Helikopta za UM Zakabiliana na Waasi wa M23 Kivu Kaskazini, DRC

Kusikiliza /

 

Roger Meece

Ndege za aina ya helikpota za Umoja wa Mataifa, zimekabiliana na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mnamo siku ya Alhamis, kwa mujibu wa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Roger Meece.

Bwana Meece amesema, hali mashariki mwa Kongo imelazimu matumizi ya helikopta hizo, ambayo si ya kwanza katika hali kama hiyo. Amesema Umoja wa Mataifa una wajibu wa kufanya vyovyote vile kuulinda usalama wa raia na maeneo ya watu wengi kama vile mji wa Goma, kutokana na uvamizi zaidi wa wanamgambo wa M23.

Amesema wanajaribu kutumia ndege za kulinda doria na habari kutoka kwa duru zote zilizopo, na kushirikiana kwa karibu na jeshi la taifa la Kongo, ili kuelewa malengo na mienendo ya kundi la M23.

[CLIP YA ROGER MEECE]

Wakati huo huo, mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo WFP na OCHA yanasema, wahudumu wake hawana uwezo wa kuwafikia wakimbizi wote wanaohitaji msaada, kwani njia nyingi hazipitiki kwa sababu za kiusalama. Hali hiyo imefanya mashirika ya huduma za kibinadamu kusitisha shughuli za kutoa misaada na kupunguza usafiri wa wahudumu na shehena za misaada. Hata hivyo, hakuna shrike lolote ambalo limeondoka au kukoma kukomesha shughuli zake kabisa eneo la Rutshuru au jimbo la Kivu Kaskazini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031