioripotiwa kuaga dunia. Wizara ya afya nchini Uganda inashirikiana na washikadau pamoja na washirika wake [...]

03/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka Waasi wa M23 kuacha Mapigano

Kusikiliza / MONUSCO

Baraza la Usalama limerejelea mwito wake kutaka makundi ya askari waasi wanaoendesha vitendo viovu huko kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuweka silaha nchini kwa mustakabala wa taifa hilo na wananchi wake. Baraza hilo limesema kuwa kundi la askari waasi wa M23 wanapaswa kujieopusha na matumizi ya silaha kuzorotesha usalama katika eneo walikopiga ng'ome [...]

03/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yajenga Vituo vya Afya Kuwasaidia jamii ya waliokosa makazi Zimbabwe

Kusikiliza / kituo cha afya nchini Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM leo limekabidhi vifaa tiba kwa vituo vya afya vinavyotoa huduma za utabibu katika maeneo ya vijijini vilivyoko kusini mashariki mwa mji wa Harare. Vifaa hivyo lakini vinatazamiwa kuwa habari njema kwa mamia ya waliokuwa wafanyakazi wa mashambani ambao wengi wao hawana makazi maalumu Kiasi cha wafanyakazi [...]

03/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

OHCHC yasema kuwa vikosi vya usalama vimewaua watu wakati maaandamno kwenye jimbo la Darfur

Kusikiliza / Bi Ravina Shamshadani wa OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema kuwa vikosi vya usalama kwenye jimbo la Darfur huenda viliwaua watu wannane ambapo watano kati yao walikuwa ni wanafunzi walio na umri wa chini ya miaka mitano na kuwajeruhi watu wengine 50 siku ya Jumanne wakati walipowafyatuilia risasi waandamanaji kwenye mji wa mji mkuu [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii ya Kimataifa imetakiwa kufanya juhudi za Kukabiliana na hali nchini Mali

Kusikiliza / UNHCR

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonia Guterres ametoa wito wa jamii ya kimataifa kufanya kila iwezalo kukabiliana na hali iliyopo nchini Mali na kuzitaka nchi kusadia oparesheni ambazo sasa hivi zinakabiliwa na uhaba wa fedha kwenye eneo hilo ambalo halina uwezo wa kujilisha. Zaidi ya watu 250,000 wameikimbia Mali kwa [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawapa Mafunzo Wafugaji nchini Kenya

Kusikiliza / wafugaji nchini Kenya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha shughuli ya kuwapa mafunzo wafugaji 180 kutoka maeneo sita kwenye wilaya ya Daadab kaskazini mwa Kenya kuhusu jinsi watakavyowatunza mifugo wao wakati kunapotokea ukame. Ufugaji wa ng'ombe ndio tegemeo kwa wenyeji wa kaskazini na kaskazini masharki mwa Kenya walioko maelfu ya wasomali wanaokimbia vita na ukame nchini mwao. [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasaidia waathirika wa Mafuriko DPRK

Kusikiliza / mafuriko kaskazini mwa Korea

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK wanatoa msaada wa chakula, vifaa visivyo chakula, madawa, maji na vifaa vya usafi kufuatia athari za mafuriko nchini humo. Mashirika hayo yanatarajiwa kuendelea kusaidia kutokana na mahitaji ya watu wa DPRK. Wakati kipaumbele kimetolewa kwa nchi ambazo zimemetembewa, [...]

03/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyota wa Muziki Beyonce Aungana na Mashirika ya Kimataifa kwenye Siku ya Kibinadamu Duniani

Beyonce

Nyota wa muziki Beyonce na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa wanazindua kampeni ya kimataifa hii leo inayowashauri na kuwapa watu motisha ya kuwafanyia vyema wengine. Siku ya kimataifa ya kibinadamu inaadhimishwa ili kusherehekea ubinadamu na moyo wa watu kusaidia watu. Video ya wimbo ya nyota huyo kwa jina "I Was Here" inatarajiwa kuchezwa [...]

02/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Familia zaidi ya 129,000 za Kipalestina kupokea msaada wa chakula kutoka Uturuki

Kusikiliza / nemba ya UNRWA

Zaidi ya familia 129,000 za Kipalestina zitafaidika na msaada wa chakula kutoka serikali ya Uturuki ambao unathamani ya dola milioni 6.6 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada klwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Tani 12,500 za ngano zitawasili katika wiki nane zijazo hku awamu ya kwanza ikiwasili leo na zitaweza kuwalisha watu wapatao 687,000 [...]

02/08/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Misaada zaidi inahitajika kuwafadhili wakimbizi wa Mali walioko mafichoni:Guterres

Kusikiliza / Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa shirika la kuwahumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres amesema kuwa wakati huu kuna hali ya mkwamo inayowandama mamia ya wakimbizi wa Mali waliokwama vichakana na akaenda mbali zaidi kwa kuitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza mafunga ya msaada kwa ajili ya kuwanusuru raia hao. Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuogeza [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amedhibitisha mwakilishi wake Yemen

Kusikiliza / Jamal Benomar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amedhibitisha bwana Jamal Benomar ambaye amepewa jukumu la kuwa mwakilishi wake huko Yemen akihusika zaidi na jukumu la kujenga mashirikiano mema hasa wakati huu taifa hilo likiwa kwenye kipindi cha mpito. Bwana Benomar amekuwa kifanya kazi kama mwakilishi wake nchini humo kuanzia mwezi April mwaka jana lakini [...]

02/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bima inaweza kusaidia kuwalinda maskini dhidi ya Ongezeko la joto duniani:ILO

Kusikiliza / ILO

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO hali ya hewa haiwezi kuwekewa bima lakini baadhi ya athari zake zinaweza kukatiwa bima hata kwa masikini ambao huathirika zaidi na athari za ongezeko la joto duniani. Craig Churchill ambaye anaongoza kitengo cha ILO kinachohusika na masuala ya bima anasema licha ya changamoto, kwa msaada wa ruzuku, [...]

02/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mataifa lazima yakabili Chuki, Ghasia na Ubaguzi dhidi ya Roma:UM

Kusikiliza / roma-se-europe

Mataifa yote na hususani yenye jamii za Waroma lazima leo yaadhimishe kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya Waroma yaani Roma Holocaust, huku yakijikita katika kukabiliana na chuki, ghasia na ubaguzi dhidi ya Roma na kutafuta suluhu ya kutengwa kwa jamii hiyo. Kauli hii imetolewa na wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Moto Waunguza Soko kwenye Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Kusikiliza / moto katika kambi ya Dadaab, Kenya

Moto mkubwa uliochoma soko katika Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya mwishoni mwa wiki umeonyesha haja ya kuwa na maandalizi bora ya moto na usalama Katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani. Moto ulizuka siku ya Jumapili jioni katika soko la kambi ya Dagahaley ambayo ni moja ya makambi tano katika Kambi kubwa ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kofi Annan Kujiuzulu kama mwakilishi wa UM na Umoja wa Nchi za Kiarabu Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Taarifa iliyotolewa hivi pnde na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Alhamisi inasema kwa masikitiko anatangaza taarifa za kujiuzulu kwa Kofi Annan kama mwakilishi maalum wa Umoja na moja wa nchi za Kiarabu nchini Syria. Bwana Annan amemuarifu Katibu Mkuu wa Muungano wan chi za Kiarabu Nabil El Araby kuhusu nia yake ya [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uongozi wa Somalia lazima kujitahidi Kuwalinda Waandishi Habari:Mahiga

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ametoa wito kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwalinda waandishi habari na kazi zao. Mahiga amesema afosi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kisiasa ya Somalia UNPOS iko tayari kuisaidia serikali kukomesha ukatili na unyanyasaji dhidi ya waandishi na kumaliza mzunguko wa wahalifu [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka Amani idumu wakati wa Kuhamishwa kwa Watoro wa Iran kutoka kambi nchini Iraq

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amezitaka pande mbili husika kushirikiana na kukamilisha kwa amani kuhamishwa kwa watoro wa Iran waliosalia kwenye kambi moja nchini Iraq. Kuambatana na makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi Disemba kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq ni kwamba theluthi mbili ya watu au 2000 wamehamishwa kwenda [...]

