Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na aina zote za ubaguzi: UM

Kusikiliza /

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki za watu wa kigeni na aina zingine za ubaguzi, ametoa wito kwa mataifa kote ulimweguni kuzingatia kwa karibu sana ishara za mwanzo za ubaguzi wa rangi, ambao hatimaye huenda ukakolea na kusababisha mizozo na ukiukaji mbaya zaidi wa haki za binadam.

 Mtaalam huyo, Mutuma Ruteere, ameliambia Baraza la Haki za Binadam mjini Geneva wiki hii kuwa, kuibuka kwa vyama vya kisiasa na makundi mengine ya mirengo mikali, pamoja na suala la ubaguzi wa rangi katika jamii na katika mashindano ya michezo, kunaongeza tishio la jinamizi hili, na zaidi hasa katika mazingira ya sasa ya mdororo wa uchumi duniani.

Katika mahojiano na mwandishi wa redio ya Umoja wa Mataifa, Joshua Mmali, Bwana Ruteere amemwelezea zaidi kuhusu ripoti zake mbili kwa Baraza la Haki za Binadam.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930