Nyumbani » 11/07/2012
Entries posted on “Julai 11th, 2012”
Kusikiliza /

Mapigano mapya katika kipindi cha wiki moja iliyopita kwenye jimbo la Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, yamesababisha wakimbizi zaidi ya 5, 000 kuvuka mpaka na kuingia nchini Uganda, huku indadi isojulikana ya wengine wakihama makwao kama wakimbizi wa ndani, limesema Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani, UNHCR. Kufikia Jumatatu wiki hii, Shirika la Msalaba [...]
11/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Matumizi ya hali ya juu ya mawasiliono ya mitandao yametajwa na Umoja wa Mataifa kama fursa ya kihistoria ya kusaidia na kulinda watu, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Ripoti hiyo inaeleza jinsi mitandao ya mawasilino inaweza kuchangia habari kuhusu watu, [...]
11/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa kuunga mkono matumizi ya silaha na ghasia kwa upande wowote katika mzozo wa Syria kunaenda kinyume na dhamira ya maazimio nambari 2042 na 2043 na mpango wa amani wa Kofi Annan wenye vipengee sita. Katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama kuhusu utekelezaji wa maazimio [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Washiriki katika warsha ya udhibiti wa masuala ya maji iliyofanyika mapema mwezi huu mjini Almaty wamepitisha sheria na muongozo wa miaka mitatu hadi mitano za kuanzisha takwimu za udhibiti wa maji katika eneo la Aral Sea Basin huko Asia ya Kati. Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo ya Ulaya UNECE imesema inasaidia [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO, leo limetangaza kujitolea kuharakisha ukaguzi wake wa njia mpya na za zamani za kuzuia mimba, ili wanawake wengi katika nchi za kipato cha chini na zile za wastani, waweze kupata na kutumia njia nyingi na salama za bidhaa za kuzuia mimba. Shirika la WHO pia limeahidi kuzisaidia nchi kote ulimwenguni [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Afya ya uzazi limetajwa kuwa tatizo linaloongoza kwenye vifo vya wanawake waliohitimu umri wa kuzaa duniani huku wanawake 800 wakiaga dunia kila siku wakati wanapojifungua. Pia karibu vijana bilioni 1.8 huwa wanahitimu umri wa kuzaa bila ya wao kufahamu huduma wazohitaji ili kujilinda. Eneo lililo chini ya tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi barani [...]
11/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku masoko ya bidhaa za kilimo duniani yakiwa yametulia sasa, baada ya viwango vya juu zaidi vya bei mwaka uliopita, bei za bidhaa za chakula zinatarajiwa kusalia juu kwa muongo mmoja ujao. Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, hali hii [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tume ya kimataifa ya sheria na masuala ya HIV imezindua ripoti yake ya mwaka 2012 mjini New York inayopinga sheria zinazokandamiza haki za binadamu na vita dhidi ya ukimwi na kutoa mapendekezo ya kushughulikia tatizo hilo. Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae ambaye pia ni mjumbe wa tume hiyo amesema hivi sasa kuna ufuatuiliaji [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katika kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kufanyika juhudi zaidi kuwasaidia wale ambao wanahitaji zaidi fursa ya huduma ya afya ya uzazi. Akitoa ujumbe maalumu wa siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 11 Ban amezitaka nchi wanachama kuchukua hatua za kuziba pengo [...]
11/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »