Hukumu ya Lubanga itasaidia Kuwalinda Watoto, asema mtaalam wa UM

Kusikiliza /

Radhika Coomaraswamy

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya vita, Radhika Cooomeraswamy, ameupongeza uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, dhidi ya mbabe wa kivita Thomas Lubanga kama muhimu sana. Thomas Lubanga, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuwaingiza watoto katika kundi lake la waasi kama wanajeshi muongo mmoja uliopita.

Bi Coomeraswamy amesema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa wa haki, na kwamba utasaidia katika kuwazuia wengine kuwaingiza watoto katika jeshi na vita. Bi Coomeraswamy alikuwa ametoa baadhi ya maneno ambayo yametumiwa na mahakama hiyo kuhusu ajira ya watoto katika jeshi, ili kuwalinda watoto wengi zaidi, wakiwemo wasishana, kutokana na kulazimishwa kuingia katika ajira ya aina yoyote ile katika vita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031