Nyumbani » 20/07/2012 Entries posted on “Julai 20th, 2012”

Baraza la Usalama Laongeza Muda wa Shughuli za UNSMIS

Kusikiliza / UNSMIS

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeazimia kwa kauli moja kuongeza muda wa shughuli za waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS kwa kipindi cha siku 30 zaidi, na ambacho kitakuwa cha mwisho. Kura ya leo ya kuongeza muda wa shughuli za UNSMIS, imeelezewa kama yenye ufanisi mkubwa, kufuatia hasa kukataliwa kwa mswada [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lazitolea mwito Israel na Lebanon kuendelea na Majadiliano Kumaliza Mikwamo

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kuridhishwa kwake na hatua zinazopigwa kukwamua mkwaruzano wa mambo baina ya Israel na Lebanon ambazo zimeshindana kwa muda mrefu juu ya eneo linalojulikana ukanda wa Blue unaotenganisha mataifa hayo mawili. Hata hivyo baraza hilo limezihimiza mataifa hayo kuendelea kupiga hatua zaidi ili kuyatafutua ufumbuzi baadhi ya maeneo [...]

20/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Naibu Katibu mpya ataja Vipaumbele vyake Kwenye UM

Kusikiliza / Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ametaja vipaumbele anavyokusudia kuvipigua upatu wakati wa utumishi wake kwenye chombo hicho akitaja maeneo kama maendeleo na masuala ya kisiasa kuwa ndilo zingatio lake kuu. Naibu Katibu huyo ambaye amekabidhiwa wadhifa huo hivi karibuni hata hivyo siyo mgeni sana katika utendaji wa chombo hicho na yeye [...]

20/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya kulinda amani Cyprus

Kusikiliza / Cyprus

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha muda wa kusalia kwa vikosi vya kulinda amani nchini Cyprus hadi kufikia January 2013 huku pia likiwataka viongozi wa pande mbili Ugiriki ya Cyprus na wale wa Uturuki Cyprus kuongeza juhudi za majadiliano ili kukwamua mkwamo unaoliandama eneo hilo. Katika azimio lake liliungwa mkono na nchi 13, [...]

20/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Kuwa na Maji na Usafi aelekea Kiribati

Kusikiliza / Catarina de Albuquerque

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na maji na usafi Catarina de Albuquerque anaendelea na ziara yake kwenye eneo la Pacific ambapo anatarajiwa kuizuru Kiribati kuanzia tarehe 23 hadi 26 mwezi huu kukagua haki ya haki za bidamu kuhusu maji na usafi. Ziara yake ndiyo ya kwanza kufanywa na mtaalamu huru [...]

20/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Katiba mpya nchini Tunisia ni lazima izingatie haki za binadamu

Kusikiliza / Bendera ya Tunisia

Naibu mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Wha Kang kwa sasa anashiriki kwenye shughuli zinazohusu mazungumzo kuhusu katiba, sheria na haki za binadamu nchini Tunisia. Ofisi ya kamishina wa haki za binadamu nchini Tunisia imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali pamoja na mashirika ya umma kuhusu mazungumzo hayo. Kang amesisitiza kuwa katiba [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka pande Zinazozozana nchini Syria Kuzuia Mauaji ya raia

Kusikiliza / Navi Pillay

Huku mapigano yakiwa yanaendelea katika karibu kila sehemu nchini Syria, mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezitaka pande husika kuwa makini na kuhakikisha kuwa hakuna vifo vya raia kwenye mapigano hayo. Pillay anasema kuwa ghasia zinazoendelea hasa mijini ni hatari kwa usalama wa raia akiongeza kuwa watu wasiokuwa na hatia [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni mwaka mmoja tangu Kutangazwa Njaa nchini Somalia

Kusikiliza / wakulima wa Somalia

Imetimu mwaka mmoja tangu Umoja wa Mataifa kutangaza njaa kusini mwa Somalia. Janga hilo lililodumu kwa muda wa miezi sita lilisababisha kufa kwa maelfu ya watu na lilihitaji huduma kubwa za kibinadamu kabla ya kutangazwa kungamizwa mnamo tarehe tatu mwezi Februari mwaka huu. Kwa sasa Somalia inaelelea kupata nafuu lakini hata hivyo hali inasalia kuwa [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaangazia huduma za HIV kwa wahamiaji katika mkutano wa kimataifa wa 19 kuhusu Ukimwi

Kusikiliza / wahamiaji

Licha ya kauli za kisiasa kwenye viwango vya ngazi ya juu zaidi kuhusu kukabiliana na hatari ya kiafya na HIV kwa wahamiaji, watu hawa na jamii nyingine za kuhamahama bado wanashindwa kupata huduma za HIV katika mataifa mengi tu. Hii ni kasoro ya afya ya umma ambayo inahitaji kushughulikiwa kwa dharura, hasa katika ulimwengu unaotegemea [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR asikitishwa na Idadi ya Watu Walokimbia ghasia Syria

Kusikiliza / Antonio Guterres

Kamishna mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, leo ameelezea hofu yake kuhusu idadi ya watu wengi kupindukia wanaokimbia makwao kwa ajili ya ghasia zaidi nchini Syria. Maelfu ya raia wa Syria walivuka mpaka na kuingia Lebanon hapo jana. Duru za habari zinasema kati ya watu 8, 500 na 30, [...]

20/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lugha ya Kiswahili iko katika Hali ya Kupoteza Uasili Wake

Kusikiliza / kitabu

Lugha ya kiswahili ambayo huzungumzwa vyema katika eneo la Afrika mashariki na Kati, kwa sasa inapitia katika wakati mgumu kutokana na kuzuka kwa matumizi yasiyo sahihi ambayo watumiaji wengi, hupenda kuchanganya maneno ya kiswahili na kiingereza, yaani Kiswangilishi. Katika makala yetu leo, George Njogopa anamulika hali hiyo na hatma ya lugha yenyewe. (MAHOJIANO NA GEORGE [...]

20/07/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031