02/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU kuboresha uwezo wa Broadband barani Afrika

Kusikiliza / nembo ya ITU

Mungano wa teknolojia ya mawasiliano ITU na kampni ya Nexpedience moja ya wasambazaji wakubwa wa miundombinu ya broadband wanashirikiana ili kupanua wigo wa fursa ya upatikanaji wa broadband barani Afrika. Chini ya muafaka wa pande hizo mbili Nexpedience itatoa mitambo ya thamani ya dola milioni 1 itakayopelekwa katika mataifa sita barani Afrika. Taifa la kwanza [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WaSyria milioni 3 wanahitaji msaada wa Chakula, Mazao na Mifugo:FAO na WFP

Kusikiliza / msaada wa chakula kwa watu wa Syria

Takribani watu milioni tatu wanahitaji msaada wa chakula, mazao na mifugo nchini Syria kwa mujibu wa tathimini ya karibuni iliyopfanywa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria. Watu milioni 1.5 kati ya hao wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita ijayo na hususani kwenye maeneo ambayo yanashuhudia vita [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuendelea kutoa Msaada wa Chakula kwa Wakimbizi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / msaada kutoka WFP, Sudan

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema lina mpango wa kuendelea kutoa msaada unaohitajika haraka wa chakula kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi kwenye jimbo la Upper Nile Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WFP Sudan Kusini Chris Nikoi wakimbizi wanaowasili kamimbini huwa wamedhoofu na wenye njaa baada ya kusafiri wiki kadhaa msituni [...]

02/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu Ban ashtumu Mashambulizi katika mji mkuu wa Somalia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Ugaidi ni lazima usiruhusiwe kurudisha nyuma mafanikio muhimu katika mchakato wa amani unaoendelea wa kuunda serikali mpya na taasisi za kudumu nchini Somalia. Huu ndio ujumbe wa Katibu Mkuu, katika taarifa aliotoa kufuatia jaribio la kushambulia jengo ambapo Mkutano wa Kimataifa wa Baraza la Katibu uliokuwa ukifanyika, kupitisha katiba mpya leo Jumatano. Katibu Mkuu amekaribisha [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika ni lazima izingatie Biashara ya Kilimo kwa Uchumi Wake:Yumkella

Kusikiliza / Kandeh Yumkella

Bara la Afrika linahitaji kutilia maanani mseto wa uchumi pamoja na bishara ya kilimo ili kuweza kuliinua bara hilo kutoka umaskini na kuliweka kwenye mkondo wa maendeleo. Hii ni kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu kutoka kwenye Umoja wa Mataifa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo ya kiviwanda la Umoja wa Mataifa Kandeh [...]

01/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baada ya miaka Takribani 40 Somalia yapata Katiba Mpya:Mahiga

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia na wawakilishi wa majimbo yote ya nchi hiyo wanaokutana Moghadishu wamepitisha kwa wingi wa kura katiba mpya  ambayo inafungua mlango wa kuchaguliwa kwa serikali mpya mwezi huu. Jumla ya wawakilishi 825 walikuwa wakijadili kuhusu katiba hiyo kwa juma zima na 621 wamepiga kura ya ndiyo, 13 wamepinga na [...]

01/08/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban amteua mwanadiplomsia wa Austria kama mratibu wa Masuala ya Wingi wa Lugha

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Peter Launsky

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua msaidizi wake wa masuala ya mawasiliano na habari kwa umma Peter Launsky-Tieffenthal kuwa mratibu wa masusla ya wingi wa lugha. Uteuzi huo unajiri baada ombi la baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa Ban wa kumataka amteue afisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa [...]

