Nyumbani » 23/07/2012
Entries posted on “Julai 23rd, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amewasili nchini Serbia siku ya Jumatatu, ambacho ni kituo cha hivi karibuni zaidi kwenye ziara yake Uchina na Kusini Mashariki mwa bara Ulaya. Ban amefanya ziara rasmi nchini Montenegro kwa mara ya kwanza, na kuelezea kuwa siku za usoni zitakuwa zenye matumaini makubwa kwa nchi hiyo. Amesema [...]
23/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Iraq (UNAMI), umelaani vikali mashambulizi mabaya ya bomu ambayo yamewaua watu wengi na kuwajeruhi wengine zaidi. Naibu mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisiasa, Gyorgy Busztin, ametaja viwango vya ghasia na umwagaji damu nchini Iraq kama vya kufadhaisha. Wimbi la ghasia lilizuka [...]
23/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi , kifua kikuu na malaria umetangaza matokeo mapya hii leo yanayoonyesha kuongezeka kwa matibabu ya ugonjwa wa ukimwi na kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa watu milioni 3.6 wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa sasa wanapata matibu kupitia programu [...]
23/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa linawasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limeelezea hofu yake kuhusu kuzorota zaidi kwa hali nchini Syria, ambako takriban wakimbizi nusu milioni wa Kipalestina wamekuwa wakiishi. Shirika la UNRWA pia limeelezea hofyu yake kuhusu usalama wa wafanyakazi wake na ule wa maeneo na vifaa vyake vya huduma, hasa katika mji mkuu Damascus. [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa mpango wa Shirika la Ajira Duniani kuhusu HIV na maeneo ya ajira, Alice Ouedraogo, ametoa wito kuhusishwa zaidi kwa sekta ya kibinafsi katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na HIV na UKIMWI. Akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kumi na tisa kuhusu UKIMWI unaoendelea mjini Washington Marekani, Bi Ouedraogo amesema hatua ikichukuliwa [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakurugenzi wa kampuni maarufu zaidi duniani, zikiwemo Levi Strauss, Coca-Cola, Johnson & Johnson, NBA na Virgin Unite, wametoa wito kwa nchi 46 ziondoe vikwazo vya usafiri kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV. Zaidi ya wakuu wa kampuni 20 wametia saini azimio la kuahidi kupinga vikwazo vinavyohusishwa na HIV katika kuingia, kuishi au kupata makazi [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalam wa kamati maalum ya Umoja wa Mataifa wamependekeza kuwa mwongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuwalinda wanunuzi unafaa kufanyiwa mabadiliko. Hayo ndiyo matokeo ya mkutano wa wataalam hao 300, uliofanyika katika makao makuu ya Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo, UNCTAD, kati ya Julai 12 na 13. Mkutano huo uliowajumuisha wataalam [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na lile la afya ya wanyama OIE yanatoa wito kwa nchi kushiriki kwenye utafiti wa kimataifa unaojumisha utafiti wa virusi vya ugonjwa wa sotoka vilivyo hai kwenye mahabara. FAO na OIE wanashirikiana katika kuangamiza virusi hivyo hatari na bidha zingine za kibaolojia zinazohifadhiwa kwenye zaidi [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wanasayansi, watafiti na viongozi wa ki-sera kutoka zaidi ya nchi themanini wanakutana wiki hii mjini Vienna Austria kujadili umuhimu wa kudhibiti udongo katika kuimarisha usalama wa chakula. Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, likishirikiana na Shirika la Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO, lina idara inayotumia mbinu za kinyuklia kufanya utafiti katika [...]
23/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »