WHO yaonya kuhusu Maradhi ya Kuambukiza wakati wa Olimpiki London

Kusikiliza /

mashindano ya Olympics

Wakati mashindano ya Olimpiki yakifunguliwa rasmi mjini London, Shirika la Afya Duniani, WHO, limeelezea hofu yake kuhusu masuala ya afya kutokana na mikusanyiko ya halaiki wakati wa mashindano hayo. Shirika la WHO limesema kuwa hali kama hii inahusisha mkusanyiko wa watu wengi, ambao huenda wakabeba maradhi ya ajabu ajabu.

Limeonya kuwa hatari ya kuambukiza ipo juu zaidi kuliko kawaida, na kuongeza hali hii huenda ikatoa nafasi kwa ugaidi wa bayo, kupitia kwa maji na chakula, au kemikali kali. Shirika hilo limesema kwa sababu kama hizi, ni lazima mfumo wa afya uwe tayari kukabiliana na chochote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031