Nyumbani » 10/07/2012
Entries posted on “Julai 10th, 2012”
Kusikiliza /

Idadi ya watu wasio na ajira katika eneo linalotumia sarafu ya Euro huenda ikapanda kutoka milioni 17.4 hadi milioni 22 katika kipindi cha miaka minne ijayo, ikiwa sera za pamoja hazitawekwa kubadili mkondo huo- imesema ripoti mpya ya Shirika la Ajira Duniani, ILO. Ripoti hiyo iitwayo: Utata wa ajira katika eneo la Euro, inaangazia jinsi [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Makundi ya kisiasa barani afrika yameanza mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kwa shabaha ya kujadilia nafasi ya vyama vya kisiasa pamoja na mwelekeo mpya wa ufadhili wa mafungu ya fedha. Wajumbe kwenye mkutano huo ambao umefunguliwa na makamu wa rais Dr Gharib Bilal wanatazamia kumulika nafasi ya vyama vya siasa nanma vinavyoweza kushiriki kwenye [...]
10/07/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya vita, Radhika Cooomeraswamy, ameupongeza uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, dhidi ya mbabe wa kivita Thomas Lubanga kama muhimu sana. Thomas Lubanga, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na [...]
10/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati kukaribia muda uliowekwa wa kufikia ukomo wa serikali ya mpito nchini Somalia, Umoja wa Mataifa umeelezea kile kinachopaswa kupiganiwa sasa na wananchi wa taifa hilo ambalo bado linashuhudia hali ya uhasama. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Augustine Mahiga amesema zingatio linalopaswa kutupiwa macho ni kuangalia hamta ya taifa hilo baada ya [...]
10/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wajumbe wawili maalum wa Umoja wa Mataifa wameshutumu vikali ukikaji wa haki za kitamaduni na haki ya kuabudu kaskazini mwa Mali kufuatia kuharibia kwa sehemu za kuabudu likiwemo eneo la kitamaduni la Timbuktu. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masusla ya haki za kitamaduni Farida Shaheed anasema kuwa vitendo hivyo vinaashiria hali ngumu kwa wenyeji [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya umaskini, maji na usafi, elimu, afya, chakula, mshikamano wa kimataifa na madeni ya nje, limeonya leo kuwa hakuna wakati wa kupoteza huku kukibaki tuu miaka mitatu kufikia 2015, ambao ni mwaka wa mwisho wa kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs). Kundi hilo limetoa [...]
10/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kazi ulimwenguni ILO limeonya juu ya kile ilichokiita ongezeko kubwa la watu ambalo matokeo yake yanadhihiri kwenye vita vya kuwania ubunifu na ukuzaji vipaji. Kwa mujibu wa ILO kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu duniani kunasukuma pia mbio za kuwania nafasi muhimu jambo ambalo limesisitiza kuwa linaacha kitisho juu ya mustakabala wa [...]
10/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kilichowaua zaidi ya watoto 50 nchini Cambodia, sasa kimetambuliwa kuwa aina hatari ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa mikono, miguu na midomo, ambao hupatikana hasa miongoni mwa watoto. Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema aghalabu ugonjwa huo huwa ni wenye athari ndogo na wenye dalili zisizo ngumu kutambuliwa. Lakini, kutegemea ni aina gani ya virusi vinavyohusika, [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mradi wa kibinadamu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wenye lengo la kuunga mkono mpango wa kuwafidia walioathiriwa na mafuriko nchini Pakistan mwaka 2010 kwa gharama ya dola milioni 1.1 unaelekea kumalizika. Mpango huo unaoongozwa na serikali unaojulikana kama Watam Card ulizinduliwa mwezi Machi mwaka 2010 na ndio mkubwa zadi kuwai kutekelezwa nchini Pakistan. [...]
10/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi kutokana na kuripotiwa mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye sehemu kadha za eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika ambapo maelfu ya watu kwa sasa wameathiriwa na ukame. Kati sehemu zilizoathirika zaidi ni pamoja na Niger, kaskazini mwa Mali ambapo mvua zinazonyesha zimesababisha hali [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imemhukumu mbabe wa kivita raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Thomas Lubanga Miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuwaingiza watoto kwenye kundi lake la waasi kati ya mwaka 2002 na 2003. Majaji kwenye kesi hiyo wanasema kuwa hata kama ni vigumu kubaini [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, amesema kuwa kutokuwepo taasisi thabiti kunaendelea kuwa kizuizi katika kutekeleza haki na uongozi wa kisheria nhcini Kyrgyzstan. Bi Pillay amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bishek, wakati wa ziara yake nchini humo. Amesema serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa kuna uajibikaji kwa ajili ya [...]
10/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC, imesema inatiwa wasiwasi na hali ya mambo inayoendelea kujiri sasa huko mashariki mwa taifa ambako vikosi vya waasi m23 vinaendesha mashambulizi na uvamizi wa raia. Msemaji wa vikosi hivyo MONUSCO amesema makundi hayo ya waasi yanaripotiwa kupiga hatua kusonga mbele kwa kutwaa maeneo muhimu [...]
10/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusu mzozo wa Syria, Kofi Annan, amesema Iran inatakiwa kuhusishwa katika kutafuta suluhu kwa mzozo wa Syria. Bwana Annan ambaye amekuwa Tehran kufanya mazungumzo na viongozi wa Iran kuhusu mzozo wa Syria, amesema mchakato mzima wa kisiasa ambao unatakiwa kuwaleta wahusika wote pamoja [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeelezea hofu yake kuhusu hali ya afya katika kambi za wakimbizi zilizopo Sudan Kusini, na hasa uwezekano wa mkurupuko wa magonjwa katika kambi hizo. Kwa mujibu wa UNHCR, hali katika kambi za wakimbizi imeendelea kuzorota katika kipindi cha siku chache zilizopita, kufuatia idadi kubwa ya wakimbizi [...]
10/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »