UNHCR yapongeza Hatua ya Kuokoa zaidi ya watu 60 kwenye Pwani ya Croatia
Kusikiliza /Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limepongeza hatua ya walinzi wa pwani ya Croatia ya hapo jana ya kuwaokoa watu 65 waliokuwa wakielekea kwenye mashua katika eneo la Adriatic.
Mashua hiyo ilionekana ikielekea kutoka kisiwa cha Mljet Jumapili usiku ambapo walinzi wa pwani walitoa chakula na madawa kwa waliokuwa kwenye mashua kabla ya kuivuta kwenda bandarini. Mashua hiyo inaripotiwa kundoka nchini Ugiriki kabla ya kukumbwa na hitilafu za kimitambo na kuelea baharini kwa muda wa siku mbili. Abiria wote waliokuwemo kwenye mashua walikuwa ni wa kiume wanaokisiwa kuwa raia wa mataifa 12 yakiwemo Syria , Afghhanistan, Somalia na Misri. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.
(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)
