Nyumbani » 17/07/2012
Entries posted on “Julai 17th, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo ametoa wito kwa viongozi kote duniani kutumia vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twitter na Facebook mara kwa mara, hata zaidi ya jinsi anavyofanya yeye. Bwana Ban ambaye yuko ziarani Uchina, amesema amekuwa akiwasiliana mara kwa mara kupitia njia hii, ili kutoa ujumbe kwa dunia [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Anna, amefanya mazungumzo na rais wa Urusi, Vladmir Putin mjini Moscow kuhusu mzozo wa Syria. Bwana Anna ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kuwa mzaungumzo yake na rais Putin yamekuwa mazuri sana, na kwamba yameangazia hatua zinazohitajika kuchukuliwa ili kukomesha ghasia [...]
17/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mwenendo wa mabavu na utumiaji mkubwa wa vikosi vya usalama katika jaribio la kuwakabili waandamanaji nchini Maldives. Ripoti zinasema kuwa katika harakati za kuyakabili maandamano hayo,vikosi vya serikali vilitumia mbinu kadhaa ikiwemo kuendesha magari katika mwendo wa kasi kuelekea yaliko makundi ya waandamanaji. Taarifa za [...]
17/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji limetaka kupatiwa mafungu ya fedha ili kuwahudumia mamia ya wahamiaji ambao sasa wanaanza kurejea kwa wingi nchini Libya baada ya kuwa uhamishoni wakikimbia machafuko yaliyolikumba taifa hilo. IOM imesema kuwa kuna idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Chad wanaoingia kwa wingi nchini Libya kwa shabaha ya kusaka kazi [...]
17/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kuna ripoti kwamba idadi ya wakimbizi wa Syria walioandikishwa katika nchi za Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki imeongezeka mara dufu na sasa inakadiriwa kufukia 112,000. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa kiasi kikubwa cha wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwamba idadi hiyo inaweza kupindukia katika siku za usoni. [...]
17/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mfanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na mtaalam mmoja wa kimataifa wamejeruhiwa wakati gari lao liliposhambuliwa na watu wenye silaha mjini Karachi, Pakistan. Katika taarifa yake, WHO imesema hali za watu hao wawili ambao walikuwa wakifanya kwenye huduma ya WHO si mbaya sana. Wawili hao walikuwa wakisaidia mkakati unaoendelea nchini humo wa kuwapa watoto [...]
17/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema kuwa serikali ya Uholanzi imetoa dola milioni 2.1 kusaidia juhudi zake za kuwasaidia wahamiaji kutoka pembeni mwa Afrika, ambao wamekwama nchini Yemen wakijaribu kwenda Saudi Arabia. Mchango huo ambao ndio mkubwa zaidi kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa harakati za IOM Mashariki ya Kati, utatumiwa kutoa huduma za [...]
17/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametaka kukatwa rufaa kwa kesi inayohusu mauaji ya mwanaharakati wa haki za binadamu raia wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Floribert Chebeya Bahizire na kutoweka kwa dereva wake Fidèle Bazana Edadi. Bwana Chebeya alipatikana akiwa ameuawa tarehe mbili mwezi Juni mwaka 2010 viungani mwa [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa IOM Lacy Swing, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Sudan ambao wameathiriwa na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali ya Sudan na kundi la SPLM North katika jimbo la Blue Nile. Bwana Swing amesema hayo wakati akiizuru kambi ya wakimbizi ya Bambasi iliyoko kwenye eneo la [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tatizo la nzige nchi Mali na Niger linaripoitwa kusambaa kwa haraka baada ya wadudu hao waharibufi kuwasili maeneo ya kaskazini mwa nchi hizo mbili mwezi uliopita wakitokea Algeria na Libya. Nzige hao waliripotiwa kwanza kusini magharibi mwa Libya karibu na Ghat mwezi Januari mwaka huu na pia kusini mashariki mwa Algeria. Mwezi Machi shirika la [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa Utawala kwenye milki ya nchi za kiarabu imenzisha oparesheni dhidi ya watetesi wahaki za binadamu. Ripoti zinasema kuwa wanaharakati hao huwa wanadhulumiwa , wanazuiwa kusafiri , mikataba yao inasimamishwa na kufukuzwa nchini humo. S iku ya Jumatatu mwanaharakati mashuhuri Ahmed Abdul Khaleq [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya raia wa Somalia ambao wameikimbia nchi yao sasa imepita watu milioni moja kwa kujibu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Miongo miwili ya vita iliyoambatana na ukame wa muda mrefu na uhaba wa chakula ni kati ya masuala ambayo yamewalazimu wasomalia kuhamia mataifa jirani yakiwemo Kenya, Ethiopia, na Yemen. [...]
17/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani afrika wameanza mkutano wao wa siku nne jijini dar es salaam nchini Tanzania kujadilia kile kinachoitwa uchumi wa uvuvi wa samaki ambao unaripotiwa kukua kwa kasi lakini ukiandamwa changamoto ya kushamiri kwa uvuvi haramu. Kutoka DSM, George Njogopa ameandaa taarifa ifutayo inayoangazia mkutano huo ambao pia umejuisha wataalamu kutoka nchi [...]
17/07/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »