Wataalamu wa UM Wachunguza Visa vya Kutoweka kwa Lazima
Kundi la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masusla ya kutoweka kwa watu kwa lazima au kwa hiari limechunguza ripoti 13 za kutoweka kwa lazima pamoja na visa vingine 200 vikiwemo vya hivi majuzi.
Wataalamu hao watano huru walichunguza kesi hizo zinazohusu mataifa 32 kote ulimwenguni. Waatalamu hao pia walijadili madai yaliyowasilishwa kuhusu vizingiti vivyozuia utekelezwaji wa makubaliano na kufamya mazungumzo jinsi watakavyofanya kazi.
