UNECE Inasaidia Udhibiti wa Taarifa kuhusu Maji ya Asia ya Kati
Kusikiliza /Washiriki katika warsha ya udhibiti wa masuala ya maji iliyofanyika mapema mwezi huu mjini Almaty wamepitisha sheria na muongozo wa miaka mitatu hadi mitano za kuanzisha takwimu za udhibiti wa maji katika eneo la Aral Sea Basin huko Asia ya Kati.
Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo ya Ulaya UNECE imesema inasaidia katika mikataba ya masuala mbalimbali ya maji kwenye eneo hilo ikiwepo ushiriki wa jamii na fursa za kupata taarifa, ajali za viwandani na athari za mazingira.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Bank ya dunia, ushirikiano wa maendeleo wa Uswis na UNECE iliwaleta pamoja washiriki ktoka mataifa 50 na wataalamu kutoka Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgystan, Tajikistan, Turkmenistan , Uzbekistan, mashirika mbalimbali ya kikanda na wahisani.
