Nyumbani » 12/07/2012 Entries posted on “Julai 12th, 2012”

Vifaa vya kujenga amani vyahitaji kuboreshwa, laambiwa Baraza la Usalama la UM

Kusikiliza / baraza la usalama

Mwisho wa mzozo kawaida haumaanishi amani imewasili. Hii ndio mojawepo ya sababu za Umoja wa Mataifa kuunda Tume ya Kujenga Amani. Lakini ili ujenzi wa amani utendeke kwa njia inayofaa, ni lazima vifaa vinavyotumiwa katika ujenzi huo viendelezwe na kuimarishwa, vikiwemo kutoa ufadhili wa kifedha ufaao kwa mataifa husika, ili kuendeleza miradi ya kujenga amani. [...]

12/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tuzo ya Wangari Maathai yazinduliwa:FAO

Kusikiliza / tuzo ya Wangari Maathai

Shirika la Ushiirikiano Kuhusu Misitu (CPF), umetangaza tuzo ya Wangari Maathai, ambayo ni ya kwanza ya aina yake, kwa heshima na kumbukumbu ya mwanamke huyo mwenye uwezo wa ajabu, ambaye alikuwa mwanaharakati wa mambo ya misitu kote ulimwenguni. Tuzo hiyo ya jumla ya dola 20, 000, itatolewa kwa mtu ambaye amefanya mchango mkubwa katika kuhifadhi, [...]

12/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban Awataka Viongozi wa Rwanda na DRC Kukutana ili Kuzikabili Hujuma za Waasi wa M23

Kusikiliza / kundi la waasi la M23 nchini DRC

Huku akiwatolea mwito viongozi wa mataifa ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameweka wasiwasi wake juu ya kuendelea kuimarika kwa vikosi vya waasi vinavyoendesha machafuko mashariki mwa DRC. Kundi hilo la waasi lililojipachika jina la M23 ni muunganiko wa vikosi kadhaa ambavyo hapo awali vilikuwa [...]

12/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takriban Familia 84,000 Zakabiliwa na Njaa Madagascar:FAO

Kusikiliza / FAO Madagascar

Takriban jamaa 84, 000 nchini Madagascar zinakabiliwa na tishio la kutokuwa na usalama wa chakula, kufuatia hali mbaya ya hewa. Wimbi la chamchela lililotokea mwezi Februari lilisababisha uharibifu mkubwa, ambao umeshusha matarajio ya uzalishaji wa mpunga, ambao ndio chakula cha kutegemewa. Makadirio yaliyofanywa mara tu baada ya chamchela hiyo, yalionyesha kwamaba kati ya asilimia 50 [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuboreshwa kwa Mito na Kupanuliwa kwa Mbuga ya Sochi kati ya Mapendekezo ya UNEP

Kusikiliza / green-winter

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limetoa mapendekezo kadhaa yakiwemo ya kudumishwa maeneo ya uvuvi kwenye mto Mzymta na kupanuliwa kwa sehemu za mbuga ya Sochi nchini Urusi kama moja ya jitihada zinazoendelea za kuboresha hali ya kimazingira kabla ya mashindano ya msimu wa baridi ya Sochi mwaka 2014. Kundi la wataalamu wanaongozwa [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan ataka Kutekelezwa Mpango wa Amani wa Pande Sita nchini Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu Kofi Annan hapo jana amesisitiza umuhimu wa kutekelezwa kwa mpango wa pande sita wa amani ili kusitisha ghasia zinazoendelea nchini Syria na kusema kuwa jamii ya kimataifa ni lazima ishirikina kuhakikisha ghasia nchini Syria zimekomeshwa. Mapema leo Annan aliliarifu Baraza la Usalama la [...]

12/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mchango kwa eneo la Sahel kupitia Kampeni ya Mtandao Wazidi Matarajio yake

Kusikiliza / suala la njaa katika eneo la Sahel

Zaidi ya akina mama na watoto 15, 000 katika eneo la Sahel watapata vyakula bora ili kukidhi mahitaji yao ya lishe katika kipindi cha siku 100 zijazo, kufuatia kampeni ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ya kuchangisha pesa kupitia mtandao wa internet ilomalizika mwezi ulopita. Walioendesha kampeni hiyo wamesema matokeo yake yalizidi shabaha [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto Wenye Ulemavu Wako kwenye Hatari ya Kudhulumiwa

Kusikiliza / mtoto mlemavu

Watoto walio na ulemavu wako kwenye hatari ya kudhulumiwa mara nne zaidi kuliko wale wasio na ulemavu. Hii ni kwa mujibu wa utafiti kutoka kwa shirika la afya duniani WHO. Ripoti hiyo inasema kuwa watoto walio na ulemavu unaohusu matatizo ya kiakili na ulemavu wa viungo vya mwili wako kwenye hatari ya kudhulumiwa kimapenzi ikilinganishwa [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi wa UNRWA Wasaidiwa na Korea Kusini Kufungua Mawasiliano na Ulimwengu

Kusikiliza / gaza-korea

Serikali ya Korea Kusini, kupitia shirika lake la ushirikiano wa kimataifa (KOICA), imetoa tarakilishi 600 kwa wanafunzi wakimbizi wa Kipalestina kwenye Ukingo wa Gaza kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina, UNRWA. Tarakilishi hizo zitawasaidia takriban wanafunzi 30, 000 kupata mafunzo ya kompyuta na elimu ya mtandao. Katika hotuba yake [...]

12/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uhuru wa Watu Kufanya Mikutano Umebanwa sana nchini Kazakhstan:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Uhuru wa watu kukutana na kufanya maandamano umebanwa sana nchini Kazakhstan na sheria za mwaka 1995 zinapaswa kubadilishwa ili ziende sambamba na viwango vya kimataifa, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay. Kwa mujibu wa Bi Pillay, wanaoandaa maandamano na mikutano ya hadhara nchini humo huwajibika kwa usalama wa [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Zaidi Yawalazimu Zaidi ya Watu 200, 000 Kuhama Makwao DRC:OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Hali ya usalama imezorota zaidi kutokana na vitendo vya kundi la waasi la M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na kuwalazimu zaidi ya watu 200, 000 kuhama makwao, limesema shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA. Kwa mujibu wa msemaji wa OCHA, Jens Laerke, wengi wa watu waliohama makwao [...]

12/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031