UNHCR yahofia Hali ya Afya Katika Kambi za Wakimbizi Sudan Kusini

Kusikiliza /

wakimbizi wa Sudan

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeelezea hofu yake kuhusu hali ya afya katika kambi za wakimbizi zilizopo Sudan Kusini, na hasa uwezekano wa mkurupuko wa magonjwa katika kambi hizo. Kwa mujibu wa UNHCR, hali katika kambi za wakimbizi imeendelea kuzorota katika kipindi cha siku chache zilizopita, kufuatia idadi kubwa ya wakimbizi wanaozidi kuwasili na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Shirika la UNHCR na wahudumu wa afya wameanza kujiandaa kwa kufanya upimaji wa halaiki ili kupata idadi kamili ya watu waliofariki, na ile ya watu ambao wamepata chanjo katika kambi zote za wakimbizi kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity State. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA  ADRIAN EDWARDS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930