01/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

China kupigwa na vimbunga viwili kwa wakati mmoja

Kusikiliza / kimbunga

Watabiri wa hali ya hewa wameitahadharisha China juu ya uwezekano wa kuzuka kwa kimbunga kiitwacho Saola ambacho kinaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na maisha ya watu. Tayari watu kumi wamefariki dunia wakati kipunga hicho kilipopiga sehemu ya Philippines Kwa mujibu wa tangazo lilitolewa na mamlaka ya hali ya hewa ya kimataifa WMO pamoja na [...]

01/08/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vita vyashika Kasi Syria, Serikali yatumia Ndege za Kivita na Wapinzani Silaha Nzito:UNSMIS

Kusikiliza / silaha nzito nchini Syria

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Syria unasema waangalizi wa kimataifa wameshuhudia ndege za kivita zikishambulia kwenye mji mkbwa kabisa wa Syria ambako mapigano yametanda kwa karibu wiki mbili sasa. Msemaji wa mpango huo UNSMIS Susan Ghosheh ameelezea hofu yake kuhusu hali mjini Aleppo. Amesema jana kwa mara ya kwanza wameshuhdia mashambulizi hayo ya anga [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP yakaribisha hatua ya Nigeria ya Usafishaji Mafuta Ogoniland

Kusikiliza / Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limekaribisha uamuzi wa serikali ya Nigeria wa hatua kubwa ya usafishaji wa mafuta machafu ya Ogoniland kwenye jimbo la Niger Delta. Miezi 12 iliyopita UNEP iliwasilisha tathimini yake ya uchafuzi wa mafuta Ogonland kwa Rais wa serikali ya Nigeria Goodlck Jonathan ikielezea athari kubwa za mafuta hayo [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yataka unyonyeshaji kwa kina mama urahisishwe

Kusikiliza / wiki ya unyonyeshaji

Katika maadhimisho ya 20 ya wiki ya unyonyeshaji duniani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema sera imara za kitaifa kuunga mkono unyonyeshaji zinaweza kuzuia vifo vya takribani watoto milioni moja wa chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka katika nchi zinazoendelea. UNICEF inasema licha ya shahidi kwamba unyonyeshaji unazuia maradhi [...]

01/08/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Masuala ya Syria na Mali yataendelea kutawala Baraza la Usalama mwezi Agosti

Kusikiliza / rais wa Baraza la Usalama-Ufaransa

Ufaransa inaanza mzunguko wa Urais wa Baraza la Usalama mwezi huu wa Agosti na balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa anatumai kwamba kutakuwa na muafaka wa kimataifa kuhusu kuchukua hatua dhidi ya Syria. Balozi Gérard Araud anasema ni bahati mbaya kwamba wajumbe hawajapata suluhu ya mgogoro wa Syria ambao umeshika kasi wiki za karibuni. Balozi [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yawapelekea msaada wa dharura wa chakula Allepo

Kusikiliza / WFP-Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limepeleka msaada wa chakula kwa watu 28,000 mjini Aleppo kwa siku chache zijazo baada ya kupata taarifa za upungufu wa chakula,g esi na umeme vilivyosababishwa na mapigano yanayoendelea kwa wiki kadhaa sasa. Shirika hilo linasema hali ya kibinadamu inazidi kuzorota na mahitaji ya chakula yanaongezeka [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge la Somalia lapitisha Katiba Mpya

Kusikiliza / Katiba mpya ya Somalia

Viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia wanaokutana Moghadishu wamepitisha kwa wingi wa kura katiba mpya ya nchi hiyo ambayo inafungua mlango wa kuchaguliwa kwa serikali mpya mwezi huu. Jumla ya wabunge 825 walikuwa wakijadili kuhusu katiba hiyo kwa juma zima na wabunge 621 wamepiga kura ya ndiyo, 13 wamepinga na 11 hawakupiga kura kabisa. [...]

01/08/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930