Nyumbani » 25/07/2012
Entries posted on “Julai 25th, 2012”
Kusikiliza /

Mkuu mpya wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS, amesema anatarajia kupungua kwa kiwango cha machafuko wakati wa kipindi cha mwisho cha operesheni ya UNSMIS nchini humo. Luteni Jenerali Babacar Gaye, ambaye amekaribishwa kwa waandishi wa habari mjini Damascus siku ya Jumatano, amesema anashika usukani wakati mgumu sasa. Hata hivyo, amesema kuwa UNSMIS inarejea [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Afisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA, imetangaza kuwa Umoja wa Mataifa utapunguza kiasi cha fedha za msaada wa kimataifa unazochangisha kwa ajili ya kulisaidia taifa la Haiti kwa sababu mwitikio wa wafadhili haujakuwa wa kutia moyo mwaka huu. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port au Prince, afisa mkuu [...]
25/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye maeneo yaloathirika na vita, Radhika Coomeraswamy, leo amezindua tovuti mpya, ambayo itasheheni habari na maktaba ya maelezo muhimu kwa ajili ya wale wanaotaka kuyapata. Tovuti hiyo http://childrenandarmedconflict.un.org itakuwa na maelezo na taarifa muhimu zinazotolewa na idara hiyo ya Umoja wa Mataifa, na kuonyesha picha [...]
25/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na maji na usafi Catarina de Albuquerque ametoa wito kwa serikali ya kiribati kushughulikia masuala ya maji na usafi. Mjumbe huyo anasema kuwa alishangazwa na idadi ya juu ya vifo vya watoto nchini Kiribati ambavyo ni vya juu zaidi kwenye nchi Pacific akiongeza kuwa ikiwa [...]
25/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Watu 350 kutoka kote ulimwenguni wanakusanyika mjini Geneva wiki hii kwa mkutano wa 62 wa kamati maalum kuhusu mkataba wa biashara ya kimataifa katika viumbe walio katika hatari ya kuangamizwa kabisa, CITES. Mkutano huo utaangazia jinsi ya kukabiliana na biashara haramu ya pembe za ndovu na vifaru, pamoja. Pamoja na hayo, mkutano huo pia utajadili [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur unasema kuwa amani imenukia kwa watu wa Darfuf lakini eneo hilo bado linakabiliwa na changamoto nyingi. Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID Ibrahim Gambari anasema kuwa bado yanasalia mengi ya kufanywa na huenda hali ya zamani ikarudia ikiwa hatua madhubuti [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Zaidi ya wahudumu wa afya 27,000 na watu wanaojitolea wametawanyika kwenye mikoa 16 nchini Afghanistan kwa muda wa majuma mawili yaliyopita kwa lengo la kuangamiza ugonjwa wa kupooza kupitia kwa kampeni mpya ya Umoja wa Mataifa. Kampeni hiyo inayotekelezwa na wizara ya afya ya umma nchini Afghanistan, mapema juma hili ilitoa chanjo kwa zaidi ya [...]
25/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania leo kimetangaza ripoti yake ya awali inayoangazia mwenendo wa haki za kibinadamu kwa nchi hii katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kutaja kasoro kadhaa ikiwemo kushamiri kwa matukio ya ubakaji unawandama hasa wanawake na watoto wa shule pamoja na vyombo vya dola kuangukia kwenye lawama [...]
25/07/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa wito kwa serikali kote duniani kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Hepatitis, ambao huathiri ini na unasemekana kuwaua watu milioni moja kila mwaka. Ujumbe huu wa WHO umetolewa kabla ya Siku ya Hepatitis Duniani, ambayo huadhimishwa kila Julai 28. Takriban watu nusu bilioni huumwa mara kwa [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa nchi jirani za Syria kuacha mipaka yake wazi kwa ajili watu wa Syria wanaokimbilia usalama wao. Serikali ya Uturuki imeripotiwa kufunga mipaka yake kwa sababu ya kuzorota kwa hali ya usalama. Katika mahojiano na radio ya Umoja wa Mataifa mjini Genevea, msemaji wa [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nusu ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS, wameshaondoka nchini humo kwa mujibu wa msimamizi wa shughuli za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous. Wiki ilopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza muda wa shughuli za UNSMIS kwa kipindi cha mwisho cha siku 30. Bwana Herve Ladsous amewaambia waandishi [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki za binadamu nchini Myanmar anatazamiwa kutembelea eneo hilo akiwa na dhima ya kutathmini hali ya mambo. Tomás Ojea Quintana anatazamiwa kuwa huko kuanzia July 30 hadi August 4 akitathmini hali jumla ya haki za binadamu pamoja na maendeleo mengine. Taifa hilo linapitia kwenye mageuzi makubwa [...]
25/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesema kuwa amehuzunika na kusononeshwa na taarifa za kufariki dunia kwa rais wa Ghana John Atta Mills na ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa taifa hilo. Amesema jamii itaendelea kumkumbuka daima kiongozo huyo ambaye alijitolea muda wote kuwatumikia watu wa taifa lake. Amesema katika [...]
25/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amekubaliana na mpango uliotumika katika kuwateua wanachama 825 wa kundi linalotarajiwa kukutana juma hili kujadili , kupiga kura na kupitisha katiba mpya ya taifa hilo la pembe ya Afrika. Mahiga amesema kuwa ni jambo la kutia moyo kutokana na maendeleo yaliyopatikana. [...]
25/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »